Kwanini Rais Magufuli alimfunga Kabendera?

Ndugu wanajamvi,

Tumesikia kuhusu kitabu kipya cha Erick Kabendera kinachoitwa "In the Name of the President: The Memoirs of a Jailed Journalist". Kabendera amefunguka kwa kina juu ya utawala wa Magufuli na madai ya udikteta. Hii inatufanya tujiulize maswali mengi kuhusu sababu halisi za kufungwa kwake.

Ni wazi kuwa Kabendera alikuwa mwandishi wa habari shupavu, lakini je, hatua za kumkamata na kumfungia zilikuwa za haki? Au zilikuwa juhudi za kumnyamazisha kwa sababu ya uandishi wake?

Kwa vile tunafahamu kwamba baadhi ya wanachama wetu hapa ni wafanyakazi wa idara za usalama, jeshi, na ulinzi, wafanyakazi wa ikulu na watumishi wa inner circle tunapenda kupata mitazamo yenu juu ya suala hili:

1. Je, ni nini hasa kilichosababisha Kabendera kuonekana tishio kwa utawala wa Magufuli?

2. Kuna ukweli wowote katika madai kuwa utawala huo ulitumia nguvu za dola kuzima uhuru wa vyombo vya habari?

3. Kwa maoni yenu, je, kufungwa kwa Kabendera kulikuwa na athari gani kwa tasnia ya uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania?

4. Kwa nini utawala wa Magufuli ulikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya waandishi wa habari huru kama Kabendera?

Tunaomba mjadala huu uwe wa kistaarabu, wa kina, na wa kuheshimu maoni tofauti. Ikiwezekana, tusaidiane kupata ukweli ili kuangazia mustakabali wa uhuru wa vyombo vya habari nchini mwetu. Jambo zuri ni kwmaba mzee hayupo tena kwa sababu kipindi cha utawala wake hadi hili jukwaa la siasa lilikuwa compromised. Niliwahi kupost threads zenye hoja na zilifutwa na maadmin bila sababu hali hii ikasababisha nilichukie sana hili jukwaa la siasa.

Karibuni kwa mjadala.

View attachment 3191541
Kule Israel, ukanda wa Gaza Netanyau kazuia Aljezira kurusha matangazo, na baadhi ya waandishi wameuwawa, unadhani kwa nini?, Usalama wa nchi kwanza
 
Ina maana walengwa(watumiaji) wa kitabu chake ni jamii gani? Watanzania au? Au hajui kiswahili? Kabendera ni mtanzania kweli?
Ndio ujue kwamba huyo mkimbizi Kibendera Hana nia njema na taifa hili Kwa hicho kitabu chake kukiandika Kwa lugha ambayo zaidi ya 80% ya watanzania hawaielewi.

Kwa ufupi tu amewalenga watu wa mataifa ya magharibi huko walikompa hifadhi... Na huu ni mwendelezo wa ukibaraka(kazi ambayo amekuwa akiifanya Kwa muda mrefu sana).
 
Kule Israel, ukanda wa Gaza Netanyau kazuia Aljezira kurusha matangazo, na baadhi ya waandishi wameuwawa, unadhani kwa nini?, Usalama wa nchi kwanza
Kuna majuha hapa wanaamini kila jambo linatakiwa lisululishwe kidiplomasia hata kama linahatarisha maslahi ya nchi.

Mara nyingi wasaliti/wakosoaji huwezi ukadeal nao kidiplomasia na ukafanikiwa, maana wao ni watu ambao wameamua kuwa anti-governmet, Sasa njia pekee na Bora ya kudeal nao ni kuwapoteza kabisa kwenye uso WA hii Dunia.... Na hicho ndicho kitu ambacho viongozi mahiri na shupavu popote pale duniani wanakifanya, anzia Kwa Putin uje mpaka Kwa Kagame.

Huyu Kibendera na watu WA aina yake ingekuwa ni Rwanda Wala hata wasingekuwa hai mpaka leo.
 
Kwa taarifa yako Mimi natamani siku Moja serikali ipige marufuku ukoo wote wa Magufuli kushiriki siasa Tanzania mpaka kizazi Cha 8.
Very ludicrous wishful thinking...

Kwa taarifa yako tu wewe utakufa hata kabla Hilo wazo lako la kipumbavu halijaskika popote.

Halafu unadhani kuwa mwanasiasa nchi hii ni dream ya kila mtu ehee?? Akili huna kabisa wewe
 
Kibendera kaandika kitabu Kwa ajili ya maslahi yake binafsi ya kufedha, pamoja na kujipa relief kutokana na uchungu alionao baada ya kuenyeshwa sana na serikali ya Magufuli uliompelekea kupoteza mzazi....!!

Na kafanya hivyo sababu Kuna wenzake wengi sana ambao bado wana uchungu kama yeye na wanahitaji relief ambapo wataipata kwa kumpa support ya kununua na kukisoma hicho kitabu.

Ila Kwa bahati mbaya kwao hakuna chochote kitakachabadili image na mitazamo waliyonayo watanzania kuhusu Magufuli.

