Kwanini NSSF isiwe na tawi la bank kusaidia wateja wake?

Great Sir!!!

Mkuu huyo asikusumbuwe ni malimbukeni katika taaluma...wazo lako hata Dr Dau alipendekeza Mkuu watu wenye upeo na mawazo mbadala Taifa linawahitaji sana ...huyo jamaa hajui hoja yako
 
Njoo Arusha nikuajiri ...wewe elimu yako ni kiwango cha creche...ukiendesha vitz na kamshahara kidogo unajiona matawi ya juu....

watu tunamakampuni mpaka Namibia wewe unaleta ubepari wa kumiliki vitz...

Niko hapa Picnic nagonga Kitu cha Namibia baridiiii ...kapuro wewe
 
1. Huduma za Kibenki Nchini zipo kwa mujibu wa sheria na zinadhibitiwa na BOT.

2. NSSF ipo kisheria na majukumu yake yameainishwa kwenye sheria kuwa ni kusajili wanachama, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao.

3. Kwa hapo tu ni wazi kuwa NSSF hawezi kufanya shughuli za kibenki.

4. Kingine cha muhimi, NSSF kwa sasa haishughuliki na watumishi wa umma (kama nimekuelewa mleta mada). Badala yake ni Shirika linaloshughulika na wafanyakazi walio kwenye sekta binafsi pekee.
 
Kama wamewekeza Kwenye mabenki si ni biashara tayari?why not it's own bank?
Kwenye principles za social security protection hizi companies zinatakiwa kuwekeza kwenye Govt bonds, real eastate na capital markets. Kufanya kazi ya benki moja kwa moja ni kuondoka nje ya sheria iliyowaanzisha. And hiyo ndiyo best practice world wide.
 
kijana sio muelewa! sjui anajua hyo benk ya nssf ishaanzishwa..! umeenda far sana, kwani ukisoma comment ukaelewa unahisi utachelewa kuandika.. πŸ™‚
 
great thinkerπŸ‘
 
Mzee nssf walikuwa wanajenga majengo sana tu, pia wamejenga daraja la kigamboni
usingemuelewesha hao huwa wanapenda kubishana tuu! ukitutumia muda kuwaelesha utaishiwa bando.. πŸ™„
 
wazo zuri
 
Kwa serikali ya sasa unachokisema hakiwezekani na hakiwezi kuwa..
NSSF ni pesa ambazo kwanza huwa hazichangishwi tu zikakaa pale kisubiri watu wastaafu, bali serikali inazichukua inazifanyia kazi palipo na mapungufu alafu inaaanza kuzirejesha mdogo mdogo kulingana na idadi ya wastaafu...kwa hiyo ukisema iwe bank maana serikali haiwezi kufaidika nazo kitu ambacho ni kigumu sana serikali kukubali ajenda kama hiyo
 
Sidhani kama miradi inajengwa na NSSF.lete ushahidi.

😁😁😁 Bwana mdogo unachekesha sana.
Kuna vitu vingine haviitaji ushahidi wazi hivo kama unavyotaka, kuna vitu vingine ni siri ya serikali, serikali inapochukua hela za NSSF na kuzitumia kwenye miradi mingine usidhani kwamba lazima iwatangazie wateja wake.

Kubali kuwa hizo hela hazichangishwi zikaa tu pale bank, kuna mahali serikali inazihitaji kwa dharura kufanyia mambo yake na huzirejesha kidogo kidogo kulingana na wahitaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…