Kwanini Polisi wetu washangilie ujio wa wachunguzi wa Kichina hata kabla ya matokeo?

Kwanini Polisi wetu washangilie ujio wa wachunguzi wa Kichina hata kabla ya matokeo?

Miwatamu

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2012
Posts
1,450
Reaction score
489
Leo asubuhi karibia vyombo vyote vya habari vimeandika juu ya ujio wa wachunguzi wa mambo ya milipuko na mabomu huko Arusha, wakitokea China. Kwangu binafsi nililipokea kwa furaha, lakini furaha yangu ilianza kuingiwa kiwewe pale Jeshi letu lilipoonesha kuwa tayari wanajua nini matokeo yatakayotolewa na makomandoo hao.

Je, tutaaminije taarifa zao kama hazitakuwa zimetengenezwa na serikali na wao wakaletwa kama mawakala wao na vipaza sauti tu wa kutoa taarifa iliyoandaliwa?

TAFAKARI
 
Wachina nao watu basi.....hamna watu nisio waamini kama wachina....mtaona tu....lakin CCM pia si walikuwa wamepiga kambi huko kitambo kidogo...?
 
Kabla haijatokea tayari mipango ilishapangwa huko China chini ya Kinana na Mwigulu,kwa hiyo yanayoendelea
ni utekelezaji wa kile walichokipanga huko na hao wachina,hakuna la maana la kusubiri hapo
 
Chinese are proven to be spineless and worst virus around.
 
Leo asubuhi karibia vyombo vyote vya habari vimeandika juu ya ujio wa wachunguzi wa mambo ya milipuko na mabomu huko Arusha, wakitokea China. Kwangu binafsi nililipokea kwa furaha, lakini furaha yangu ilianza kuingiwa kiwewe pale Jeshi letu lilipoonesha kuwa tayari wanajua nini matokeo yatakayotolewa na makomandoo hao.

Je, tutaaminije taarifa zao kama hazitakuwa zimetengenezwa na serikali na wao wakaletwa kama mawakala wao na vipaza sauti tu wa kutoa taarifa iliyoandaliwa?

TAFAKARI

na sisi tutaaminije mawazo yako kama yako sahihi au siyo ya kichochezi na kwa nini ukimbilie kutilia shaka kama wewe siyo mhusika,
 
acheni dora ifanye kazi kuingilia kazi ambazo hazituhusu siyo busara.
 
Kabla haijatokea tayari mipango ilishapangwa huko China chini ya Kinana na Mwigulu,kwa hiyo yanayoendelea
ni utekelezaji wa kile walichokipanga huko na hao wachina,hakuna la maana la kusubiri hapo

mkuu mwigulu anakufanya usilale naona huishi kumtaja hata kidogo,kwa siku unamtaja zaidi hata ya mara kumi.
 
ilikuwa FBI sasa n wachina, duh!, hii issue itapotelea kichakani kama nyingine nyingi2.
 
Halafu magazeti yetu bila research ya kutosha wanasema ni FBI ndo wamekuja hiyo yote ni kutengeneza ushahidi
 
Leo asubuhi karibia vyombo vyote vya habari vimeandika juu ya ujio wa wachunguzi wa mambo ya milipuko na mabomu huko Arusha, wakitokea China. Kwangu binafsi nililipokea kwa furaha, lakini furaha yangu ilianza kuingiwa kiwewe pale Jeshi letu lilipoonesha kuwa tayari wanajua nini matokeo yatakayotolewa na makomandoo hao.

Je, tutaaminije taarifa zao kama hazitakuwa zimetengenezwa na serikali na wao wakaletwa kama mawakala wao na vipaza sauti tu wa kutoa taarifa iliyoandaliwa?

