Kwanini nyumba nyingi Tanzania zina mabati marefu?

Mabati si marefu, paa ndilo refu. Urefu wa paa unasaidia paa kutiririsha maji na umande hivyo bati hukauka haraka na kutopata kutu haraka, ndiyo faida yake.
 
Sijui Afrika utakuta anafuga msukule.
Ulaya utaona hilo bati refuu kumbe juu ni store kuna mazaga kibao miaka na miaka.
Na kitanda kipo saafi siku mkewe akicheza wekundu akatibuka.
Jamaa anapiga ngazi analala huko juu kimya kimya.
 
Elimu elimu elimu ..urefu wa paaya bati una faida zifuatazo ..
1)kufanya nyumba isiwe na joto
2)kufanya bati au paa kudumu muda mrefu zaidi kutokana na mvua na jua
3)kufanya paa lisipate kutu kirahisi kutokana na kutuama kwa vitu kama vumbi au majani.
4)kupendezesha jengo.
 
ni urithi wetu wa Christianity, paa la namna hiyo ni Christian symbol, angalia Kanisa linavyojengwa yote (karibia) yako hivyo ila non-Christians wanatumia flat roof.

flat roof ni antichrist na satanic, mnara wa babeli ulikuwa na flat roof ...
Kijakazi katika ubora wake wa kuharibu topics.
 
Elimu Elimu Elimu...urefu una kikomo ndugu.Kwanza yale mapaa marefu ambayo mleta mada amemaanisha ambapo mapaa ni marefu kuliko boma kamwe nyumba hazipendezi. Vile vile ni rahisi kuezuliwa na upepo mkali. Kuna slope standard sio tu kujinyanyulia ,unahatarisha usalama .
 
Now it s part of our culture
 
Yule Msukuma aliyenipauliwa aliniharibia Sana. Alinijia na Swaga za French sijui English Styles akaniingiza Mjini.

Paa refu kama vile aenda na Artemis II
 
Uko sahihi Paa refu kuliko Boma ndio nyumba inakuwa Konyagi. Yangu ni Panasonic Sana, so urefu umebalance
 
kuna fundi umeme aliitwa nyumbani kwa tajiri mmoja kuchek shot akapanda darini fresh duh anakwambia alikuta kwenye makench ya angle za paa pamepigwa ngozi za kondoo nyingi na mafuvu ya vichwa vya binadamu
Hahaha hii Chai
 
Hasa mkoa wa mbeya ni VURUGU!?
Sawa, kama hoja ni kupunguza joto, je mikoa kama Arusha na Mbeya ambako hali ya hewa ni ya baridi kiasi, kwa nini nako mtindo huu umeenea sana? Hapo ndipo naona kuna mchango mkubwa wa mtindo wa usanifu kuliko sababu ya hali ya hewa pekee.
 
Huwa najiuliza paa linazidi vipi urefu wa Boma? Angalia mapaa ya majengo ya serikali. Yote ya wastani kwasababu wanafuata vipimo vya kitaalamu. Haya marefu kama ghala ni idea za mafundi na wamiliki wasiojua wanawasikiliza mafundi. Mimi huwa nawaambia sitaki paa refu,nataka kipimo cha majengo ya serikali. Utawasikia boss nyumba hairapendeza nawaambia ndio nataka isipendeze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…