A
Anonymous
Guest
Habari wadau,
Kwanza napenda kuipongeza Serikali kwa kutuletea huduma ya umeme kupitia mradi wa REA katika Kijiji cha Mwalugulu, Kata ya Mwalugulu, Halmashauri ya Msalala.
Kijiji cha Mwalugulu ni miongoni mwa vijiji vilivyopangwa na kupimwa vizuri tangu enzi za Mwalimu, hususan katika mpangilio wa maeneo na barabara.
Wananchi waliopata maeneo katika kijiji hiki wamekuwa wakiheshimu mipaka na miliki ya barabara (road reserve), wakifahamu kuwa maeneo hayo yanatakiwa kutumika kupitisha miundombinu ya Serikali. Hata hivyo, katika usambazaji wa umeme, REA wamepitisha miundombinu hiyo kwenye baadhi ya maeneo bila kuzingatia mipaka hiyo.
Mimi nina kiwanja ambacho nimekiendeleza kwa kuzingatia miliki ya barabara, lakini REA wamepitisha nguzo za umeme katikati ya kiwanja changu na kukigawa katika sehemu zisizo na mpangilio, hali iliyoharibu mpango wa matumizi ya eneo hilo.
Naomba ushauri kutoka kwa wadau; je, katika hali hii ninastahili kudai fidia kutoka TANESCO au mamlaka husika? Ni hatua gani ninazopaswa kuchukua ili kupata haki yangu, kwa kuwa mimi nilizingatia na kuheshimu eneo la hifadhi ya barabara?
Ufafanuzi soma ~ TANESCO yasema imeanza kuchukua hatua kutatua changamoto ya miundombinu ya hifadhi ya barabara