Kwanini Rais Samia huwa anacheza vizuri halafu mambo yanapoelekea kukaa sawa anabutua?

Mataga na Hardliners wa jiwe ndio wanaokoroga mambo, bado wako na hangover. Jambo la kushangaza hawaondoi kwenye system!
 
Kuifungua nchi kwa kuwaumiza wale unaowaongoza mimi naona ni ujinga tu, kwangu mwerevu akishafanya kosa na akagundua amekosea hubadilika, lakini kuendelea kukomaa kutenda kosa ni ujinga.

Hii consistency ya aina hii ni majanga, sio ya kupongezwa.
 
Ni kama JK alivyofanya kwenye ishu ya Katiba Mpya,alianza vizuri lakini hotuba aliyoitoa kwenye Bunge Maalum la Katiba iliharibu kila kitu,kazi yote nzuri iliyofanywa na tume ya Jaji Warioba ikachakachuliwa na wanaccm.
 
Ongeza hii

Kaongeza mishahara, Kaongeza posho. Watu wakati wako kwenye lindi la furaha.

Mara paaa. Kaleta kikokotoo watumishi wastaafu kuanzia July hawatapata tena 50% ya mafao yao bali watapata 33%. Hii inatupa mashaka na ubora wa Rais wetu.
 
Umeongea uongo mtupu
 
Yaani anapiga ndole mpaka mpira unafumuka?
 

Hangaya hana confidence na maamuzi yake, Nakumbuka baada ya mfanyabiashara wa madini na askari kuuwawa kule Mtwara aliunda tume kuchunguza vifo vile; lakini mpaka leo Sirro bado anadunda na hakuna lolote linaloendelea zaidi ya kusema kutokana na malalamiko juu ya polisi amewaongeza nao polisi wawemo kwenye tume yake ya Katiba!!! It is pathetic!
 
Huyu si ndiye alisema wapigwe tu.Watu wamekaa madarakani mpaka wamestaafu,wamekuwa wazee bado wanapewa vyeo vya ajabu ajabu.Wakati mwingine ni kudhalilisha cheo cha mtu.Waziri mkuu mstaafu (mzee) yupo kwenye kikosi,spika wa bunge mstaafu Anne (mzee)Mkiti Sensa ya makazi.

Hawa wasomi waliosoma na maphd yao vijana wapo tu,wala hawaonekani wala hakuna anayewajali.Inasikitisha sana
 
Kaongeza posho na malipo ya kazi maalum kwa bajeti iliyopigiwa kwa rates za zamani. Hii ni siasa na hapo maana yake posho hizi zitakuwa effected sawasawa kwenye bajeti ya 2023/24 na siyo 2022/23.

Mathalani; Ulikuwa unamlipa mtu posho ya 100,000 kwa siku 10 kila mwezi ambayo ni sawa na milioni kwa mwezi na kwa mwaka ulimtengea bajeti ya 12,000,000. Mwaka unaofuata unatenga hiyo hiyo 12,000,000 na unatangaza sasa posho nitakulipa kwa rate ya 200,000 badala ya 100,000 na itaanza kulipwa Julai mosi ila utatumia bajeti ile ile ya 12,000,000 kwa mwaka. Maana yake hapo umepandisha kiwango ila umefix kwa bajeti ile ile, hivyo hata mlipaji atakulipa 200,000 mara siku 5 badala ya 10 ili asivuke bajeti iliyotengwa ya 12,000,000. Hizi figure ni mfano tu lakini mtakuwa mmeelewa siasa iliyochezwa hapa.
 
Nchi nyingi hasa za Africa zinashindwa kuwa na siasa nzuri zenye kuheshimu sheria na haki za binadamu sababu viongozi wake ni waoga. Matokeo yake wanavunja sheria kwa maana ya katiba, wanavunja haki za binadamu. Kwa uoga wao wanatumia mabavu kwa kuhofia kesho yao!. Kiongozi anayefuata sheria huku akiwa hana chembe ya wizi hana haja ya kuogopa kwa kutumia vyombo vya dola kujenga hofu miongoni mwa wananchi. Rais Samia atang'ara kwa kuwa anafuata katiba na hafikirii kuwa na makundi au matabaka. Amejitahidi kwa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…