Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa Kanisa Katoliki?

Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa Kanisa Katoliki?

Kitaja,
9 Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.

Ufunuo wa Yohana 6 :9

10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?

Ufunuo wa Yohana 6 :10

11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao.

Ufunuo wa Yohana 6 :11

Soma kwa utulivu bila mihemko. Kwavile mnapenda sana nukuu labla ubishane na maandiko sasa. Ndugu kama wewe ni Mkristo na huamini ukifa katika hali ya neema huendi direct mbinguni basi wewe tumaini lako ni bure ....nenda kajifunze upya maana ya ufufuo wa wafu ....
 
Kuabudu maana yake ni kufanya ibada kwa kitu ambacho unaamini kuwa ni muweza wa yote/ muumbaji, swali je wakatoliki katika ibada wanazitukuza zile sanamu na kuziabudu au huwa ni ibada kwa Mungu?? Kama wanaabudu sanamu mbona wakianza ibada kuna sala wanasali WANASADIKI KWA MUNGU MMOJA.....WANASADIKI KWA YESU KRISTO...... Na PIA WANASADIKI KWA ROHO MTKTIF.... Mbona hawasemi wanasadiki kwa sanamu...
Iweje muwalazimishe kuwa wanaabudu sanamu???

Shukrani
Porojo nyingi za nani? Kama hawaabudu sanamu kuna haja gani ya kuweka sanamu kanisani? Nipe jibu hapo.
 
Porojo nyingi za nani? Kama hawaabudu sanamu kuna haja gani ya kuweka sanamu kanisani? Nipe jibu hapo.
Good, umeshasema wameziweka kanisani... Ishu unaelewa kwanza maana ya kuabudu au unakurupuka usingizini??? Wenyewe wanasema wanaamini kwa Mungu mmoja aliyezifanya mbingu na nchi we unawaforce wanaabudu sanamu....kama kweli wanaabudu sanamu waje hapa waseme wenyewe...
Mbona wewe unamswalia mtume lakini hawakuingilii....Jaman ombeni neema ya kuijua kweli na kweli itawawek huru..
 
Unawazimu..?
Pole sana mkuu....,hawa jamaa umejitahidi sana kuwaelewesha lkn wanjitia manunda.....!ila natumaini wameelewa tatizo ni ununda wao

Hv huyu Kitaja ebu atuambie William Miller alitumia kifungu gani ktk biblia takatifu kutabiri mwisho wa dunia 1844.......?alafu tumpe maudhui ya hivyo vifungu alivyovitoa....!

Tafsiri zile za upotoshaji za 1844 za bwana Miller ndizo hizi anatuletea leo mjukuu wake bwana Kitaja,nimemuomba bwana Kitaja ebu nipe andiko alilotumia Miller kutabiri mwisho wa dunia na kama hajui aseme........?kukwepa swali sio ishu....
 
MTAZAMO,
Naona unaukaribia ukweli kwa kuwa unapenda kutumia maandiko katika hoja zako.wenzio wengi hawapendi kabisa nukuu za Biblia bali hupenda tusikilize hadithi zao za kutunga.

Sasa nirejee kwenye hoja na nukuu ulizotuwekea hapa.
Nukuu ya Ufunuo 6:9-11 inazungumzia hatima ya watakatifu waliouawa kwa ajili ya Neno la Mungu.Kitabu cha Ufunuo kinatumia lugha ya mafumbo na inahitajika uongozi wa Roho Mtakatifu kuelewa kitabu hiki. Hizo roho zonazolia zinathibitisha kuwa Mungu ni mhukumu wa haki na atawapatia haki watoto wake waliouawa kwa ajili yake. Kwa ufupi mafungu haya humaanisha kwamba Mungu anatambua mateso ya wafia dini na muda si mrefu atalipa kisasi.Mamlaka ile ile iliyohusika kutesa watakatifu wa awali itapata nguvu tena na kuendeleza mateso yake kwa watu wa Mungu wanaotii amri za Mungu."

Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu,nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao,watakaouawa vile vile kama wao." Ufunuo 6:11. Fungu hili huthibitisha kuwa kuna mateso zaidi yatakuja kabla ya Yesu kurudi.Lakini watakatifu wanafarijiwa kuwa bado muda kidogo, wapewe haki yao hii ikiwakilishwa na nguo ndefu, nyeupe.Vazi huwakilisha haki ya Kristo.

Hizo roho pia zinawakilisha hukumu ya upelelezi inayoendelea kwenye madhabahu mbinguni, hao wafia dini wamehakikishiwa wokovu na Mwanakondoo aliyekufa kwa ajili yao. Hata wale watakaouawa kwa namna ile ile pia fungu hili linawahakikishia wokovu. Mamlaka ya kipapa ilitesa watu wa Mungu waliokuwa wamesimama katika kweli.Wale watakatifu waliouawa na kanisa katoliki ndio husemwa hapa.

Hivi karibuni, mamlaka ya kanisa katoliki itarudi kwa nguvu kubwa chini ya new world order.Mateso yatarejea kama zamani." Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, walio huru kwa watumwa,watiwe chapa katika mkono wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao.Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza,isipokuwa ana ana chapa ile, yaani jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.

Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo maana ni hesabu ya kibinadamu.Na hesabu yake ni mia sita,sitini na sita".Ufunuo 13:16-18.
 
Hv huyu Kitaja ebu atuambie William Miller alitumia kifungu gani ktk biblia takatifu kutabiri mwisho wa dunia 1844.......?alafu tumpe maudhui ya hivyo vifungu alivyovitoa....!
Badala ya kukupa jibu, ataingiza mambo ya B/Maria, wafu..nk.nk.