Eti ameona aandike Kwa lugha ya kigeni kabisa hahahhaha..!!
Mnatukana tu lakini tatizo hakuna mtu anabisha kwa hoja wadau wake Magufuli na Media yake ya wakati ule kwanini hai pingi ukweli ? Kama ni uongo kwanini hawasemi lolote
 
Hakuna mtu mwenye akili timamu atapoteza muda wake eti anaenda mahakamani kupambana na kitabu Cha Kibendera, hili iweje Sasa?

Huyo Kibendera kama kweli yeye angekuwa ni jasiri na msema kweli basi angekitoa kitabu chake muhusika akiwa Bado yupo hai, maana Kwa vyovyote vile hii kesi lazima ingeenda mahakamani.

Sasa amesubiri muhusika hayupo eti ndio anatoa kitabu chake, halafu anatupa sisi ambao sio wahusika jukumu la kwenda mahakamani eti hili atoe uthibitisho wa haya anayoyasema, hiyo ni akili ya wapi???

Ni wajinga na wahanga wenzake WA awamu ya Tano ndio watamuona amefanya jambo la maana.
 
Basi kama ni kweli acheni lakini wengi wetu tunajua jamaa kasema ukweli. Ukweli unauma ishini vizuri na watu
 
Ndugu wanajamvi,

Tumesikia kuhusu kitabu kipya cha Erick Kabendera kinachoitwa "In the Name of the President: The Memoirs of a Jailed Journalist". Kabendera amefunguka kwa kina juu ya utawala wa Magufuli na madai ya udikteta. Hii inatufanya tujiulize maswali mengi kuhusu sababu halisi za kufungwa kwake.

Ni wazi kuwa Kabendera alikuwa mwandishi wa habari shupavu, lakini je, hatua za kumkamata na kumfungia zilikuwa za haki? Au zilikuwa juhudi za kumnyamazisha kwa sababu ya uandishi wake?

Kwa vile tunafahamu kwamba baadhi ya wanachama wetu hapa ni wafanyakazi wa idara za usalama, jeshi, na ulinzi, wafanyakazi wa ikulu na watumishi wa inner circle tunapenda kupata mitazamo yenu juu ya suala hili:

1. Je, ni nini hasa kilichosababisha Kabendera kuonekana tishio kwa utawala wa Magufuli?

2. Kuna ukweli wowote katika madai kuwa utawala huo ulitumia nguvu za dola kuzima uhuru wa vyombo vya habari?

3. Kwa maoni yenu, je, kufungwa kwa Kabendera kulikuwa na athari gani kwa tasnia ya uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania?

4. Kwa nini utawala wa Magufuli ulikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya waandishi wa habari huru kama Kabendera?

Tunaomba mjadala huu uwe wa kistaarabu, wa kina, na wa kuheshimu maoni tofauti. Ikiwezekana, tusaidiane kupata ukweli ili kuangazia mustakabali wa uhuru wa vyombo vya habari nchini mwetu. Jambo zuri ni kwmaba mzee hayupo tena kwa sababu kipindi cha utawala wake hadi hili jukwaa la siasa lilikuwa compromised. Niliwahi kupost threads zenye hoja na zilifutwa na maadmin bila sababu hali hii ikasababisha nilichukie sana hili jukwaa la siasa.

Karibuni kwa mjadala.

View attachment 3191541
Hapana alifushitakiwa Kwa money laundry ambayo alikuja Kili yeye mwenyewe
 
Sswa mimi mjinga ila jibu swali. Kabendera angepindua vipi hii nchi ilihali hata jeshi hana? Au ndo insecurities za jpm baada ya Kabendera kuhoji mambo ya ndnai ya familia ya JPM?
Unamjua bwana mmoja aliitwa Lugangira aliyeasisi jaribio la mapinduzi dhidi ya Nyerere, lile lililowahusisha kina Hans Pope?

Hakuwa hata na mgambo, mpiga push up wala baunsa mnyanyua vyuma.
 
1. Je, ni nini hasa kilichosababisha Kabendera kuonekana tishio kwa utawala wa Magufuli?

2. Kuna ukweli wowote katika madai kuwa utawala huo ulitumia nguvu za dola kuzima uhuru wa vyombo vya habari?

3. Kwa maoni yenu, je, kufungwa kwa Kabendera kulikuwa na athari gani kwa tasnia ya uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania?

4. Kwa nini utawala wa Magufuli ulikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya waandishi wa habari huru kama Kabendera?

View attachment 3191541
1. Alikuwa anatumika kuichafua nchi kwa makala zake za hovyo nje ya nchi, alitumika katika mnyororo wa kuwasaidia magaidi wa MKURA, Mkuranga,Kibiti, Rufiji, pesa zilikuwa zinatumwa kwake yeye anazisambaza.

Makala yake zikitumika kama cover ya kupata hizo pesa. Akiweka pressure wale magaidi wasizibitiwe, akizungumzia haki zao za kibinadamu bila kujali haki za binadamu waliouwawa na magaidi.

