Kwanini Rwanda wametuzidi katika hili?

Kagame Kiongozi iliyeweza kuwatawala watu wake ila ameshindwa kuuongoza mdomo wake.
 
Kwani tumepitwa na Rwanda tu katika Africa, au wewe unaona huu ni muda wa kulinganisha Rwanda na Tz? Kukua kwa uchumi kuna faida gani kama hakuakisi maendeleo halisi ya watu?
 
Inanipa shida pale wachangiaji wengi wakiacha kujadili mada na kuanza kujadili watu, na haiingii akilini pale ambapo mtu anaacha kuvumilia hoja ya mwenzake hata kama ni mbovu na kuanza kufulumusha matusi!
Tuweni wastaarabu jamani, ukweli ni kwamba humu watu wanatofautiani vyama (siyo itikadi), lakini isiwe sababu ya kutukanana, kama cha kujibu huna si ukae kimya tu.
 
Rudi huko kwenu Rwanda ukamilishe idadi ya wahamiaji haramu waliovuka mpaka
 
Tanzania tuna serikali dhaifu,Inatakiwa tufungue soko la kimataifa la dhahabu,almasi,tanzanite,uranium,gesi uchumi ungepaa kuliko!

Serikali ikufanyie kazi na wewe ubaki kwenye kiti umenyoosha miguu ukisubiri kulishwa.
 
-------- mkubwa wewe swali gani hilo? Ukuaji wa uchumi wa rwanda si endelevu kwasababu hautegemei nguvukazi ya wanyarwanda bali mali asili zinazoporwa kutoka drc, vta ya kongo ikikoma hata panadol mtakuwa mnakopa .

Huo ni mtazamo wako ambao ni hasi.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Watz hatujui matusi kama anayoyatoa mwenzetu. Nina wasiwasi na uraia wake. Si ajabu ni kati ya wahamiaji haramu huyu
 
Badilisha jina ujiite bongoamka utaona mabadiliko jinsi utakavyochangia michango chanya tofauti na sasa unapotumia jina la bongolala. Hilo jina waachie chadema

You are mistaken. Chadema waliamka tangu juzi wako macho kisawasawa na tena wamekaa kikazi zaidi.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ni kwababu Rwanda wanaishi kwa wizi wa mali za DRC, na ndiyo maana Kagame hakutaka ushauri wa Kikwete because anajuwa wamekwisha kiuchumi.
 
-------- mkubwa wewe swali gani hilo? Ukuaji wa uchumi wa rwanda si endelevu kwasababu hautegemei nguvukazi ya wanyarwanda bali mali asili zinazoporwa kutoka drc, vta ya kongo ikikoma hata panadol mtakuwa mnakopa .

Tuache vitu vya kufikirika una ushaidi juu ya wizi huo kama ni hivyo sisi tuna madini mengi ambayo hao Rwanda hawana lakini je tunayatumia katika kuwaletea watu maendeleo? kama sio yanaishia kwa watu wachache tu na wanufaika zaidi ni tunaowaita wawekezaji.

Mimi nafikiri tunashindwa kuelewa mada hapa uCCM na uCDM unatokea wapi ndugu habari hii imesomwa na ITV na imeeleza uhalisia jamani tuache ujinga wa kujiondoa akili na kuwaza CDM kila kikicha.

Unajua hawa wana CDM wote akili zao nyembamba tu kuanzia mwenyekiti wao hadi wana JF, nadhani umempa jibu ambalo ni kama ameendekeza u-form four ataishia kutukana tu.
Kwa hiyo kwa akili yako hata yule Mtangazaji wa ITV aliyeitangaza habari hii ni CHADEMA kuweni na akili mnaposoma na kujibu thread unatakiwa uelewe nini hasa kilichoandikwa na source ya habari ni ipi.

