Kwanini Polisi walishindwa kuifichia aibu familia ya Mzee David Makerege? Yesu aliwaambia "asiye na dhambi miongoni mwenu awe wa kwanza kumtupia jiwe"

Polisi wamekosea sana kuweka hadharani faragha ya marehemu alafu kuna watu humu wanakaa kuwatetea tetea.

Siku kila muda ni kuwaunga mkono viongozi, kuna wakati tunapaswa kuwapa challenge kidogo.
 
Polisi wamekosea sana kuweka hadharani faragha ya marehemu alafu kuna watu humu wanakaa kuwatetea tetea.

Siku kila muda ni kuwaunga mkono viongozi, kuna wakati tunapaswa kuwapa challenge kidogo.
Hao wanaotetea polisi hawelewi kanuni za msingi za kikatiba za presumption of innocence and right to privacy.

Ni kukosa elimu tu.
 
Unasema kama angekuwa mtu wangu wa karibu! Na huyo binti angekuwa wako ingekuwaje! Mungu amuweke mahali pema ila wazee waache hii tabia. Ni mengi yanayoendelea yasiyojulikana kwa mabinti wetu.
 
Unasema kama angekuwa mtu wangu wa karibu! Na huyo binti angekuwa wako ingekuwaje! Mungu amuweke mahali pema ila wazee waache hii tabia. Ni mengi yanayoendelea yasiyojulikana kwa mabinti wetu.
Hakuna aliye mkamilifu chini ya jua. Kila mmoja wetu ni mdhambi kwa namna tofauti tofauti.
 
Kwa sababu zinaa ni dhambi. Maandiko yamesema wazi kabiza
MITHALI 6:32
Naye azinie na mwanamke hana akili kabisa. Afanya jambo litakalo iangamiza nafsi yake, ATAPATA JERAHA NA KUVUNJIWA HESHIMA WALA FEDHEA YAKE HAITAFUTIKA
 
Unasema kama angekuwa mtu wangu wa karibu! Na huyo binti angekuwa wako ingekuwaje! Mungu amuweke mahali pema ila wazee waache hii tabia. Ni mengi yanayoendelea yasiyojulikana kwa mabinti wetu.
Kuna hoja mbili zinazochanganywq hapa.

1. Huyo Mzee kufanya vibaya.

2. Polisi kukosa faragha

Huyo Mzee kufanya vibaya ni suala la mahakama kujadili. Kama huyo binti alikuwa over 18 years na hakulazimishwa hapo ni suala la watu wazima wawili walivyoelewama.

Kwa hiyo sielewi watu wanashikia bango nini hapo.

2. Polisi wana wajibu wa kutunza habari za raia, hususan ikiwa raia hawajaonekana kuwa na hatia katika mahakama. Kwenye hili, Polisi kutoa habari za huyu mzee wamekosea.
 
Umefafanua vizuri sana mkuu
 
Kwa sababu zinaa ni dhambi. Maandiko yamesema wazi kabiza
MITHALI 6:32
Naye azinie na mwanamke hana akili kabisa. Afanya jambo litakalo iangamiza nafsi yake, ATAPATA JERAHA NA KUVUNJIWA HESHIMA WALA FEDHEA YAKE HAITAFUTIKA
Kwani yeye pekee ndiye mdhambi? Hao Polisi hawatendi dhambi kama wanadamu? Wao ni malaika?
 
Sasa afe kwa upumbavu wake halafu polisi wafiche ili iweje?!

Yaani askari wasemeje sasa kuwa alianguka barabarani au alienda guest kulala tu akapata shida ya moyo?!
 
Hujui lolote kaa kimya! Huoni kuwa Ni tukio lilifanyika nje ya familia yake? Na linahitaji uchunguzi wa kisheria?

Angefia kwake hapo polisi wasingehangaika, ila kafia guest house unataka polisi wasifuatilie?
Kufuatilia ni lazima, kujitangaza hadharani sio lazima.
 
Kama yeye mwenyewe alishindwa kuficha aibu yake ya kumkalia uchi mjukuu, polisi Ni Nani mpaka waifiche??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…