Kwanini RC wa Manyara, Makongoro Nyerere alimpigia saluti ya kijeshi Rais wakati wa kiapo?

ngaiwoye

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
2,150
Reaction score
3,225
Wakuu, naomba kuuliza kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Je ni mwanajeshi mstaafu ama mwandamizi?

Nadhani wengi wetu hatufahamu. Makongoro Nyerere anakubalika sana na wananchi. Sisi wananchi tumefurahi Sana Mh. Rais wetu kuikumbuka familia ya baba wa Taifa.

Your browser is not able to display this video.
 
Ni mihemko tu ya kulamba uteuzi kimasihara! Kwani hata kama ni mjeshi mstaafu salute za kijeshi hazitolewi tu kienyeji, zina kanuni zake. Sasa mtu hata sare hajavaa anapiga salute hiyo miongozo ni ya jeshi gani??
Nakupinga kwa miguu na mikono yote watoto wa Nyerere wote hawana hulka hizo, huyo Makongoro angekuwa wa kujipendekeza angekuwa mbali sana na angekuwa MTU mkubwa sana hapa Tanzania.
 
Ni huyu ndiyo aliulizwa na mwandishi "Nasikia unapenda sana wanawake" akajibu kwa swali "Sasa ndugu yangu ulitaka nipende wanaume?"
Nadhani alimaanisha anapenda wanawake akiwemo Rais Samia.
Sema Makongoro ni muongeaji sana kwahiyo maelezo yake yalikuwa marefu, hayakufika mwisho.

Makongoro ni mtu wa comedy sana.
 
Ni mihemko tu ya kulamba uteuzi kimasihara! Kwani hata kama ni mjeshi mstaafu salute za kijeshi hazitolewi tu kienyeji, zina kanuni zake. Sasa mtu hata sare hajavaa anapiga salute hiyo miongozo ni ya jeshi gani?
Hakupiga saluti, alitoa heshima ambayo mwanajeshi yoyote ambae hajavaa uniform anapaswa kuitoa.
 
Ni mihemko tu ya kulamba uteuzi kimasihara! Kwani hata kama ni mjeshi mstaafu salute za kijeshi hazitolewi tu kienyeji, zina kanuni zake. Sasa mtu hata sare hajavaa anapiga salute hiyo miongozo ni ya jeshi gani??
Alibana mikono kwa ukakamavu na kunyanyua visigino mbele ya amiri jeshi mkuu.
 
Anafaa sn kwa kweli
 
Hangover is real.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…