Kwanini Rais Samia naye anataka kutumia mabavu kutawala? Umuombee dua gani?

Kwanini Rais Samia naye anataka kutumia mabavu kutawala? Umuombee dua gani?

Si anajua raha ya urais. Anamalizia awamu ya Magufuli Halafu aanze 10 more years za kwake. Huyu ni mzanzibari, she doesn’t care. Matunda ya mwungano hayo. This is the woman who told us Magufuli was not sick but resting when he was actually dead. All that forgotten, mama mama mama!
Kweli aisee. Watu hawawajui vizuri Wazanzibar. Never Under rate them. Alishindwa Kusema Rais anaumwa japo wanaompenda wakamwombea Dua?
 
mara ya mwisho kusikia mwanamchi anahitaja chadema mtaani ilikuwa duh muda sana
 
Marais wote toka ccm watakaofuata baada ya Magufuli, watafanya kazi kwa kubanwa sana.

1) Kulazimika kuendeleza miradi ya Magufuli iliyoungua bila kuiva, ambayo inagharimu kuliko uwezo wa nchi, iliyokuwa inategemea fedha za "Dhulma".

2) Kwa kuwa ccm ni chama mfu kinachojiegemeza kwenye Dola, watalazimika kuvibana vyama vya upinzani visifurukute. Wataoneshwa mfano wa Kikwete aliyejaribu kuwapa wapinzani mwanya kidogo tu, wakachukua nchi uchaguzi wa 2015, sema tu ilibidi mbinu za ziada zitumike kupindua meza.

3) Kutokana na rushwa kushamiri, mipango mibovu, historia mbaya, ccm imeshindwa kuleta ufumbuzi wa Kweli wa matatizo ya nchi. Imeishiwa pumzi. Ubabe ni muhimu, na suala la Katiba mpya litaleta matatizo zaidi kwa ccm.

4) suala la Muungano ni bomu linalongoja kulipuka muda wowote. Angalau ccm inahitaji kuwepo madarakani ili ilikalie bomu hilo. Chama kingine kikiingia madarakani, kitalitegua na kuufumua Muungano. Wachawi wa ccm hawataki kusikia habari hiyo. Wako radhi kuficha kichwa mchangani kama mbuni
Tinataka katiba mpya.
 
Haiwezekani unazuia mikutano ya kisiasa wakati katiba inaruhusu, huwezi kuzuia watu kujadili katiba ya nchi wakati siyo uhaini wala hakuna katiba iliyovunjwa. Hivi kwani Uchamungu umekua ni msamiati mzito sana kwa watawala wetu?

Unaweka makatazo batili maana yake nini? Yaani tusubiri ujenge uchumi wakati mambo mengine hayasubiri? Haya makatazo ni kwa mujibu wa sheria ipi?
msimuombee mabaya , sala iwe "Mungu wa Israel ampende"
 
Nilimpenda sana huyu mama alipoingia madarakani, lakini sasa naona ameanza kushindwa kwa speed kubwa mno! Huu ni ushindi mnono sana kwa 'watesi wake' ndani ya chama lake. Lakini huyu mama yeye anafikiria wabaya wake wako nje ya ccm! Hili ndio kosa linalokwenda kumgharimu huyu mama!
 
Back
Top Bottom