Kwanini Polisi wanawapiga mabomu wananchi, katika msimu huu wa hekaheka za uchaguzi?

Kwanini Polisi wanawapiga mabomu wananchi, katika msimu huu wa hekaheka za uchaguzi?

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,175
Reaction score
4,181
Kwa kweli msimu huu wa uchaguzi ni kama sherehe katika nchi ,kwa wananchi wengi kujichagulia kiongozi wao kutoka chama kitakachobahatika kupaa kura nyingi kihalali au kimipango.

Sasa inakuwaje polisi wanaonekana kubeba upande mmoja kwa visingizio vya kijinga sana,hata Afande wao mkubwa nafikiri wanampa tabu sana kukutana na waandishi wa habari,maana unapiga watu mabomu ili iweje?

Leo mabomu first warning baadae top risasi kupigwa juu baadae risasi kwa wananchi kuingia mwilini,Bara sio Zanzibar ,polisi mchezo mnaozoea kuwafanyia WaZanzibari bora muufanye hukohuko Tanganyika au Tanzania bara ni kubwa sana sana ,wananchi wakishindwa kuwavumilia mjue mtapata tabu.

Sisemi mtashindwa hapana mtapata tabu,hio Dar pekee ikichafuka kiwendawazimu within a short time mtajutia kurusha mabomu kuisaidia CCM,ni hatari wananchi wataogopa lakini mwisho wake watakuwa kama nyinyi wapo tayari kufa,kulinda heshima yao.

Msichokonoe chokonowe wala msijidanganye na kuwatisha wananchi waliochoka na maisha,wapemba juzi mmewasikia,wapo tayari kufa wala kupigwa waliko pigwa basi ikitokea mara hii itakuwa ama zao .

Mabomu hayo mnayotekenya watu siku wakija kutekenyeka mtashindwa pa kuziba maana ukiziba Kibaha utasikia Mbagala kunavuja ,ukikimbilia kuziba Mbagala utasikia feri yaripuka ,nchi mshaichafua kwa mabomu yenu kuilinda CCM na kuwalinda washusha bendera za Chadema.

Msiwe watumwa waCCM mpaka mnavuka mipaka,vigogo wengi wa CCM kwa walipofikia wanauwezo wa kuishi nchi za nje, Je nyie mapolisi si tutabakia hapahapa na kubanana,kisa mlianza kurusha bomu kuwatisha wananchi katika msimu wenye mhemko ya kila aina.

Polisi mnatisha sana,nchi hii ndugu zanguni ikichemka ni hatari,msifananishe na kuzuia maandamano ,msifananishe na kumzuia mgombea kuruka njia,hali inakuwa nyengine kabisa, wakati huo mnaowalinda na kuwakingia ubavu hamuwasikii.

Mambo yakichemka ni hatari,watafariki watakaofariki na watapona watakao pona ,ila msidhani katika kundi hilo hamtakuwemo .

Naona mnafananisha kuvurugika nchi na maandamano,

Nchi ikivurugika inashinda vita,maana vita adui yako yuko Uganda na Sisi tupo Tanzania aidha tulivuka mpaka na kumfukuza adui lakini vurugu ya nchi ni kila hatua ya nchi yupo mwananchi utwazuia vipi,ukiangalia waote njaa tupu,itakuwa hakuna cha ccm wala chadema wote wanakuwa wamoja na kila mmoja anakata kipande cha keki.

Polisi kuweni waangalifu sana ,msiingie katika kuingizwa katika sababu za kijinga,unamzuia mtu asiruke njia.Hivi ukimuacha akaruka ndio atamshinda Magufuli na CCM yake?
 
Polisi msidhane wala msifananishe maandamano na machafuko ya nchi,mnajisifu mmejipanga lakini mbali ya kujipanga kwenu hivyo ni vitu viwili tofauti na havilingani hata kwa ladha yake.
 
Hawana uwezo wa kupiga mabomu nchi nzima, kwanza Wana mpasuko wao kwa wao Wana itikadi mbalimbali pia hasira za kutoongezwa mishahara kwa miaka 5
 
Back
Top Bottom