TAFAKARI

Kiwewe cha nini? Tusubiri matokeo
 
Nimeshangazwa sana na taarifa zilizozagaa kuanzia jana kuwa kuna wachunguzi kutoka nje wamekuja kuchunguza chanzo cha mlipuko wa bomu arusha.Mwanzoni kabisa walisema ni FBI wamekuja.Ghafla leo tunaambiwa ni wachina wamekuja kuchunguza chanzo cha milipuko au kutafuta wahusika wa milipuko hiyo.
Lakini suala la kujiuliza ni kwamba hao wataalamu kutoka china wanatafuta waliolipua bomu au aina ya bomu lililolipuka?
Pili ni kwamba kuleta wataalamu kutoka chini kwa nionavyo ni expensive kuliko kuunda tume huru ya kijaji kuchunguza tukio hilo.Kwa nini serikali haitaki kuunda tume huru na wanatumia polisi ambao ni watuhumiwa katika kuchunguza.
Nahisi wachina wameletwa kwa ajili ya kuua usshahidi au kutengeneza mazingira ya kuwahusisha watu fulani na milipuko hiyo.
Kuna kigugumizi gani kuunda tume katika tukio la arusha?
Ikumbukwe pia mwigulu na kinana wamezuru china hivi karibuni,kuna uwezekano mkubwa wanaoitwa wataalamu wa kichina ni mamluki walioandaliwa rasmi kuvuruga ushahidi arusha.
Hebu tujiulize kwa nini polisi wanashangilia sana ujio huu na kwa nini mkuu wa mkoa wa arusha amegeuka kuwa msemaji mkuu wa maendeleo ya uchunguzi arusha badaka ya polisi wenyewe.Tusubiri
 
Hakuna wachunguzi hapo.this is just another game as usual!
 
ALHAMISI, JULAI 04, 2013 05:13 NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

*Wataalamu kutoka China watua kuchunguza
*Polisi watamba kufichua siri ya milipuko yote

TAARIFA za awali kutoka kwa makachero wa Jeshi la Polisi nchini zimefanikiwa kubaini mtandao wa ulipuaji mabomu katika jiji la Arusha, imefahamika. Mpaka sasa taarifa zinadai mtandao uliohusika na milipuko miwili iliyotokea kwa nyakati tofauti jijini hapa ulipangwa ndani ya jiji la Arusha.

Mlipuko wa kwanza ulitokea katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti, Mei 5, mwaka huu na kuua watu watatu, wakati mlipuko wa pili ulitokea Uwanja wa Soweto Juni 15, mwaka huu na kuua watu wanne, huku majeruhi wa matukio yote wakifikia zaidi ya 100.

Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) jana jijini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alisema mbinu hizo zimejulikana kutokana na wananchi waliojitokeza kuwasilisha ushahidi kwa vyombo vya dola.
Alisema mpaka sasa ushahidi unaonyesha kuwa mtandao wa waliolipua wa mabomu hayo ulianzia jijini Arusha, na kikubwa kabisa wanawashukuru wakazi wa Arusha waliokuwa wakifika kutoa ushahidi wa wahusika.

"Ukweli wa mambo haya utajulikana hivi karibuni na Serikali itamchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kuhusika na mtandao huo, bila kujali wadhifa wake. Mambo haya yamedhalilisha na kufedhehesha Taifa," alisema Mulongo.

Akiwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, aliendelea kubainisha kuwa upelelezi wa matuko hayo mawili unaendelea kwa umakini mkubwa na kikubwa kinachoangaliwa ni kuepuka kukamata watu wasiohusika.

"Tunachukua umakini ili waliofanya hivi vitendo vya kinyama wasiendelee kutamba, kwani wanajua tukikamata wasiohusika wao watajiona wameshinda hawajakamatwa," alisema Mulongo.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa aliwataka pia wanasiasa nchini kutoigeuza milipuko ya mabomu hayo kama njia ya kujitafutia umaarufu wa kisiasa.

"Kugeuza tukio hili la kinyama kuwa agenda ya kisiasa kunaidhalilisha Tanzania nje ya nchi na kuleta athari za kupoteza wageni," alisema Mulongo.

Mulongo alisema taarifa za awali za kikachero zinaonyesha kuwa bomu lililorushwa katika viwanja vya Soweto lilitengenezwa China.

Mkuu huyo wa mkoa alisema, tayari wataalamu kutoka China wamekwisha wasili jijini Arusha kwa ajili ya kufanya utambuzi wa taasisi iliyonunua bomu hilo.

