Mangungo II
JF-Expert Member
- Jul 6, 2012
- 18,133
- 26,766
Tambaza CLass of 2009-2011
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Damme yupo jela..!1994 kuna mwingine alikuwa anajiita van damme nae alikuwa mkorofi sana.
Kuna shule ubungo national housing ilikuwa ni evening class kwa secondary jamaa alileta vurugu siku tatu wanafunzi hawaendi shule.Damme yupo jela..!
Alikua anasimamisha mechi ya sinza star na abajalo...yeye mwenyewe anazuia mtu sabaKuna shule ubungo national housing ilikuwa ni evening class kwa secondary jamaa alileta vurugu siku tatu wanafunzi hawaendi shule.
Aksante kwa kumbukumbu hii! Nyongeza kidogo kwenye kumbukumbu hii wanafunzi waliokamatwa kwenye zoezi la utambuzi walipelekwa Segerea kufungua gereza jipya!SHULE YA TAMBAZA NA KUMBUKIZI YAKE.
Miaka hiyo shule hii ilivuma sana ikiwa inasifika kwa vurugu hasa katika michezo, hata hivyo ilikuwa inasifika kwa taaluma, wanafunzi wengi waliitamani na waliochaguliwa walipenda kuvaa sare za shule hiyo hata wakiwa nyumbani.
Awali shule hii ambayo ni moja ya shule kongwe na maarufu jijini Dar Es Salaam na hata Tanzania, ilikuwa chini ya umiliki wa shirika la Elimu la H.H, ilijengwa na shirika la Elimu la H.H. Aga Khan na kufunguliwa na H.H. Shan Karim Al Hussein, Aga khan IV Novemba 23 mwaka 1957, wakati huo ilikuwa inaitwa H H Aga khan Boys.
Udahili wa kwanza ulifanyika januari 14 mwaka 1958 ambavyo kama zilivyo shule nyingi za wakati huu kutoa elimu kwa makundi, hii pia ilitoa elimu kwa wanafunzi wenye asili ya Asia pekee.
Katika mwaka huo jumla ya wavulana 117 walidahiliwa, wote wakiwa na asili ya Asia, Ilipofika mwaka 1962, shule hii
ilianza kudahili wanafunzi wenye asili ya Afrika ambao pia walikuwa wakisoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
Katika kipindi chote hiki, shule hii ilikuwa ikidahili wanafunzi wa jinsia moja tu, ambao ni wavulana, mwaka mmoja baadaye 1963, shule hii ilianza pia kudahili wanafunzi wa kidato cha tano ambao kwa sasa walikuwa ni mchanganyiko wa wasichana na wavulana.
Katika kipindi chote hiki, Serikali ilikuwa bado haijataifisha shule hii, Hatimaye mwaka 1970 ndipo ilipotaifishwa, kisha jina lake kubadilishwa na kuitwa Tambaza.
Tangu kutaifishwa kwake, Tambaza ilikuwa ikipokea wanafunzi wa kidato cha Kwanza hadi cha sita mpaka ilipofika mwaka 1994 ambapo ilibaki kuwa ya kidato cha tano na sita tu, mabadiliko haya yalitokana na mfululizo wa matukio yakiwemo lile la, mwaka 1994, wakati wa michezo ya UMISETA Mkoa wa Dar Es Salaam, Ilipigwa mechi kati ya timu ya Sekondari ya Tambaza na Jitegemee katika uwanja wa Taifa Wilaya ya Temeke.
Kila timu ilikuwa imejiandaa vya kutosha, kipindi kile wanafunzi wengi wa Tambaza walikuwa na muonekano wa watu wazima, wengi walikuwa na ndevu hata kama ni kidato cha pili, pale shuleni kwao wauza askrimu walikuwa wanauza kwa mashaka, wakati mwingine walirudi bila mauzo, askrimu zote zililiwa na wanafunzi wa Tambaza.
