Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa Kanisa Katoliki?

Hao watoto na Yusifu unaweza wataja..?
Yakobo, Yosefu, Simoni, Yuda na dada zake.
mathayo 13.
53 Yesu alipomaliza kusema mifano hiyo alitoka mahali hapo, 54 akaenda kijijini kwake. Huko akawa anawafundisha watu katika sunagogi hata wakashangaa, wakasema, "Huyu amepata wapi hekima hii na maajabu? 55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?" 57 Basi, wakawa na mashaka naye. Lakini Yesu akawaambia, "Nabii hakosi kuheshimiwa, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani mwake!" 58 Kwa hiyo, hakutenda miujiza mingi pale kwa sababu ya kutoamini kwao.
 
Martin Luther alishapata cheo cha , 'uaskofu' wakati huo. Dhana kwamba alifuta vitabu 7 napata shida mamlaka hayo aliyapata wapi? Mnyonge mnyonge lakini haki yake mpe
Mkuu Luther hakuwa askofu!!
 
.
*uandishi wako unaonyesha kua huijui historia ya kanisa,,,
kwa mfano huzungumzii sala kwa bikira maria na cheo chake cha umalkia, ubatizo,,, imani, na neno..
Wewe umeenda nje ya topic kabisa. Anayeongelewa ni Martin Luther
 

Pombe imehalalishwa kwenye Biblia lakini kwa kunywa kiasi. Na ndio maana hata nuhu alitoa laana kwa wanae akiwa amekunywa pombe, na laana zikashika. NB: Roman Catholic ni kanisa lilianzishwa na Petro chini ya unabii wa Yesu kuwa juu ya Mwamba huu nitalijenga kanisa, kaburi la Petro liko Vatican
 
Alikufa mkuu ila mwili wake haukuzikwa !! Ila ulipalizwa mbinguni!!

Wewe siku ukifa tutakuzika ndani ya jeneza BT yeye kwa mujibu wa mapokeo, wakati wakiristo na mitume wakiwa wamekusanyika wanasali baada ya kifo cha maria, walishitukia eneo alilokuwepo limeja maua ya waridi (roses) na mwili hauonekani, ndio chimbuko la imani hii ya katholiki.
 

Chimbuko la imani ya Katoliki ni Petro, pale alipoambiwa juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa, fuatilia. Kanisa katoliki lilianzishwa na Yesu
 
philos,
kosa la Martin Luther kwa mujibu wa kanisa sio kulikosoa kanisa bali kulikimbia kanisa, alikuwa na hoja za msingi na ndio maana kanisa lilitafuta ufumbuzi kwa kuitisha mtaguso na kuanzisha shirika la watawa wasomi (Jesuits) kwaajili ya kufanya na kutoa mabadiliko na maoni mtawalia (respectively)
 
Ila jaman hivi inawezekanaje mtu badala ya kuungama kwa mungu akaungame kwa mwanadamu mwenzake?
 
Chimbuko la imani ya Katoliki ni Petro, pale alipoambiwa juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa, fuatilia. Kanisa katoliki lilianzishwa na Yesu
Sikumaanisha ulivyoelewa, imani niliyomaanisha ni kupalizwa.
 
Babu zetu waliletewa hizi dini. Ukichunguza sana dini zakuja haziendani na mila na desturi za waafrika. Lakini kwasababu ya ukoloni, dini zilikubaliwa na madhara yake ndio haya hapa. Kuna kuwa na ubishi wa kutafuta ushahidi kwenye Imani ya binadamu. Ukiona binadamu anatafuta ushahidi kwenye dini ujue huyo sio muumini bali mwanachama tu.
 
Mama Maria... Mama wa Mungu utuombee sisi wakosefu.. sasa na saa ya kufa kwetu.....(Naona mmempitisha)

Sasa sijui Yesu alikuja kufanya nini......
mbona kwenye harusi ya Kana alikuwepo tena mubashara mitume licha ya mazoea walimfuata mama yake !! Baadae maza akasema " chochote atakachowaambieni mfanye"
 
Kwa nini pale msalabani Bwana Yesu alimwambia Petro amuangalie mama yake? Na haikuwa kumwambia Petro mwambie mama akuombee?

Na washawasha!


 
Good man umenena Kweli!
 
kiukweli umekuwa mkristo usie na faida.
kuabudu miungu na kuvunja amri za Mungu ndiko kunakutesa mpaka umkosoe martini luther.
kajipange upya na hoja zako zenye kukinzana na imani ya ukristo.
Kwanini Martin Luther asikosolewe?
 
Kwenye kitabu cha ufunuo unayajua yale makanisa saba? Kama Yesu alianzisha kanisa katoliki, Mbona kanisa katoliki halikutajwa kwenye yale makanisa saba? Jibu Hilo swali kwanza?
 
Kwenye kitabu cha ufunuo unayajua yale makanisa saba? Kama Yesu alianzisha kanisa katoliki, Mbona kanisa katoliki halikutajwa kwenye yale makanisa saba? Jibu Hilo swali kwanza?
Kanisa Lako Lilitajwa?...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…