Kwanini Rais amepoteza mvuto kabla ya kutimiza siku 100?

Kwanini Rais amepoteza mvuto kabla ya kutimiza siku 100?

Usiniwekee maneno mdomoni..... nimeachana na nani?
Serikali yetu ipo imara
Huwezi mlinganisha SAMIA SULUHU au DR MPANGO na SALUM MWALIMU au TUNDU
Salum Mwalimu na Tundu wamewahi kuongoza serikali?

Ndio yale yale ya kujifanya kana kwamba CCM ndio kwanza imetutawala.

Amandla...
 
Salum Mwalimu na Tundu wamewahi kuongoza serikali?

Ndio yale yale ya kujifanya kana kwamba CCM ndio kwanza imetutawala.

Amandla...

Oook
Kumbe wangeshinda uchaguzi wangeongoza nini

Kweli Chadema ni wanaharakati🤔🤔🤔
 
Ndio mwenyewe sasa.JPM hafufuki move on maisha lazima yaendelee.Tulisema ajenge mifumo na sio mtu ndio mvumilie tu.Mama mitano tena

Who said kwamba JPM alikuwa bora?

Au kwamba tunataka afufuke?

Acheni kuwa insecure, kila anayewakosoa mnakimbilia kumtaja JPM, that man was disgrace, we thought his death will get us better but it is looking like we got the worst.
 
Habari wanaJF,

Katika uwanja wa siasa kwa ngazi ya Urais tumezoea kuona Rais aliyeingia Madarakani akijizolea umaarufu na sifa kedekede pindi anaposhika hatamu ya uongozi

Kipimo cha Rais huanza ndani ya siku 100 tangu ale kiapo. Lakini imekuwa kinyume kwa Rais wa sasa amekuwa wa kawaida sana ndani ya muda mfupi.

Nadhani yafuatayo yamechangia yeye kupoteza mvuto kwa kasi:

- Hotuba zake zimekosa msisimko, nadhani ni kwasababu Waandishi wake wamekuwa waki-copy na kupaste hotuba zake. Kila hotuba tunasikia yale yale (Taifa kufiwa, Jinsia yake, lazima aombe epewe muda nk)

- Wizara ya Habari inamuangusha kwa 100% watu wanatamani kuona ubabaishaji unaondoka Serikalini lakini ndani ya wiki Moja Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imetoa maboko mara mbili (1: BASATA na Wasanii, 2: Mechi ya Simba SC vs Yanga SC)

- Kuendelea kuwepo Madarakani kwa baadhi ya Watendaji ambao Wananchi tuliamini walipaswa kuondoka baada ya zama za Mwendazake kuisha. Ameondoka mmoja tu, yule aliyekuwa boss wa Manispaa ya Temeke. Lakini bado kuna wengine wengi wanapaswa kupumzishwa.

Hayo ni kwa uchache, nakushauri fanya yafuatayo kujinusuru dhidi ya chuki na visirani vya Wananchi kabla haujachelewa.

- Safisha Serikali yako, baki na watu Wenye weledi tu (mfano ni Mama wa Afya anapaswa kupumzika ametulaghai sana)

- Kama kuna wafungwa wa kisiasa basi nakusihi wape uhuru wao. Familia zao zinawapenda na kuwahitaji.

- Ile ripoti ya matumizi ya fedha Serikalini ambayo uliomba bado haijakamilika? kama tayari basi tuweke wazi na ikiwezekana watu wawajibike kama kuna makandokando

- Usijidanganye ukaendelea kugawa Mabenz ya Serikali au ya fedha za walipa Kodi. Wananchi hatuoni mantiki ya kufanya hivyo.

- Acha kuwa na hotuba zinazojirudia rudia. Siku hizi ukianza tu tunajua unakoelekea.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Ukiachilia mbali speech zake kukopi na kupest pia yeye mwenyewe jinsi anavyodeliver speech yenyewe inatoa mvuto kabisa aaaa. Kuna speech nyingi tu anainama mwanzo mwisho hiyo huwa inaboa Sana.
 
Sukuma gang mlikuwa mnafuja tu sasa teee ...hatutaki mvuto kinachotakiwa kutokuona maiti kwenye viroba coco beach..nchi imetulia tuliiii...
Kwamba nchi imetulia???? basi wewe hujui kinachoendelea nchini juu ya wastaafu wa nafasi za urais kulalamikiwa wakati ni haki zao kisheria, hujui kilichotokea Jmosi ya Dabi ya Simba na Yanga na mengine mengi! Fuatilia kisha utoe mrejesho iwapo kweli nchi imetulia!
 
Oook
Kumbe wangeshinda uchaguzi wangeongoza nini

Kweli Chadema ni wanaharakati🤔🤔🤔
Kumbe unazungumzia hisia zako? Watu hawajawahi kuwa Rais na Makamu wa Rais lakini unawafananisha na walioisha kuwa marais?
Unadhani uanaharakati ni tusi? Hata Nyerere mpaka Mwenyezi Mungu anamchukua alikuwa mwanaharaki.

Amandla....
 
Ukiachilia mbali speech zake kukopi na kupest pia yeye mwenyewe jinsi anavyodeliver speech yenyewe inatoa mvuto kabisa aaaa. Kuna speech nyingi tu anainama mwanzo mwisho hiyo huwa inaboa Sana.
Asante sana
 
Kumbe unazungumzia hisia zako? Watu hawajawahi kuwa Rais na Makamu wa Rais lakini unawafananisha na walioisha kuwa marais?
Unadhani uanaharakati ni tusi? Hata Nyerere mpaka Mwenyezi Mungu anamchukua alikuwa mwanaharaki.

Amandla....
Waligombea ili wawe nini kumbe🤣🤣🤣
 
Nyie ambao mnataka hotuba za kufokea watu na matusi ndio mnaona Raishana mvuto. Rais kwangu ana mataumaini makubwa sana hasa kwenye kukuza sekta binafsi iliyokuwa inapumulia mashine, na kurekebisha uhusiano na majirani na biashara za watanzania kuruhusiwa kuendelea kati yake na nchi jirani.

Sio kiki za kutembea na makamera muda wote na kufokafoka, matusi, rais sio celebrity kila siku kwenye camera na mitandaoni huku wananchi hali ngumu, biashara haziendi, ajira hakuna na majirani wametupiga pini
[emoji120][emoji120][emoji106][emoji106]
 
Hapendwi mtu wala chama bi dada.

Chadema au CCM, Mama au Jiwe? Tenda wema, utupe haki zetu, uhuru wetu, maendeleo yetu na zetu zote zilizopo. Tutakuwapo kukuunga mkono wakati wote kama watanzania wazalendo.

Mama anapotenda vyema tunampongeza, akienda fyongo tutasema kama watanzania wazalendo.

Yule wa awamu ile alikuwa akitenda fyongo mno ndiyo maana alivuna alichopanda!
[emoji120][emoji120]
 
16 bado ni Asilimia ndogo sana
Wewe mama ondoka huko kwenye mavyama. Sasahivi nchi imeshikwa na dereva asiyetaka aina hiyo ya makelele. Subiri uone na kama hujabadirika kisaikolojia, utaumia sana. Soon anakwenda kufanya yasiyowapendeza wana CCM, anamtazamo wa kitaifa huyu.
 
Back
Top Bottom