Wengi walikuwa wanatembea mitaa ya mjini hawajachomekea mashati yao, au hawajavaa soksi, hakuna wa kuwauliza, walikuwa wababe tu, Siku hiyo ya mechi, wanafunzi wa Tambaza walishaanza kuongea mapema wakiwa jukwaani, kuwa siku hiyo haijalishi washinde au wasishinde lazima wafanye fujo, baada ya mpira kuanza, Jitegemee wakafunga goli la kwanza, walipoongeza la pili, vurumai ikaanza baada ya Tambaza kulikataa goli hilo.
Wanafunzi wa Tambaza walifanikiwa kumkamata mwanafunzi wakike mmoja wa Jitegemee wakamvua nguo ya ndani na kuitundika juu ya mti, wiki nzima yule msichana hakuja shule kwa aibu, kwasababu Tambaza walikuwa upande wa juu, waliyatumia yale mambao ya jukwaa kuwarushia Jitegemee waliokuwa upande wa chini.
Mbao zile zilikuwa zinakuja kama mapangaboi vile, ilikuwa unaweza ukafyekwa shingo usipokaa vizuri, vurugu ya mapigano ikiwa inaendelea baadhi ya wanafunzi wa jitegemee wakakimbilia shuleni kwao na kuwataarifu askari wa JKT, MP, ambao walianza kuja eneo la uwanja wa Taifa, Ghafla, Tambaza walipowaona MP, wakaanza kukimbia wakielekea kituo cha Keko.
Kundi la kwanza kufika kituoni likasimamisha daladala ya kwanza ili waingie ndani waelekee mjini, Konda alipokataa wasiingie wakampa kipigo akadondokea uvunguni mwa gari na kufariki. Siku ya pili daladala zote za jiji la Dar Es Salaam zikagoma kubeba abiria, ikabidi watu waende makazini, katika biashara na mashuleni kwa miguu au magari binafsi, Umoja wa Daladala Mkoa wa Dar Es Salaam ukadai unakwenda kumzika mwenzao.
Waliofuata wakatawanyika maeneo mbalimbali yakiwemo Chang'ombe, Temeke, Mbagala, Keko machungwa nk. Huku nyuma Jitegemee wakarudi shule, Mkuu wa Shule Fabian Massawe, akaitisha kikao uwanja wa damu, na kuwaasa wanafunzi wawe makini huko njiani wakielekea makwao, na kwamba kashatoa taarifa Polisi hivyo wawe waangalifu.
Siku ya pili tu akakamatwa mwanafunzi wa jitegemee na wanafunzi wa Tambaza akapewa mkong'oto mkali, akaenda shuleni kwao akiwa tumbo wazi, hana begi, viatu, soksi nk, kabakiwa na kaptura tu.
Masawe akawaonya wanafunzi wake watembee kwa makundi sababu hali ni mbaya, yakatokea matukio mfululizo ya kupigwa wanafunzi leo anapigwa wa Tambaza na kesho anapigwa wa Jitegemee, Polisi wakaanza kuwasaka Tambaza, wanafunzi wa Tambaza wakawa sasa wanakwenda shuleni kwao kiraia, wanabadilishia sare wakiwa shuleni kwao kukwepa mkono wa Polisi.
Kipindi hicho palikuwa na ma-School Bus ya wanafunzi, Rais akiwa mzee ruksa, Ali Hassan Mwinyi, Tambaza walikuwa wanavizia basi mpaka lijae, likianza kutoka tu ndipo wanaibuka toka uchochoroni na kulidandia, waliishi kwa mtindo huo mpaka kulipopoa wakiwakwepa askari kanzu.
Hata kwa upande wa magari aina ya, Chai Maharage, waliyavizia kwa mtindo huo, Serikali ikachoka ikaona iingilie kati baada ya wazazi na walimu kupiga kelele za malalamiko kuhusiana na ugomvi huo wa kati ya shule hizo mbili.
Ndipo siku moja Polisi wa kituo cha Chang'ombe wakapeleka karandiga Shule ya Jitegemee, ghafla walipokusanyika wanafunzi wote, Fabian Massawe, Mkuu wa Shule wakati huo, akawaeleza wanafunzi wake kuwa, kwa wale wanaowakumbuka wanafunzi wa Tambaza waliofanya vurugu wapande karandinga tayari kwa safari ya kuelekea Tambaza kuwatambua wale wote waliofanya vurugu siku ya mechi.
