Kwanini PSSR siku hizi wanaita watu kazini kwa awamu badala ya mkupuo kama ilivyozoeleka?

Doz m

Member
Joined
Nov 17, 2022
Posts
6
Reaction score
1
Kwanini PSSR siku hizi wanaita watu kazini kwa awamu, badala ya kuita wote kwa mkupuo kama ilivyozoeleka?

Yaani mfano, tumeomba kazi mwezi wa 5 mwaka jana, tukaitwa interview mwezi wa kwanza na wa pili, placement ndio inafanyika sasa lakini kwa awamu.

Watu tumefanya usaili siku moja, halafu wengine sasa wako kazini, sisi tunarushwa matumbo joto tu. Sioni mantiki ya kutoa kwa awamu, mianya ya rushwa hapa inapigwa kama kawaida, tuendelee kuteseka. Yaani mchakato unatumia zaidi ya mwaka mmoja, wenzetu TAMISEMI wanatumia miezi mitano.

Hawa PSSR kuna haja ya kuchunguzwa na Wajibu, kwani uratibu wao umekuwa wa tofauti na ilivyozoeleka, kwanini wanatumia muda mrefu namna hii?!
 
Tatizo nadhani siyo PSRS bali ni Serikali yenyewe!! PSRS kumbuka ni wakala tu anayefanya kwa niaba ya waajiri katika utumishi wa umma. Mwajiri huomba kibali cha kuajiri serikalini, serikali kupitia wizara ya utumishi hutoa vibali vya kuajiri kwa maana ya kwamba fedha ya mishahara na mchakato wote inaingizwa kwenye bajeti ya mwaka husika. PSRS wanaanzisha mchakato wa kutafuta waajiriwa kwa kutangaza nafasi za kazi na kufanyisha usaili. Tatizo linakuja mahali ambapo Halmashauri husika haijapewa hilo fungu la kuiwezesha kuajiri watumishi wapya!!. Halmashauri zote hazipewi fedha hizo kwa pamoja!! Sababu ni kwamba Serikali haijafanikiwa kupata pesa yote iliyotarajiwa kupatikana kutokana na kodi!! Kwa hiyo inalazimika kutoa pesa kidogo kidogo kwa kadri inavyopata makusanyo ya kodi na haina ujanja mwingine zaidi ya makusanyo ya kodi.
Kwa mfano MDA&LGA walitangaza ajira mwezi wa 5 mwaka 2022. Hiyo pesa ilikuwa imepangwa kwenye bajeti yake ya 2022/2023. PSRS waliitisha usaili wake mwezi wa pili mwaka huu 2023!! Ikaanza kuita watu kazini kidogo kidogo kwa kadri halmashauri zinavyokuwa tayari kuwapokea kwa kuwezeshwa kuwalipa mishahara na stahiki zingine!! Usilaumu wakala (PSRS) afanyaye kwa niaba ya waajiri. Lakini pia usiwalaumu waajiri maana hawajawezeshwa bado kuwapokea waajiriwa wapya wote kwa mkupuo!! Lakini pia usiilaumu Serikali maana haina namna nyingine ya kupata pesa zaidi ya kodi na mikopo/misaada. Kama serikali haijapokea kodi kama ilivyotarajia, haina ujanja mwingine zaidi ya kusubiri. Mchawi mkubwa ni mlipa kodi na mkusanya kodi (TRA). Bado watanzania walio wengi hawapendi kulipa kodi kwa wakati na kwa ukamilifu. Sasa wakija TRA nao kwa baadhi ya watumishi wao kukosa uaminifu hupokea kitu kidogo (rushwa) kwa wafanyabiashara ili wawasaidie kukwepa kulipa kodi kwa wakati na kwa ukamilifu!!. SULUHISHO LA KUDUMU: Watanzania tuone fahari kulipa kodi kwa ukamilifu na kwa wakati. Kinyume cha hapo, tutasubiri sana!!​
 
Watanzania tubadilike tuone kuwa inalipa sana tukikubali kuwa tunaambiana ukweli!! Tupende kulipa kodi, tufurahie kulipa kodi, ili kuiwezesha serikali kuandaa mazingira mazuri kwa wananchi wake kuendelea kiuchumi na kijamii!!
 
Tatizo nadhani siyo PSRS bali ni Serikali yenyewe!! PSRS kumbuka ni wakala tu anayefanya kwa niaba ya waajiri katika utumishi wa umma. Mwajiri huomba kibali cha kuajiri serikalini, serikali kupitia wizara ya utumishi hutoa vibali vya kuajiri kwa maana ya kwamba fedha ya mishahara na mchakato wote inaingizwa kwenye bajeti ya mwaka husika. PSRS wanaanzisha mchakato wa kutafuta waajiriwa kwa kutangaza nafasi za kazi na kufanyisha usaili. Tatizo linakuja mahali ambapo Halmashauri husika haijapewa hilo fungu la kuiwezesha kuajiri watumishi wapya!!. Halmashauri zote hazipewi fedha hizo kwa pamoja!! Sababu ni kwamba Serikali haijafanikiwa kupata pesa yote iliyotarajiwa kupatikana kutokana na kodi!! Kwa hiyo inalazimika kutoa pesa kidogo kidogo kwa kadri inavyopata makusanyo ya kodi na haina ujanja mwingine zaidi ya makusanyo ya kodi.
Kwa mfano MDA&LGA walitangaza ajira mwezi wa 5 mwaka 2022. Hiyo pesa ilikuwa imepangwa kwenye bajeti yake ya 2022/2023. PSRS waliitisha usaili wake mwezi wa pili mwaka huu 2023!! Ikaanza kuita watu kazini kidogo kidogo kwa kadri halmashauri zinavyokuwa tayari kuwapokea kwa kuwezeshwa kuwalipa mishahara na stahiki zingine!! Usilaumu wakala (PSRS) afanyaye kwa niaba ya waajiri. Lakini pia usiwalaumu waajiri maana hawajawezeshwa bado kuwapokea waajiriwa wapya wote kwa mkupuo!! Lakini pia usiilaumu Serikali maana haina namna nyingine ya kupata pesa zaidi ya kodi na mikopo/misaada. Kama serikali haijapokea kodi kama ilivyotarajia, haina ujanja mwingine zaidi ya kusubiri. Mchawi mkubwa ni mlipa kodi na mkusanya kodi (TRA). Bado watanzania walio wengi hawapendi kulipa kodi kwa wakati na kwa ukamilifu. Sasa wakija TRA nao kwa baadhi ya watumishi wao kukosa uaminifu hupokea kitu kidogo (rushwa) kwa wafanyabiashara ili wawasaidie kukwepa kulipa kodi kwa wakati na kwa ukamilifu!!. SULUHISHO LA KUDUMU: Watanzania tuone fahari kulipa kodi kwa ukamilifu na kwa wakati. Kinyume cha hapo, tutasubiri sana!!​
This is powerful comment.!
 
Back
Top Bottom