MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
Nilishangaa mno ile ya mara ya Kwanza kuona Wakazi wa Zanzibar hawakupewa nafasi ya Mwili kwenda Kisiwani Kuagwa ila kwakuwa jana Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (atokaye Zanzibar) Kaapishwa leo mmeiweka.
Kama kuna Upuuzi mkubwa niliouona katika Ratiba mpya (iliyobadilishwa) ni kuona tarehe 22 Mwili utakuwa Dodoma halafu tarehe 23 utakuwa Zanzibar na tarehe 24 utakuwa Mwanza.
Mlioipanga hii Ratiba Vichwani mwenu mko vizuri kweli? Yaani Mwili muutoe Dar es Salaam kisha muupeleke Dodoma halafu urudi Zanzibar (nyuma ya Dodoma Kijiografia) na baadae Mwanza?
Kwanini Mwili baada ya kuutoa Dar es Salaam kwasababu ya ukaribu wa Kijiografia usiende Zanzibar kisha ndiyo uende huko Dodoma, Mwanza na ukamalizie Kwao Chato Mkoani Geita?
Na kwanini hii (hiyo) Ratiba inabadilika mno? Mlishindwa nini tu Kujipanga na Kuipanga vyema ikaeleweka? Na nini kiliwafanya mwanzoni Wazanzibari mliwasahau Kuwajumuisha wakati nao ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Mlitusisitiza sana kuwa Marehemu atazikwa tarehe 25 na Ratiba yenu mpya ( mliyoibadili ) mnasema sasa atazikwa tarehe 26. Je, na Siku za Mapumziko nazo zimebaki zile zile Mbili au sasa baada ya Kuibadili tena Ratiba sasa kuna Siku ya Tatu ya Kupumzika / Mapumziko?