Kwanini pale mtu anapofariki huwa wanatoa nguo zake zote na kuzigawa?

Kwanini pale mtu anapofariki huwa wanatoa nguo zake zote na kuzigawa?

MOONFISH

Senior Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
135
Reaction score
268
Habari wakuu natumaini ni wazima wa afya kabisa.

Swali langu kubwa ni kuwa hivi kwanini pale mtu anapo fariki huwa wanatoa nguo zake zote na kuzigawa.

Mfano kama mimi kuna mzazi wangu mmoja ali tangulia ila hata kabla hawaja mzikaa wakakusanya nguo zake zote na kuzikunja na kuzipack yani mapema tu.

Ile kitu iliniumiza sana maana nikiangalia ni mtu wa karibu na ukiingia room kwake hakuna kumbukumbu hata moja yani hata kiatu ni kama room iko empty kama alikuwa haishi hapo.

Ikabidi nipate nafasi ya kusubiria nione maana ndo ilikuwa mara ya kwanza, baadae kwenye eneo la kutawanyika ndo nikaona vitu vina letwa na kugaiwa kwa ndugu mbali mbali dhaaaa aiseee ile kitu iliniuma sana.

Swali langu ni:

1: Kwanini wasiwe wanavihifadhi kwa mda flani kisha ndo wana pata nafasi ya kuwapa wale watu wa karibu au walio kuwa rafiki na marehemu.

2: Kwanini wasiwe wana acha kwa ajili ya kumbukumbu

3: Kwanini wasi chome moto tu. maana una kuta marehemu alikuwa anatupia balaa halafu nguo anaenda kuchukua mtu back.

4: Wazo lako je? Maoni yako tafadhari
 
Hiyo inategemeana na mila na desturi za kabila, na hata ukoo husika. Watu wa jamii yako ndio wana majibu sahihi kabisa ya kwa nini wanafanya hivyo.

Jaribu kuongea na watu wa karibu huko vinginevyo utaje kabila lako au sehemu kuliko fanyika hayo ili upate majibu sahihi kutoka kwa watu sahihi.

Kuna makabila au koo zinazika maiti kwa kuwaelekeza vichwa upande fulani tu-sababu wanaijua wenyewe.

Kuna watu wanachoma maiti-sababu wanaijua wenyewe tu.

Watu wanaokufa kabla ya kuzaa wanawekewa mkaa matakani wakati wa mazishi-sababu inajulikana na wenyewe.

Kuna watu wanazika fasta ukifa hata kama ni jioni-sababu wanaijua wenyewe.

Kuna msela baada ya kufa alivukishwa hadi maji ya bahari wakati kwao ni bara-sababu wanaijua jamii yake.

Kuna watu wanazikwa na pesa na nguo zao-sababu inajulikana na wenyewe tu.

Sasa majibu yatafutwe toka jamii hisika.
 
Ina maanisha Mali na vitu vyote duniani si Mali yetu tutaacha tu. Mali na vitu vinatumiwa duniani ukitambua ivyo basi huko hamna tena ivyo vitu Labda kama Kuna Maisha utaanza upya uko, dunia ni uwanja wa fujo we jibane bane tu kama unao uwezo nunua vitu vizuri hata thamani ambavyo unatumia kila siku kama simu, nguo, perfume nzuri, viatu, saa kali.

Wacha kuishi kama mpare ubahili na vitu utaacha lundo watu watatumia hata pesa kule bank wanachota zote wakifuatilia watajua kila kitu, so tumia vitu vaa vizuri sio unavaa manguo ya ovyo Kama fundi ujenzi yupo site!!! Kumbuka na kujali watu.

Mi hata sijafa ila nguo zangu mdogo wangu anavaa mno.
 
Ina maanisha Mali na vitu vyote duniani si Mali yetu tutaacha tu. Mali na vitu vinatumiwa duniani ukitambua ivyo basi huko hamna Tena ivyo vitu Labda kama Kuna Maisha utaanza upya uko, dunia ni uwanja wa fujo we jibane bane tu kama unao uwezo nunua vitu vizuri hata thamani ambavyo unatumia kila siku kama simu, nguo, perfume nzuri, viatu ,saa kali
Wacha kuishi kama mpare ubahili na vitu utaacha lundo watu watatumia hata pesa kule bank wanachota zote wakifuatilia watajua kila kitu, so tumia vitu vaa vizuri sio unavaa manguo ya ovyo Kama fundi ujenzi yupo site!!! Kumbuka na kujali watu.

Mi hata sijafa ila nguo zangu mdogo wangu anavaa mno.
Kwahiyo mdogo wako yeye hana pesa ya kununua nguo?
 
Mama yangu alipofariki niligawa nguo kwa maamuzi yangu baadhi nimebaki nazo Hadi Leo. Hizo ni taratibu zilizoanzishwa na watu kama wewe waliokuwa na mawazo yao lakini sio sheria fanya unachoona kinafaa kwa wakati huo.
 
Mambo hayo ni tamaduni na mila tu za sehemu fulani lakin kwa upande mwingine mamb hayo yamepitwa na wakati na mtu yoyote yule pia anaweza pewa kama kumbukumbu kutumia vitu vilivyoachwa na marehemu.
 
Mama yangu alipofariki niligawa nguo kwa maamuzi yangu baadhi nimebaki nazo Hadi Leo. Hizo ni taratibu zilizoanzishwa na watu kama wewe waliokuwa na mawazo yao lakini sio sheria fanya unachoona kinafaa kwa wakati huo.
sasa kwangu mimi ndo nataka iwe hivi yani mimi ndo nakuwa na mgawia mtu ila sio zina chukuliwa na kwenda kugawiwa uko kijijini hapana.
 
Huyu mleta mada inaonekana ni mchoyo na mtu mwenye roho nyembamba sana
 
sasa kwangu mimi ndo nataka iwe hivi yani mimi ndo nakuwa na mgawia mtu ila sio zina chukuliwa na kwenda kugawiwa uko kijijini hapana.
Aisee hivi umefikiria vizuri? Kama umezaliwa peke yako katika familia unadhani ni wote? Mgao hufanyika kwa makubaliano ya watoto wa marehemu wenye haki ya kwanza ya kurithi. Kama umezaliwa peke yako waweza kufanya unavyopenda.
 
Back
Top Bottom