2. Uhuru wowote una mipaka. Huwezi kuchochea kuangamiza taifa lako, kuchochea ugaidi serikali yoyote duniani ikuache. Vyombo vya habari ni muhimu kuliko kitu chochote kujenga au kubomoa Taifa.

3. Ulisaidia kukomesha ugaidi MKURA ulioanza kusambaa kusini. Link yao kubwa ilipotea.

4. Ni mfano wa waandishi wanaotumiwa na mafisadi, idara za ujasusi za nje, kuliangamiza taifa lao.
 
Basi kama ni kweli acheni lakini wengi wetu tunajua jamaa kasema ukweli. Ukweli unauma ishini vizuri na watu
Well, kwamba wewe unaweza ukambaka mtoto wako WA miaka 16 na kisha ukamaliza na kumuua hapo hapo sio?

Yaelekea huyo Kibendera hata kesho akija na tuhuma kwamba mama yako alikuwa ni kahaba pale manzese na wewe alikupatia hapo hapo na huyo unayeamini ni baba yako sio baba yako halisi.... Bila shaka utamuamini Kwa 100% Kwa sababu ni Kibendera kasema sio?
 
1. Alikuwa anatumika kuichafua nchi kwa makala zake za hovyo nje ya nchi, alitumika katika mnyororo wa kuwasaidia magaidi wa MKURA, Mkuranga,Kibiti, Rufiji, pesa zilikuwa zinatumwa kwake yeye anazisambaza.

Makala yake zikitumika kama cover ya kupata hizo pesa. Akiweka pressure wale magaidi wasithibitiwe, akizungumzia haki zao za kibinadamu bila kujali haki za binadamu za waliouwawa na magaidi.

2. Uhuru wowote una mipaka. Huwezi kuchochea kuangamiza taifa lako, kuchochea ugaidi serikali yoyote duniani ikuache. Vyombo vya habari ni muhimu kuliko kitu chochote kujenga au kubomoa Taifa.

3. Ulisaidia kukomesha ugaidi MKURA ulionza kusambaa kusini. Link yao kubwa ilipotea.

4. Ni mfano wa waandishi wanaotumiwa na mafisadi, idara za ujasusi za nje, kuliangamiza taifa lao.
Aisee kama ni hivi, basi JPM alifanya kosa kubwa sana kumuacha aendelee kuwa hai, huyu kibendera uhai wake ulistahili kuishia kule kule jela alipokuwa amefungwa kipindi kile huku uraiani alitakiwa aje akiwa maiti tu.

He should have been executed for treasonous acts.
 
Ndio ujue kwamba huyo mkimbizi Kibendera Hana nia njema na taifa hili Kwa hicho kitabu chake kukiandika Kwa lugha ambayo zaidi ya 80% ya watanzania hawaielewi.

Kwa ufupi tu amewalenga watu wa mataifa ya magharibi huko walikompa hifadhi... Na huu ni mwendelezo wa ukibaraka(kazi ambayo amekuwa akiifanya Kwa muda mrefu sana).
Nakubaliana na wewe mkuu.

Nina wasi wasi na uraia wake ila ili jina la Kabendela ni la kinyarwanda kabisa.
 
Aisee kama ni hivi, basi JPM alifanya kosa kubwa sana kumuacha aendelee kuwa hai, huyu kibendera uhai wake ulistahili kuishia kule kule jela alipokuwa amefungwa kipindi kile huku uraiani alitakiwa aje akiwa maiti tu.

He should have been executed for treasonous acts.

Alikuwa na huruma za kibidamu, alifiwa na mama yake, lakini pia kulikuwa na pressure kubwa kutoka vyombo vikubwa vya habari vya magharibi hasa vya Uingereza na balozi zao kulinda asset yao walikuwa wanaenda kumtembelea mahakamani wakiiomba serikali imwachie.

Kwa kukomesha ule ugaidi actually Magufuli ameongeza uhuru kwa Watanzania wote na hasa uhuru wa vyombo vya habari hasa Pwani, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Tunduma, mpakani na Msumbiji. Sehemu hiyo yote magaidi walitaka iwe himaya yao. JPM asingesimama leo tungekuwa na matatizo mengi sana.

JPM alitoa order hataki mateka. Hakuna kukopeshana walipwe haki zao kikamilifu on spot with fair bit of interest. Kwamba magaidi wote waangamizwe hakuna longolongo, kwenda mahakamani. Kwake JPM ile operation ilikuwa sensitive sana kuliokoa taifa hili.

Kabendera yeye ndio alikuwa kiungo wao muhimu coordinator wao pia kiungo muhimu magaidi wasiwindwe mchana na usiku, jeshi lipunguze kuwasakama. Alipiga kelele nyingi kupitia report zake, tuwekewe vikwazo, wawekezaji wasije Tanzania, tume za uchunguzi zije kutoka ulaya.

Ilifikia wakati watu waliogopa kufanya shughuli zao, za kijamii, kiuchumi shughuli zao zozote kwa kuogopa kutekwa na kuuwawa hayo maeneo.
 
Back
Top Bottom