Kwanini polisi wameweka pembeni PGO na kuamua kukamata raia kwa kutumia nguvu kubwa? Je, nao hawaamini mfumo wa Sheria?

Kwanini polisi wameweka pembeni PGO na kuamua kukamata raia kwa kutumia nguvu kubwa? Je, nao hawaamini mfumo wa Sheria?

kagoshima

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2015
Posts
2,887
Reaction score
5,687
Kuna mtindo mpya wa polisi napengine idara zingine za usalama kuvizia, kukimbiza raia wenye tuhuma za makosa. hata high profile citiezen ambao wangeweza kupigiwa simu na wange report kituoni bila shida nao wameonekana kukimbizwa kama vibaka.

Na wakati mwinge wakiwa kwenye kundi kubwa na silaha nzito kukamata raia wa kawaida mikono mitupu. Si tunaambiwa mnaongozwa na Sheria, taratibu na PGO nyie?

1. Je, nikwamba polisi hawaamini tena utaratibu wa Sheria?

2. Je, hawana Imani hata na mahakama zetu?

3. Hawaoni taharuki inayotengenezwa?

4. Je, wataendelea kufanya hivo nje ya utaratibu hadi lini?

Polisi tambueni kwamba, usalama wa nchi hujengwa kwa ushirikiano uliotukuka kati vyombo vya Dola na raia. Sote tufate Sheria zilizopo na kama zinashida tukubaliane kuzibadilisha, kuliko kuzikanyaga na kutenda nje ya Sheria kama wafanyavyo polisi kwa sasa.
 
Back
Top Bottom