Kwanini Polisi walishindwa kuifichia aibu familia ya Mzee David Makerege? Yesu aliwaambia "asiye na dhambi miongoni mwenu awe wa kwanza kumtupia jiwe"

We mwenyewe umeshindwa kuificha picha yake .... kupitia uzi wako bado unazidi kumchoresha Mzee wa watu
Kupitia uzi huu ninawakumbusha Polisi kutumia hekima katika kushughulikia masuala yahusuyo wazee
 
Yaani askari wasemeje sasa kuwa alianguka barabarani au alienda guest kulala tu akapata shida ya moyo?!
Askari waseme yote wanayoyasema lakini kwanini wataje majina yao? Mbona ndugu yangu alikufa lakini Polisi hawakutangaza?
 
Hasa hasa kama alikuwa anamke. Maana huyo mke anaanzaje kuomboleza? Shida tupu.
Ni aibu sana kwa mke lakini zaidi kwa watoto na wajukuu kwa maana wao bado wana umri mrefu zaidi wa kuwepo hapa duniani na kuendelea kunyooshewa vidole na walimwengu.
 
Polisi wamemshikilia kwa mahojiano zaidi. Hiyo ni kawaida kwa matukio ya namna hii
Matukio ya namna hii yapi ?

Kisheria unashikiliwa masaa 24 kama ni mshukiwa wa jinai. Sio kiholela holela tu kwa mahojiano zaidi.

Mahojiano zaidi kwani ametoa mwimbo mpya ?

Jamii imesema mwanamke ndio muathirika. Muathirka mbona kakamatwa?
 
Matukio ya namna hii yapi ?

Kisheria unashikiliwa masaa 24 kama ni mshukiwa wa jinai. Sio kiholela holela tu kwa mahojiano zaidi.

Mahojiano zaidi kwani ametoa mwimbo mpya ?

Jamii imesema mwanamke ndio muathirika. Muathirka mbona kakamatwa?
Sawa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…