Kwanini Nyalandu alimgaragaza kwa kura za kishindo kwenye kamati Kuu ya CHADEMA aliyekuwa mshindani wake Tundu Lissu?

Sidhani kama nyslandu anaweza akawa na jambo lolote la maana lakuongea zaidi ya kurusha vijembe na porojo za ovyo kwa chadema, porojo ambazo tumeshazizoea toka kipindi cha wale waunga juhudi walivyokua wanashamiri kuunga juhudi nakupata air time kwenye media lakini bado ulikua ni ujinga tu kama ambao nyalandu anafanya sasa.

Siasa za hivyo zilishapitwa na wakati vinginevyo tukubali kua wanasiasa wetu hawana uwezo au mawazo mapya yakuisukuma nchi mbele zaidi yakupiga mipasho isiyo na tija kwa taifa.Hii tabia ya wanasiasa kuhama chama alafu anakuja na mipasho ni ujinga wa kiwango kikubwa sana kwenye siasa za nchi hii.

Ifike mahali wanasiasa wetu wakue kwasababu matokeo ya hili tatizo ndo inapelekea mtu anakua kiongozi ofisi fulani hatatui changamoto za ofisi husika kipindi chote cha utumishi wake, siku anapotoka ndo anakuja na drama zakujifanya ofisi ilikua na mapungufu. Ata kama tunafanya kwa ajili ya matumbo yetu tujaribu ata kidogo kukua kifikra.
 
Lazaro Nyalandu alimgaragaza Tundu Lisu kwenye kura za kamati kuu.!

Huyu mzee wa MIGA ,mwanasheria a Acacia anaaminika na nani sasa kama hadi kamati kuu anashindwa kura??
Kwa kweli nyie akili zenu sijui ziko kwenye nini maana kama ni kwenye ubongo basi ni wa tope!
Ukiangalia hapa Nyalandu zina mtosha kweli? Au na nyie mnaoshabikia ndio walewale?
 
Kwanza Naomba radhi sana kuleta andiko hili hapa JF , mimi ni miongoni mwa watu waliosaidia Nyalandu kufika alipofika ndani ya Chadema (Sitafafanua ) , Nyalandu hakutakiwa kujibiwa na mimi , kwa sababu kwenye siasa za Upinzani ni mwepesi sana kwangu , mimi si Size yake hata chembe , bali nimelazimika kujitokeza ili kunyoosha baadhi ya mambo ili kuondoa upotoshaji wake .

Kwa Mujibu wa Nyalandu mwenyewe ni kwamba wajumbe wa Kamati kuu walikuwa 30 , Lissu alipata kura 24 , Nyalandu hakusema amepata ngapi na wala kura zilizoharibika hazifahamiki .

Sasa kwa hesabu ya kiwango cha chini kabisa cha chekechea aliyepata kura 24 kati ya 30 aweza kuwa amegalagazwa ?



Waandishi wa Habari wa Tanzania mnapaswa kuwa na akili hata ya kuvukia barabara , kwa hesabu hii mlishindwa kumuuliza Nyalandu awaonyeshe jinsi alivyomgalagaza Lissu ? Je ni kweli kwamba mlipewa bahasha za Khaki kabla hamjaanza mahojiano kama mmoja wenu alivyovujisha mitandaoni ili msiulize maswali magumu ?

MUHIMU : Ikumbukwe kwamba hatuna ugomvi na wanaohama Chadema na wala hatujawahi kukataza yeyote kuhama , bali wahamaji wawe wakweli kuhusu kuhama kwao , waseme wazi kwamba wanatafuta fursa , wasilete uongo wa kijinga na uongo ni dhambi na ifahamike kwamba MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI
 
Nyalandu alikuwa hana ubavu wa kumshinda Tundu Lissu, yeye ni wa kuja tu hapa asingeweza kuaminiwa hata kidogo. Yeye awe mwanaume aseme tu ukweli kuwa aliondoka CCM kuogopa, sasa hayupo tena CCM ndiyo maana amerudi. Hayo matango pori yake awalishe wenzake wa CCM.
 
Mpigie simu mhojiane, then lete mahojiano yenu hapa, otherwise you and him wote WARONGO
 
Nilivyoelewa Mimi ni kila mgombea anapigiwa kura za ndio na hapa then matokeo yanalingahishwa baadae, so Nyarandu alipata zote then lisu alipata hizo 24.

Mshindi alikua nyarandu. Hongera sana nyarandu kutoboa ugenini
 
Topic Lissu alipata kura 4 ndani ya kamati kuu.

Got none to do with Magufuli...

Lets discuss kura 4[emoji16][emoji16]

Usitutoe nje ya mada kuu
Tangia Uhuru Tanzania haijawahi kupata rais wa hovyo kama marehemu dikiteta magufuli, dikiteta magufuli asingeweza kupata kura hata moja mbele ya Membe.
 
Nilivyoelewa Mimi ni kila mgombea anapigiwa kura za ndio na hapa then matokeo yanalingahishwa baadae, so nyarandu alipata zote then lisu alipata hizo 24.
Mshindi alikua nyarandu. Hongera sana nyarandu kutoboa ugenini
Kumbe ni ulivyoelewa wewe, wenzako tumeelewa tofauti.

Nyalandu kumpita kura Lissu hata mtoto mdogo hawezi kukubali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…