Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa Kanisa Katoliki?


PICHA: Padri Martin Luther
​
Padre Luther alikuwa miongoni mwa Mapdre wenye karama nyingi ndani ya Kanisa Katoliki wakati wake, yeye alikuwa na Madai mengi sana juu ya mapungufu kwa kanisa. Hata hivyo madai yake mengi hayakuwa na msingi wowote.

Moja ya madai yake ilikuwa ni kuondoa kibali cha kwamba baada ya kuungama muumini asipewe stakabadhi ya kuonesha ameungama kwa kuwa kitubio ni siri ya mtu. Hili lilifanyiwa kazi. Mengine ikiwemo kurekebisha mfumo wa sala ya Kanuni ya Imani. Na mambo mengine mengi ambayo alipojibiwa, yeye hakuridhika pamoja na kueleweshwa vya kutosha. Alikuwa ni Great Thinker sana.

Mbaya zaidi alipokuja kusababisha mpaka akajitenga na kanisa ni kitendo cha kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ikiwemo pia kupunguza baadhi ya mistari kwenye vitabu kama cha Esta na cha Danieli.

Aliondoa vitabu vya Deutrokanoni na vingine baadhi na kuwa jumla ya vitabu 7 vilivyotolewa kwenye Biblia. Na kila kitabu alikuwa na sababu yake aliyoibainisha. Kimsingi alipata wafuasi wengi wa kumuunga mkono hoja yake hasa wale ambao walikuwa wanatafuta njia ya kuchuma pesa kiulaini. Na hapo Biblia mpya ilianza yenye Vitabu pungufu.

Na ndio maana leo watu hawaujui Ukristo vizuri na wanakinzana bila kujua historia ya kanisa. Watumishi wengi wa Mungu hasa hawa wa kileo wasiojua historia vizuri wao kila kitu wanapinga. Sio kosa lao Bali ni kosa la kutokujua historia ya kanisa.

Matumizi ya Ubani yalipingwa sana, na hapa ilikuwa ni kuondoa idadi ya waelewa. Kutokana na watu wengi walikuwa wamegeuka kama waganga kila mapepo ya kiwakabili walitumia ubani kuyafukuza na yalikimbia, lakini watu walijisahau kusali na kuomba na hata kufika ibadani ikawa nadra maana wanajua kujiponya kuondokana na majini na wachawi. Hapa Padre Luther na wenzake wakapiga marufuku matumizi ya ubani na kuwa sihi wakazanie Neno zaidi.

Hapa walichotakiwa kufanya ni kuliishi Neno la Mungu na wakati wa ibada basi ubani uchomwe kama Mungu alivyo agiza.

Luther na wenzake lengo lao lilikuwa ni biashara hapo baadae na kimsingi mpango huo ulifanikiwa. Na ndio maana mpaka Leo watu wametawaliwa na mfumo wa majini katika maisha yao kwa kuwa wamefungwa akili ya kujitambua na wanaamini maneno ya mdomoni na sio Maandiko ya Biblia kama yanavyosema.

Nimengi sana ya kujifunza lakini kwa Leo naishia hapa.
​

deogratius Nalimi Kisandu.
1. 1. 2017.


MAONI YA WADAU
-------------
-------------
-------------
-------------
-------------
-------------
--------------
--------------
--------------
Deogratius Kisandu,

DOCUMENYARY HII IMEJIBU



-------------
 

Ok9

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Posts
4,554
Reaction score
4,171
Kwanza tunaamin hiki kitabu kikiandikwa na MUNGU kupitia mkono wa binadam...na mara ya kwanza kilkuwa na vitabu vingi... lkn zinazochapwa kwa sasa zimenyimwa baadh ya vitabu... na wala sisikii vikitumika ktk mafundisho.... mf SIRA...BARUKU..SUSANA...BELI NA JOKA..WAMAKABAYO..

JE hii n kwan nn....au vilionekana havifai kwa mafundisho ya sasa....?
 
Imesahaulika hii jaman
 
Biblia inayotumiwa na Kanisa Katoliki ndio Biblia yenye vitabu vyote vilivyokubaliwa toka vitabu vya Biblia vilipokusanywa na kuwekwa pamoja.Martin Ruther ndio aliyekuja kukataa baadhi ya vitabu hivyo kuja na toleo ambalo lilitumika na waprotestant hadi kifo chake ndio wakarudisha baadhi.
 
Vitabu vingine vilikataliwa toka mwanzo kabisa na havijawahi kuwa sehemu ya Biblia......
 
Pia mkuu Mushi92 amini Yesu alilipa Kanisa mamlaka na analiongoza yeye mwenyewe hivyo fahamu vizuri mafundisho ya kanisa ambalo ndio msingi wa ukweli na kama hukubali kwavile wewe si Mkatoliki soma maswali haya (niliyokopi sehemu) ili uzidi kufikirisha kichwa ....


(1) The Bible was not put under one cover until 397 AD at the Council of Carthage. It took months to hand copy the Bible. Prior to the Bible being put under one cover, who was the authority figure for the early church? Remember, the Bible did not exist as we know it today. There is NO denying the fact that authority was the CHURCH--not the Bible.

(2) How did the early Christians each own a Bible if the printing press wa...sn't developed until the 1500's? Even after the printing press was developed by a Catholic man in Germany, how many Christian could afford to own a Bible?