Baadhi ya wanafunzi wakajitokeza na wengi wao walikuwa wasichana, wakapanda karandinga na kuelekea Sekondari ya Tambaza, Siku hiyo Mkuu wa shule wa Tambaza alishawatangazia wanafunzi wote waje shule wakiwa nadhifu na wamechomekea mashati yao, asiyefika angekuwa kajifukuza shule yeye mwenyewe.
Ghafla karandinga lilipowasili Tambaza, walikuta wanafunzi wamejipanga mstari mmoja mrefu, Polisi kiongozi, bila hata ya kuchelewa akiwa na spika kwa sauti kali, akawatangazia dhumuni la ujio wao ule, huku wakiwa na walimu wote wa shule.
Polisi kiongozi, akaeleza kuwa wanafunzi wa jitegemee watapita mbele ya wanafunzi wa Tambaza na kuwatambua waliofanya fujo uwanja wa Taifa wakati wa mechi kati ya shule hizo mbili.
Baadhi ya wanafunzi wa Tambaza wakawa wanawatolea macho wanafunzi wa Jitegemee walipokuwa wanapita, nia ni kuwatisha wasiwaonyeshe kidole, kwasababu Kamanda wa msafara alishaonya mapema, kwamba, mwanafunzi yeyote atakayeonyeshwa kidole basi bila kuchelewa alitakiwa kukurupuka na kuelekea ndani ya karandinga, asiyefanya hivyo atakabiliwa na kipigo kikali kutoka kwa FFU waliokuwa wamesimama pembeni na marungu yao wakishuhudia Gwaride hilo la Utambuzi.
Wakatambuliwa wengi kati yao waliokuwepo katika vurugu ile na kupelekwa kituoni, baada ya wengi wa wazazi wao kupata taarifa, waliripoti Polisi na kuwahangaikia dhamana na wengi walitoka nje, katika kituo hicho.
Baada ya zoezi hili la gwaride la utambuzi, hali ya hewa ikatulia, pakawa shwari bila kusikika vipigo kati ya pande hizo mbili, ikawa wanafunzi hao wakikutana wanatazamana tu kama majogoo, huku wakitupiana maneno kama vile "Cheki wanga hao wanapita" au "Angalia watoto wa massawe hao, wachawi hao" nk.
Kwa mgogoro huo kati ya Tambaza na Jitegemee haukuwa ndio mwisho wa hekaheka za shule ya Tambaza, kwani haukupita muda mrefu jiji la Dar Es Salaam likashuhudia tena mgogoro mwingine kati ya Tambaza na Sekondari ya Azania, hapa sasa yalitumika mpaka mabomu ya chupa ya Petroli, hili sasa likathibitisha kuwa Tambaza ni wakorofi kwelikweli.
Vita kati ya shule hizi mbili ikadumu kwa muda pamoja na Polisi kuingilia kati na kuwakamata baadhi ya wanafunzi. Mwisho wa siku Wizara ya Elimu ikaona kuna shida kwa wanafunzi wa tambaza na kuamua kufanya maamuzi magumu ya kuisambaratisha Tambaza na kuibakisha ikiwa na kidato cha tano na sita tu.
Hilo pia halikusaidia kitu, kwani pamoja na Wizara kukataza shule zinginezo kupokea wanafunzi wa Tambaza, mashule mengi yaliwapokea wanafunzi hao zikiwemo zile za Kasita huko Mahenge, Minaki, nk. katika shule mojawapo ya Mahenge, Mkuu wa shule alifuatwa na wanafunzi wa shule hiyo, akaruka toka ghorofa ya kwanza hadi ya chini katika nyumba yake na kuvunjika, hadi leo ni mlemavu, nguruwe wa shule walikuwa wanakimbizwa huku wakiwa wanawaka moto, aliyekuwa hataki kushiriki vurugu alifuatwa na kulazimishwa.
