Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa Kanisa Katoliki?

Inabidi utafute hayo maarifa ili uje utuelezee ukweli kwani kweli humuweka mtu huru. Nakushauri mtafute MUNGU kisha umshirikishe haya mambo nae atakuonyesha kweli kama Yeremia 33:3 inavyosema kuhusu mambo yaliyofichika.
 
Ambacho nimeona mimi ni kuwa wengi wanaobishana kuhusu Biblia kuwa na vitabu pungufu, ni watu ambao sio watu wa kusoma na kutafakari Neno la Mungu na cha zaid ni agenda zao flani flani ambazo either hazipo kwenye Biblia sasa ndo wanazitafutia uhalali kupitia maandiko mengine mengine.
Ninachoweza kukisema mimi ni kwamba Biblia hii tunayosoma pamoja na kutokuwepo kwa baadhi ya vitabu kama mnavyosema ila ina ukamilifu mwingi sana na inatosha sana kumpa mtu uelewa kuhusu huyu Mungu tunaye mwabudu.. Wasomaji wa Biblia wanalijua hili
 
MUNGU kaonya lisipunguzwe neno lolote kwenye maandiko yake kwa hiyo waliotoa hivyo vitabu tayari wamefanya makosa makubwa sana.
Mimi siungi mkono hoja yako kwa sababu ni kinyume na maandiko matakatifu ya MUNGU.
 
Ukisoma theolojia utakuja kufuta hiki ulichoandika.
 
Inabidi utafute hayo maarifa ili uje utuelezee ukweli kwani kweli humuweka mtu huru. Nakushauri mtafute MUNGU kisha umshirikishe haya mambo nae atakuonyesha kweli kama Yeremia 33:3 inavyosema kuhusu mambo yaliyofichika.
Katika mambo haya nishafikiaga maamuzi zamani sana. Sitetereki, sidanganyiki maana namiini niaminicho nimefunuliwa na Mungu aliyeiweka dunia katika uwepo wake.
 
Katika mambo haya nishafikiaga maamuzi zamani sana. Sitetereki, sidanganyiki maana namiini niaminicho nimefunuliwa na Mungu aliyeiweka dunia katika uwepo wake.
Aisee kama wewe ni mwanatheolojia ningetegemea uwe msaada kwetu.
 
Aisee kama wewe ni mwanatheolojia ningetegemea uwe msaada kwetu.
Sijasoma theolojia ile darasani kama taaluma, ila nina watu wa karibu wanaonizunguka ambao wamepita/wanapita hiko. Na kwa **** nami pia nimekuwa mdadisi sana katika haya mambo nilikuwa nahoji baadhi ya vitu vya msingi nilivyokuwa navitilia shaka, hivyo imenisababisha nikajua vitu baadhi ambavyo vinasababisha nisimame mahala nilipo ambapo naamini ni mahala sahihi.

Ila naweza kuwahakikishia watu kuwa, ukisahau kuhusu dini, ukasahau kuhusu vitabu vya dini, ukasahau maoni ya sayansi kumhusu Mungu. Na ukaanza kumfiria Mungu ukiwa umevitoa hivyo nilivyovitaja hapo juu, huenda ukawa umeanza safari itakayokupa mwangaza angalau na utakua huru kiimani. Labda kama lengo lako ni kuchunguza biblia tu
 
MUNGU kaonya lisipunguzwe neno lolote kwenye maandiko yake kwa hiyo waliotoa hivyo vitabu tayari wamefanya makosa makubwa sana.
Mimi siungi mkono hoja yako kwa sababu ni kinyume na maandiko matakatifu ya MUNGU.
Neno kama neno sina hakika limepunguzwaje nikimaanisha content ya vitabu vilivyoko kama iko sawa basi si tabu, ndo maana unaeza kuta wakat mwingine wametenga Agano jipya na Agano la kale , au kuna vitabu vina Zaburi tu, kuna vingine viko ni Mathayo mtakatifu basi, sas binafsi sidhani kama neno litakuwa limepunguzwa hapo kama kilichoandikwa hapo kwenye Zaburi separate kinaendana na kile cha kwenye Zaburi ya kwenye mkusanyiko wote kwa ujumla
 
Hakuna neno lililopunguzwa wakati kitabu kizima au vitabu vimetolewa kabisa?
Alaa wacha utani kabisa na neno la MUNGU
 
Ukisoma theolojia utakuja kufuta hiki ulichoandika.
Ni kweli Mkuu sina uelewa kabisa kuhusu theolojia lakini atleast nmeshawahi kusoma Biblia kwa kiwango flani nikaona ina utoshelevu mwingi sana. Na nafikir tafsiri ambayo unaipata unaposoma neno kwa msaada wa Roho wa Mungu ndo kitu hasa kinacho takikana mbali na uchambuz wa historia kuhusu hilo neno japo inaweza ikakupa uelewa mwingi pia zaidi
 
We si ukajisomee kwani umelazimishwa
 
Una hoja nzuri hapa, nikuelewa mkuu. Hongera.
 
Hakuna neno lililopunguzwa wakati kitabu kizima au vitabu vimetolewa kabisa?
Alaa wacha utani kabisa na neno la MUNGU
Hujanielewa Mkuu, nasema kwamba Sioni kama kupunguza idadi ni shida as long as hawajapunguza kile kilichoandikwa ndani ya hivyo vitabu. Nikasema ndo maana kuna mahali unaeza ukakuta vitabu vya methali na Zaburi vimetengwa peke yake sas Kwa tafsiri yangu siwezi sema wameongeza wala kupunguza neno hapo kama kilichoandikwa hapo kinaendana na kile kilichoandikwa kwenye Biblia yenye vitabu vyote
 
Mimi najua ili neno lake litimie lazima vyote vilivyoandikwa viwepo kisi miss hata kimoja kama unavyosema wewe.
 
Tafuta kitabu kinaitwa "How To Read The Bible: A Guide To Scripture Then and Now".

Cha James L. Kugel.

Kimefundisha mengi sana kuhusu Biblia kutoka huyu mtaalam aliyefundisha somo la kusoma Biblia mpaka Harvard.
 
Wewe mkuu kama huna Imani na uwepo wa MUNGU utaelewaje yaliyosemwa huko?
 
Paulo Alikuwa Mwanafunzi wa Aristole??? LOL...fanya utafiti kabla ya kuandika..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…