Ni kwamba hakuna msabato atakayeweza kukupa jibu kuwahusu kina Miller, Joseph Bates na wenzake
 
Mateso yatarejea kama zamani." Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, walio huru kwa watumwa,watiwe chapa katika mkono wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao
Aliyekuambia yatarejea kama zamani ni nani ..? Yatarejea lini..? Kwa watu gani...? Bado mnendelezs zile tabiri zenu za kuzimu za kina Miller na EGW...?

Chapa gani hiyo unayoongelea kwa dunia hii ya sasa ..?? Unatuletea mambo ya lesson hapa...?
 
Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo maana ni hesabu ya kibinadamu.Na hesabu yake
Unaelewa dhima ya kitabu cha Ufunuo..? Unafahamu kiliandikwa kuwahusu watu gani..? Unadhani mimi kukuita unawazimu nilikosea..?


Kwanini unatuletea mafundisho ya Miller hapa..?
 
Ufunuo 6:11. Fungu hili huthibitisha kuwa kuna mateso zaidi yatakuja kabla ya Yesu kurudi.
Biblia inatuambia hakuna ajuaye siku wa saa ajaye mwana wa Adamu... Yesu anarudi lini...?

Lakini watakatifu wanafarijiwa kuwa bado muda kidogo
Watakatifu gani hao unaongelea wewe...?

Unataka kuturudisha kule mwaka 1844(Great disappointment)...

Nakuuliza tena unawazimu..?
 
Kitabu cha Ufunuo kinatumia lugha ya mafumbo na inahitajika uongozi wa Roho Mtakatifu kuelewa kitabu hiki. Hizo roho zonazolia zinathibitisha
Yes! Kina tumia mafumbo ambayo maana yake umeshang'amuliwa toka zamani..

Apokalpse ya Yohana haijawahi kuekezea mambo ya nyakati za sasa kamwe...

Ndio maana nimekuuliza unajua dhima ya kitabu hiki..?

Unataka tuanze kukichambua tukianfalia ni lini kiluandikwa, kiliwahusu kina nani...? Walengwa wa kitabu hiki walikuwa wanaishi ktk mazingira gani..?

Bila kuyajua haya utaingia chaka na kuturudisha kwwnye mafundisho pitofu ya William Miller na Ellen G White...

Njoo tujadiliane hapa...
 
Naona unaukaribia ukweli kwa kuwa unapenda kutumia maandiko katika hoja zako.wenzio wengi hawapendi kabisa nukuu za Biblia bali hupenda tusikilize hadithi zao za kutunga.

Sasa nirejee kwenye hoja na nukuu ulizotuwekea hapa.
Nukuu ya Ufunuo 6:9-11 inazungumzia hatima ya watakatifu waliouawa kwa ajili ya Neno la Mungu.Kitabu cha Ufunuo kinatumia lugha ya mafumbo na inahitajika uongozi wa Roho Mtakatifu kuelewa kitabu hiki. Hizo roho zonazolia zinathibitisha kuwa Mungu ni mhukumu wa haki na atawapatia haki watoto wake waliouawa kwa ajili yake. Kwa ufupi mafungu haya humaanisha kwamba Mungu anatambua mateso ya wafia dini na muda si mrefu atalipa kisasi.Mamlaka ile ile iliyohusika kutesa watakatifu wa awali itapata nguvu tena na kuendeleza mateso yake kwa watu wa Mungu wanaotii amri za Mungu." Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu,nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao,watakaouawa vile vile kama wao." Ufunuo 6:11. Fungu hili huthibitisha kuwa kuna mateso zaidi yatakuja kabla ya Yesu kurudi.Lakini watakatifu wanafarijiwa kuwa bado muda kidogo, wapewe haki yao hii ikiwakilishwa na nguo ndefu, nyeupe.Vazi huwakilisha haki ya Kristo. Hizo roho pia zinawakilisha hukumu ya upelelezi inayoendelea kwenye madhabahu mbinguni, hao wafia dini wamehakikishiwa wokovu na Mwanakondoo aliyekufa kwa ajili yao. Hata wale watakaouawa kwa namna ile ile pia fungu hili linawahakikishia wokovu. Mamlaka ya kipapa ilitesa watu wa Mungu waliokuwa wamesimama katika kweli.Wale watakatifu waliouawa na kanisa katoliki ndio husemwa hapa. Hivi karibuni, mamlaka ya kanisa katoliki itarudi kwa nguvu kubwa chini ya new world order.Mateso yatarejea kama zamani." Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, walio huru kwa watumwa,watiwe chapa katika mkono wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao.Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza,isipokuwa ana ana chapa ile, yaani jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo maana ni hesabu ya kibinadamu.Na hesabu yake ni mia sita,sitini na sita".Ufunuo 13:16-18.
Unajificha kwenye chaka la rohomtakatifu na chuki mlizokaririshwa dhidi ya Kanisa katoliki. Huo ufunuo uliosoma, unasema mwisho wa dunia utakapokaribia Kanisa la Kristo litaungana na kuwa moja. Ilimaanisha nini?
 
uongozi wa Roho Mtakatifu kuelewa kitabu hiki. Hizo roho zonazolia zinathibitisha kuwa Mungu ni mhukumu wa haki na atawapatia haki watoto wake waliouawa kwa ajili yake.
Hivi wewe unahitaji Roho Mtakatifu au Manuscript za Ellen G White, Joseph Bates na Hiram....?

Wasabato tangu lini mkamjua Roho Mtakatifu..?
 
Back
Top Bottom