Mulongo katika hotuba yake aliendelea kuwataka wanasiasa kuacha dharau na kueneza maneno yasiyo na ukweli juu ya Serikali, badala yake aliwataka kuheshimu taratibu za nchi ili vyombo vya dola visilazimike kutumia nguvu kukabiliana na watu au kikundi kitakachovunja sheria zilizowekwa.

"Hivi ndugu zangu, lazima tufike mahali tujiulize hawa wanasiasa wanaotumia uongo na nguvu nyingi kuchafua nchi huko duniani, wanafanya hivi kwa faida ya nani?" alihoji Mulongo.

Bomu hilo lilirushwa katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA), wakati kikihitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata nne jijini Arusha Juni 15, mwaka huu.

Hata hivyo, siku mbili baada ya mlipuko huo, chama hicho kilitoa shutuma nzito dhidi ya Jeshi la Polisi na kueleza kuwa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), ndiye aliyerusha bomu hilo.

Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa chama chake kinao ushahidi wa picha na sauti unaothibitisha kwamba polisi ndio wahusika wa mlipuko huo.

Hata hivyo, chama hicho kimegoma kukabidhi ushahidi huo kwa jeshi hilo kwa maelezo kuwa ushahidi huo hauwezi kutolewa kwa polisi, ambao ni watuhumiwa wa tukio hilo.

Chama hicho kilitoa sharti kwa Rais Jakaya Kikwete kuunda Tume ya Mahakama itakayohusisha majaji waadilifu na kusema kuwa kipo tayari kutoa ushahidi huo mbele ya tume hiyo na si polisi.

Mbali na bomu hilo, bomu jingine lilirushwa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti na kusababisha watu watatu kufariki ambapo nalo liligundulika kutengenezwa nchini Urusi.

Wachina nao watu basi.....hamna watu nisio waamini kama wachina....mtaona tu....lakin CCM pia si walikuwa wamepiga kambi huko kitambo kidogo...?
Watanzania, kama hatuachi hizi tabia za kitu kutoka nje, basi kitakuwa na solution. Hivi mchina atachunguza nini? Tushajua bomu lilinunuliwa kwao na ni la kijeshi. Tushajua polisi walipiga watu risasi kusudi mrushaji akimbie. Sasa mchina atwambie nini? Mnataka aseme aliyerusha ni jirani ya nani au alikuwa amevaa viatu fulani?
Tujiulize tuliokwishajua tumeyafanyia nini? Bahati mbaya CCM huwa ina tabia moja. Kama kitu wamekifanya wao, hata kama ni kibaya..huwa hawawajibishi mtu. Ila wanaomba sana na hata kulazimisha kitendo kiovu kifanywe na mtu wa Chadema. Mchina hawezi kutupa taarifa zaidi ya tunayoyajua. Nina wasi wasi wanataka kupindisha hili tukio kwa kutumia wachina. Nikumbushe tu kwamba China ni taifa mojawapo kati ya mataifa yasiojali haki za binadamu. Sishangai kutumiwa na CCM.
 
Hivi huu ushirikiano na China katika upelelezi ulianza lini? Maana kugundua kuwa bomu limetengenezwa China hilo tayari na upelelezi wa ulipuaji haumuhusu mtengenezaji kupeleleza muhusika.
Kwani tungegundua bomu limetengenezwa Congo tungeita wapelelezi toka Congo kupeleleza waliolipua? Sisi tunataka kumjua mlipuaji na hiyo ni kazi ya Polisi au kama hawaaminiki kama Chadema walivyosema basi ni muhimu hiyo tume ya Kijaji iundwe ili kupokea huo ushahidi. Pia kama ni msaada wa nje tuletewe vyombo vinavyo aminika Duniani kama FBI au Scotland Yard na sio hao Wachina ambao hawapo kwenye list ya wachunguzi bora na wanafahamika wanatenda kazi zao kwa matakwa ya Serikali yao kibiashara. Kumbuka hawawezi kuiumbua serikali ya nchi hii na kuharibu dili zao za gasi nk
 
Back
Top Bottom