(3) Why does JESUS state the final authority is the CHURCH in Matthew 18:15-17?

(4) Where in the Bible does it state that the "Bible" is the only authority for Christians?

(5) How did the majority of the people who were uneducated read the Bible prior to 1500 and even to this day?

(6) What is the pillar and foundation of truth (1 Tim 3:15)?

(7) What books of the Bible did Jesus write?

(8) Where in the Bible does Jesus command the Apostles to write?

(9) How do you know that your interpretation of the Bible is correct?

(10) How did the Bible know what books to include under its cover?

---The only logical conclusion is believing that the Bible as our only guide is unbiblical!! The CHURCH came FIRST!!
 
Last edited by a moderator:
Haya leo nimeona tujifunze na mambo ya kiimani kidogo juu ya Kitabu kitakatifu. Tofauti ya vitabu 7 ni ya kihistoria. Kabla ya karne ya 16 Wakristo wote walitumia Biblia yenye vitabu 73 lakini mwanzilishi wa dhehebu la Kilutheri duniani Martin Luther alianzisha kampeni za kuviondoa vitabu 7 akidai havina pumzi ya Mungu.

Tangu hapo Wakristo wasio wakatoliki hawatambua vitabu hivi 7 kama ni sehemu ya Maandiko Matakatifu. Navyo ni: Tobiti, Yudithi, Hekima ya Solomoni, Yoshua Bin Sira, Baruku, 1&2 Makabayo.

Michango ya ufafanuzi inakaribishwa.
 
Martin Luther alishapata cheo cha , 'uaskofu' wakati huo. Dhana kwamba alifuta vitabu 7 napata shida mamlaka hayo aliyapata wapi? Mnyonge mnyonge lakini haki yake mpe

Mkuu kwa hili huna data.... Martine hakuwa Askofu, alikuwa Padre na miongoni mwa sababu zilizomuondoa kwenye kanisa Katoliki ni hili la Uaskofu, alipinga hairakia ya Kanisa na vyeo kama Uaskofu, Upapa na mengineyo. Sema tu mengi aliyoyapinga aliishia kuayatenda akiwa kwenye kanisa lake. Mengine ni suala la Useja, hakutaka kabisa kulisikia na alipoondoka aliondoka na Mtawa wa kike aliyeishia kuwa mkewe.

Mambo ni mengi sana na yanahitaji muda wa kutosha. Lakini niseme tu kwamba "siyo kila alilolipinga lilikuwa baya" mengine aliyapinga kihalali kabisa japo njia aliyoitumia haikuhalalisha kitendo chake!!!

Pili, Biblia za wapeotestanti na wapentekoste zina vitabu 66 wakati biblia ya Wakatoliki ina vitabu 72. Hili lilitokana na kuwa baadhi ya yaliyomo kwenye vitabu hivyo (deuterokanoni) vinapingana na mafundisho yao. Sababu nyingi ni za kibinadamu tu!!! Hili lilikuwa rahisi sana kwake kwani suala zima la "Utaifa" liliingizwq kwenye huu mchakato wa Luther kujiondoa kanisa, matokeo yake kwa vile alikuwa Mjerumani, dhehebu lake likawa "dini dora" ya Ujerumani, katika hali kama hii, ni rahisi kwa uwezo wa kifedha kuchapisha Biblia zenye vitabi 66 na kuviondoa vile vingine!!!!
 
Naona hujazungumzia cheo cha papa na mamlaka yake, umeshau hoja ya Marton Luther ya mamlaka milyo mpa maria kuwa muombezi wenu
Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao wanawapotosha, hawaijui biblia
 
Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao wanawapotosha, hawaijui biblia
Duh kaaazi kweli kweli hapo ndo mlipo mpa cheo binadamu mwenzenu awe mwombezi. mmesahau kwamba mariam na yeye ni binadamu kama niniyi na alishakufa anasubiri ufufuo siku ya mwisho.. sasa sijui nani kawadanganya kwamba maria yuko hai. Au ni katika kitabu gani kimemtaja Mariam Kwamba yi hai ambapo anaweza kusikia maombi yenu
 
Biblia inasema Bikra Maria ataitwa mbarikiwa, na dunia itamsifu kuwa yeye ni mbarikiwa. Bikra Maria kwa mujibu wa kumbukumbu za kanisha hakufa, alipaazwa. Ujui historia, huyu mama ni the special, hata waprotestant wakimtupa sisi Wakatoliki tutaendelea kutimiza unabii kwa kumuita mbarikiwa
 
alipazwa? lete andiko acha hizo historia za kanisa mlizo mezeshwa na zilizotungwa na watu ndio maana Luther mlishindwa kujibu hoja zake..

Haya lete andiko la kupazwa kwa Maria
 
Mbona hujaelezea jinsi ilivyokuwa watu wanauziwa vyeti baada ya kufanya dhambi kama uzinzi. eti kwa kununua cheti hicho atakuwa amesamehewa. Then anarudi tena anafanya as long as anapesa za kununua vyeti vya msamaha wa dhambi.....[HASHTAG]#hujui[/HASHTAG] tu hayo makasri ya huko Roma yamejengwaje.

njoo tukujuze..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…