Kwanini Polisi walishindwa kuifichia aibu familia ya Mzee David Makerege? Yesu aliwaambia "asiye na dhambi miongoni mwenu awe wa kwanza kumtupia jiwe"

Yaani polisi wasitoe taarifa rasmi kwa lengo la kulinda heshima/kumfichia aibu marehemu?

Unajua kuwa Mambo ya kisheria huwa hayana kupindisha?
Police hawakutoa taarifa ila iliyoleak ni ile Document halali ya Police, ambapo ni kosa kubwa maana taarifa inayosambaa ni ile ripoti iliyoandikwa na Askari wetu aloyeshuhudia tukio!taarifa tuliyotakiwa kuipata ni km ile iliyotolewa na Miladayo, kwakweli na mm nimeshindwa kuelewa vp km Ethics za Uaskari zimezingatiwa hapo!
 
Siku mzee Makerege alipokufa yalitokea matukio mngapi ya uhalifu hapa nchini? Kwanini coverage kubwa alipewa yeye tu na sio matukio mengine ambayo hayakutangazwa?...
Sio polisi walimpa coverage kubwa kasababu hawana TV Radio, au gazeti.Ni umma ndio ulimpa coverage kupitia mitandao ya kijamii.

Kwani mkuu polisi ndio waliotoa picha zake na za mwanamke?polisi wameripoti Kama tukio lingine umma Ndio ukalidaka na kuongezea Nyama
 
Hao askari Police pia ni wanadamu. Kwani wao hawatendi dhambi/makosa kama mzee Makerege? Wazee ni lazima wawe treated kwa busara na hekima.
Hakuna mahali amevunjiwa heshima,kilichoripotiwa ni kifo chake na mazingira ya kutokea kwake kwisha.Au ulisikia Polisi anasema marehemu alikosea kulala na mjukuu wake?
 
Makosa yana uzito wake ndio maana kila kosa lina adhabu yake. Mtu aliyeua kwa makusudi hawezi kuhukumiwa sawa na aliyetukana mtandaoni
Na kazi ya polisi sio kuhukumu,na Hakuna mahali taarifa imemhukumu au kumlaumu marehemu.
Kilichoelezwa ni tukio kama yanavyoripotiwa mengine hata wewe ukijinyonga Leo kesho polisi atatoa taarifa umejinyonga na mazingira ya kujinyonga Ms sababu Kama uliiweka wazi.
 
Dhambi haifichiki
 
Ujambazi na wizi utalinganisha vp na suala la huyu mstaafu wa miaka 80 kufia hotelini mkuu? Are you serious?
Unachanganya mambo,wewe nikikuajiri Leo ktk ofisi yangu kisha Nikakupa muongozo kwamba uwe unanipa taarifa ya Matukio yaliyotokea kila siku,utanipa taarifa za wizi uliotokea ofisini mpaka taarifa za balbu zilizoungua.

PGO inamuelekeza kutoa taarifa kwa umma ya Matukio yaliyotokea full stop.Iwe umejinyonga,umeuawa,ajali,wizi,umekufa mazingira tatanishi,wizi no zote ni taarifa za kutoa
 
Leo umeongea point tupu.
 
Unachanganya mambo,wewe nikikuajiri Leo ktk ofisi yangu kisha Nikakupa muongozo kwamba uwe unanipa taarifa ya Matukio yaliyotokea kila siku,utanipa taarifa za wizi uliotokea ofisini mpaka taarifa za balbu zilizoungua.

"dereva ana makosa, kwanza alishindwa kuheshimu taa zinazoongoza magari na hairuhusiwi kupita katika njia hizo za mwendokasi. Baada ya kusababisha ajali hiyo, alilitelekeza gari na kukimbia", alisema Mambosasa.

"Namba za gari la jeshi (JWTZ) kwa sasa sizikumbuki kwa kuwa nimetoka ofisini nashughulika na masuala ya mafuriko".

Number ya hii gari ilitajwa?...
 
PGO inamuelekeza kutoa taarifa kwa umma ya Matukio yaliyotokea full stop.Iwe umejinyonga,umeuawa,ajali,wizi,umekufa mazingira tatanishi,wizi no zote ni taarifa za kutoa
Achana na story za PGO mkuu, mbona huwa inapindishwa sana hiyo PGO yenu.

Kazi ya kuwa Polisi inahitaji busara pia na sio nguvu kila wakati
 
Samahani kidogo, hiv huyu mzee alikuwa ni kigogo fulani mkubwa wa serikali/mtu fulan maarufu mpaka habari yake imetrend hivi au ni mtu qa kawaida upepo mbaya tu umemwelekea habari yake ikavuma hiv?
 
Usilale Mbezi Garden chumba namba 22
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…