Siku lilipofika karandinga la Polisi shuleni Kasita, wanafunzi wengi walikuwa wamekimbilia milimani, likafanywa paredi la utambuzi, kisha walipatikana baadhi baada ya kutajwa na walimu wao, wengine kwa kusikika sauti zao tu, baadhi wakafungwa miezi sita jela, na wengine walimalizia vifungo vyao Gereza la Kingolwira mkoani Morogoro.
Haikuwa mpaka miaka ya 1997 ndipo hali ya migomo na vurugu za wanafunzi zilianza kupoteza mwelekeo na kupungua taratibu mithili ya mvua ya vuli, na Serikali tayari ilikuwa imepata mwarobaini wa kuwashughulikia wanafunzi waliokuwa wanaanzisha vurugu mashuleni kwa kuwasweka lupango, hili liliwaogopesha wengi na kuamua kufyata mikia yao.
Toka mwaka 2015 shule hii ilikuwa na jumla ya wanafunzi 910 ,wavulana 595 na wasichana 315 ambapo baadhi ya michepuo wanayosoma ni pamoja na PCM, PCB, EGM, HGE, CBG na PGM.
Ina takribani walimu 83 wenye shahada za kwanza na uzamivu, kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50 ya uhai wa shule hiyo, tayari imeshatoa madaktari, wahandisi, wachumi, na hata wanasiasa.
Tambaza ni jina la mmoja wa waliokuwa wazee mashuhuri wa jiji la Dar Es Salaam aliyekuwa akimiliki eneo kubwa la ardhi katika eneo la Upanga, mahali ilipo shule hiyo.
Jina kamili la mzee huyu ni Jumbe Mohamed Tambaza, ambaye pia alikuwa muasisi wa Chama cha TANU, Mzee Tambaza alikuwa anamiliki eneo lote kuanzia ilipo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mpaka kwenye daraja la Salender.
Mzee Tambaza alitoa ardhi ili itumike kujenga majengo ya huduma kwa wananchi kama shule na hospitali. Kwa kumuenzi mzee huyo ndiyo maana shule hiyo ikapewa jina la Tanbaza.
Licha ya shule hiyo kutoa watu maarufu wakiwemo wanasiasa madaktari na wachumi na wasomi mbalimbali, inakabiliwa na changamoto ya uchakavu, na kutakiwa kupigwa rangi, katika baadhi ya majengo yaliyojengwa toka wakati wa ukoloni ambayo bado ni imara kutokana na aina ya ujenzi wake.
Licha ya jina lake kuwa kubwa, Tambaza haipo katika orodha ya shule zinazofanya vizuri hasa katika mitihani ya Taifa.
Mfano katika matokeo ya mitihani ya kidato cha sita mwaka 2009, watahiniwa walikuwa 459, huku waliopata daraja la kwanza wakiwa 33, daraja la pili 74, daraja la tatu 224, daraja la nne 72 na waliofeli 56.
Mwaka 2010 ,watahiniwa walikuwa 462, waliopata daraja la kwanza 18,daraja la pili 64 ,daraja la tatu 209 daraja la nne 85 na daraja sifuri 86.
Mwaka 2011 matokeo ya wanafunzi walifanya mitihani 428 ,wanafunzi 15 walipata daraja la kwanza, 51 daraja la pili, 189 daraja la tatu, 84 daraja la nne, na 88 daraja sifuri.
Matokeo hayo yalisababishwa na wanafunzi wenyewe kwa kuwa wengi wanategemea masomo ya ziada badala ya kuwa makini katika kujifunza.
Wengi wa walimu wanaotegemewa kwa twisheni siyo wazuri, matokeo yake ndiyo hayo wanakuja kufeli.
Wewe ni mdogo inaonekana na akili yako ni ndogo pia maana sioni connection kati ya mada na unachokiandika havina uhusiano wowoteLazima tulete nyodo. Watu hatujazaliwa nyie mko secondary leo tupo wote JF tunachati. Kuna sehemu mtakuwa mmekosea lazima naelewa now kwanini wengi humu hamuipendi CCM.