Hizi ni simulizi za marehemu babu yangu (Mkiwa), ambae alishirikiana sana na mangi (Yohana) baba yake kama sio babu yake Justin Salakana, zamani hizo robo tatu ya Rombo yaani kutoka mto Ugwasi hadi Tarakea lilikuwa eneo la Kenya.
Babu yangu na mangi Yohana walipewa kazi ya kwenda kutoa taarifa kwa mangi Mareale kule Mwika ikitokea wenyeji wa Kenya wameingia na kuanzisha makazi eneo hilo baada ya kuchukuliwa na Tanzania.
Kwa uaminifu wao, walilinda ile mipaka kwa maana kwamba, wakenya walikuwa wakiingia maeneo hayo ya Rombo na kuwafukuza watanzania, kuwachomea nyumba zao na hata kuwaua maana walikuwa na silaha kali za jadi, hivyo ilikuwa ikiwalazimu watz hao kukimbilia misituni.
Babu yangu na mangi Yohana wakiona hayo walikuwa wanafunga safari kwa miguu kutoka huko Useri na Tarakea hadi Mwika kwa Mangi Mareale kutoa taarifa maana wakati huo hakukuwa na simu wala magari, wakishafikisha ujumbe huo, Mareale anatoa taarifa serikalini pale Moshi, jeshi linaenda kuwafukuza hao Wakenya wanarudi kwao.
Huo utaratibu uliendelea hadi uvamizi huo ukaisha na Rombo kubaki Tz na wakati huo watu wakawa wanaongezeka hadi kukajaa watu na kuwa eneo halali la upande wa Tz hadi leo.
Suala la changamoto ni kuwa; tangu wakati huo hadi leo wale watu wanaoishi eneo hilo maana lengo lilikuwa mlima Kilimanjaro ulio mrefu kuliko milima yote barani Afrika uwepo Tanzania lakini wale wanaoishi chini ya ule mlima hawanufaiki kikamilifu na mlima huo tangu enzi hizo za mababu, baba, watoto, wajukuu hadi sasa kuna vitukuu!
Pesa inavunwa pale inapelekwa DSM, ile kidogo sana inayobakizwa tangu enzi hizo haionekani hadi leo hii ule mlima haujanufaisha wakazi wa kule kimaisha.
Eneo kubwa la Rombo hasa lile linalopakana na Kenya, wakazi wa kule ni watanzania ila ni kama wanaishi Kenya! Kwanini? Radio, tv zinazoshika kule ni za Kenya, hata mitandao ya simu access kubwa ni ya Kenya kwani ukifika kule unatumia mfano mtandao wa vodacom, display inakuwa safaricom n.k.
Kwahiyo wanazielewa habari za Kenya kuliko Tanzania. Mambo yanayoendelea Tanzania hadi wayasikie idhaa ya kiswahili ya Kenya (KBC).
Kwa mustakabadhi huo siku siyo nyingi atajitokeza mangi mwingine ashinikize watu wa kule kupiga kura ya kutambua Rombo ni eneo la kenya kama ilivyofanyika Crinnes huko Urusi na Ukraine maana ukiangalia mpakani mwa kenya na rombo ni vitu viwili tofauti kabisa wakati kipindi hicho cha mababu kulikuwa sawa.
Ukiangalia Custum ya Tarakea upande wa tz na upande wa kenya, nenda mji wa Taveta, hadi kuna uwanja wa ndege! Lakini rombo iliyopo tz imesahaulika sana kimiundombinu, huduma za jamii katika mawasiliano ya vyombo vya habari n.k
WITO WANGU SERIKALI IONE HILO MAPEMA.
hata hilo soko la kisasa linaloimbwa kila siku litajengwa Mwika, bado ni kitu kidogo sana japo ni soko la SIASA. Kwanini kusijengwe uwanja wa ndege ili watalii watue kule moja kwa moja? Hatuoni watatua Taveta na kuendelea kuikosesha Tanzania mapato? Serikali yangu, mangi anakaribia kurudi Rombo!