Kwanini Redio nyingi hapa Tanzania siku ya Ijumaa wanapiga zaidi nyimbo za kaswida za Kiarabu kuliko Kiswahili?

Kwanini Redio nyingi hapa Tanzania siku ya Ijumaa wanapiga zaidi nyimbo za kaswida za Kiarabu kuliko Kiswahili?

HOPEfull

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
1,882
Reaction score
2,313
Ndugu waamini wa dini mbalimbalini nawasalimu kwa jina la bwana muumba wetu.

Siku ya Ijumaa ni siku ya ibada na mara nyingi inakuwa kama ni siku nusu ya kazi kutokana na waamini wengi wa dini ya Kiislam kwenda kusali.

Sasa hata kwenye redio zetu ambazo ni nyingi sana kwa sasa hapa Tanzania muda wa saa nane na saa tisa huwa wanaweka vipindi vya mawaidha ya Kiislam au mahubiri ya dini ya Kiislam ambayo wakati mwingine yanakuwa mubashara kutoka sehemu husika.

Baada ya mawaidha hizi redio zetu ambazo kwa sasa ni nyingi huwa wanaweka nyimbo za kaswida ambazo mimi huwa nazipenda sana lakini sasa nyimbo nyingi zinakuwa kwa lugha ya kiarabu. Hivi hapa kwetu Tanzania hatuna nyimbo za kaswida za Kiswahili?

Hizi nyimbo za dini za Kiarabu ni nzuri na zina maadili na mapigo yanayoendana na dini lakini tatizo linakuja kwenye lugha. Sasa kitu ninachowauliza hawa wamiliki wa radio hawana kaswida za Kiswahili? Ninajaribu kubadilisha stesheni karibu 5 za redio muda huu wa saa tisa lakini kote unakuta hali ni ile ile.

Siku ya Jumapili ambayo ni siku ya ibada ya Wakristu huwa redio wanapiga nyimbo za dini wakati wa asubuhi na nyimbo zinasikika na kuelewa wanachoimba. Sasa kwanini siku ya Ijumaa hizi redio zetu nyingi nyingi wasituwekee na sisi nyimbo za kaswida za Kiswahili au wawe wanatuchanganyia za Kiswahili na Kiarabu?

Tatizo ni nini? Studio hawana au wanafanya kazi ili mradi siku ipite mtu aweke kibindoni chochote kitu, au hawana ubunifu wa kuendesha vipindi vya dini?

Hapa Tanzania huwa nahudhuria harusi au sherehe za maulidi mbona huwa nakuta waimbaji wengi wanapendeza na mavazi mazuri na watoto wamevaa vizuri wanaimba kaswada safi kabisa, sasa kwanini taasisi kama redio inakosa hizi nyimbo za kumsifu Mungu kwa Kiswahili?

Unakuta nyimbo ni nzuri lakini sasa tatizo linakuja kwenye lugha.

Ninategemea kupata mrejesho mzuri kutoka hizi redio.

Kuna mwanamuziki mmoja maarufu wa mziki wa taarab alikuwa anaimba kwenye majukwaa lkn baadae nikasikia ameacha kuimba huko na kurudi kwa bwana mimi ningemsihi kama yupo basi itapendeza kama ataimba nyimbo hizi za kumsifu Muumba.Sijui yupo wapi kwa sasa.
 
Kiarabu si ndiyo lugha yenyewe ya ibada kwa Waislam? Tatizo lipo wapi mkuu?
 
Umefungua Wapo redio au redio Maria ukasikia hivyo?
 
mbona redio nzyingi juma pili wanapiga nyimbo za kikristo na kwaya na mahubiri juu waache wanaoenjoy kaswida wale raha zao au ulitaka wapige milio ya vijambo vya baba yako?
kuna harufu ya udini kwenye hii post hasa pale ulipouliza ijumaa na kaswida wakat hata j2 tunaskia vipindi kuanzia asubuh mpka jioni mambo ya kristo sjui kufa msalabani nyokoooo
 
mbona redio nzyingi juma pili wanapiga nyimbo za kikristo na kwaya na mahubiri juu waache wanaoenjoy kaswida wale raha zao au ulitaka wapige milio ya vijambo vya baba yako?
kuna harufu ya udini kwenye hii post hasa pale ulipouliza ijumaa na kaswida wakat hata j2 tunaskia vipindi kuanzia asubuh mpka jioni mambo ya kristo sjui kufa msalabani nyokoooo
Hujanielewa mimi nina maana ya kaswida za kiswahili na sio za kiarabu zaidi.Kaswida zoye ni nzuri za kiarabu ilq zakiswahili huwa sizisikii.
 
Back
Top Bottom