Yesu ni Mungu....Mungu anamuombea nani.. na kwa nani...???
Huwezi kuelewa siri hii ya ukombozi kupitia kwa Yesu Kristo. Yesu ni Mungu ndiyo, na ni mwandamu pia ndiyo maana alitwaa mwili huu unaokufa, kwani Mungu hapatikani na mauti,Lakini Mungu alimfufua katika wafu. Ndiyo maana Paulo anasema yu hai siku zote atuombee.
Pitia hapa Waebrania 7:24-26.
24 bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.
25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao
wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
26 Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;
Soma tena 1 Yohana 2:1-2.
1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi.
Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.
Bado unabisha kuwa Yesu ni mwombezi wetu kwa Baba?