Wandishi wa habari wa KAGAME siku hizi mko wengi sana humu JF, mbona mnamsahau SLAA wenu jamani si ndo mwajiri wenu?
Katika hoja hii Dr. Slaa anaingiaje ndugu? kama huna cha kuchangia kausha usijivue akili ndugu

mawazo dhaifu kama haya lazima yataiona serikali ni dhaifu, uchumi wa rwanda unakuwa? nenda ukajionee maisha ya kishenzi wanayishi sasa.
Umeandika kinadharia zaidi Rwanda kwa sasa wenzetu wanakaribia kuondokana na nyumba za kuhezeka kwa Nyasi na udongo 90% ya wakazi wa rwanda kwa sasa wanaishi kwenye nyumba za Bati na hili limefanyika kwa serikali kukopesha mabati kwa watu wake kwani hata wakulima wamekopeshwa na kipindi cha mavuno ulipa mavuno yao au fedha.

umeonae, wanafikir KAGAME atawagawia madini anayoiba KONGO, watatembeza sana mabakuli kwenye mikutano ya M4C
Huna hoja ya kuandika ungekaa kimya, ulichokiandika hakishabihiiani na mada iliyopo mezani.

Daaa kwa comment hizi tanzania tuna miaka mia ijayo kumfikia kagame

huyu ni mmoja wapo wa watumwa wa kagame
Rudia ulichokiandika halafu soma mada iliyo mezani kama vinaendana na kwa mawazo kama haya ndio mmeifikisha CCM hapa ilipofika

hana sifa ya kuitwa mtanzania huyu mtumwa.
Mimi ni Mtanzania kuliko wewe hapa tunachofanya ni kuishtua serikali iweze angalau kuiga mazuri wanayofanya wenzetu lakini nyie anaewakosoa mnamuona adui

Kwani tumepitwa na Rwanda tu katika Africa, au wewe unaona huu ni muda wa kulinganisha Rwanda na Tz? Kukua kwa uchumi kuna faida gani kama hakuakisi maendeleo halisi ya watu?
Hili lipo Tanzania tu pekee wenzetu kule uchumi unakua na maendelea ya watu yanaonekana pia, tafuta takwimu utaona ukweli wangu

Rudi huko kwenu Rwanda ukamilishe idadi ya wahamiaji haramu waliovuka mpaka
Kwa hiyo turudi Rwanda mimi na huyu mtangazaji wa ITV? maana yeye katoa kwenye TV na mimi nimeileta hapa JF
 
Ni kwababu Rwanda wanaishi kwa wizi wa mali za DRC, na ndiyo maana Kagame hakutaka ushauri wa Kikwete because anajuwa wamekwisha kiuchumi.
Kama ni kweli Yeye anaiba DRC anaijenga nchi yake huku kwetu wanaiba wanakwenda kuzificha fedha mabenk ya nje ya nchi kwahili nani afadhari?
 
Kama ni kweli Yeye anaiba DRC anaijenga nchi yake huku kwetu wanaiba wanakwenda kuzificha fedha mabenk ya nje ya nchi kwahili nani afadhari?

Yote ni majanga kwani wananchi wa DRC wanateseka kwa manufaa ya Rwanda na hapa tunateseka kwa ubinafsi wa viongozi wetu wasanii na wauza unga.
 
Hili lipo Tanzania tu pekee wenzetu kule uchumi unakua na maendelea ya watu yanaonekana pia, tafuta takwimu utaona ukweli wangu

Hili ni jibu la kubabaisha, kukubali kutojua kila kitu ni kujua vilevile. Wewe ndio unaosema kwamba uchumi wao unaenda sambamba na maendeleo ila hutaki kutuhakikishia hilo na badala yake unataka sisi tukufanyie homework. Kama huwezi ku prove unachosema kwanini useme at first place? Njoo na hizo takwimu zinazopima maendeleo ya Rwanda vs ya Tanzania na cha muhumu ningeomba u define na kutetea kipimo utakachotumia kutuaminisha kwamba uchumi wa Rwanda unaenda sambamba na maendeleo yao.
 
Ukisifiwa na bank ya dunia fahamu umekwisha. Angalia China walibezwa miaka yote hata ujiko wa kuwa permanent Member wa UN walipata kwa sokombino where are they today? Rwanda sio mfano ni takataka.
 
Tuna rais dhaifu ambaye hajui hata dynamics za uchumi. Tuna gavana wa bank bogus ambaye ameshindwa hata kudhibiti mfumko wa gharama za maisha, unategemea nini? Tutakuwa tunawasikiliza tu wenzetu wakipaa sisi gesi tukimkabidhi Mchina kama vile dhahabu tulivyowakabidhi wazungu.
 
Hivi Rwanda si ni kama Ilala tu???
I wish at least kila mkoa wa Tanzania ungekuwa kama Rwanda
 
-------- mkubwa wewe swali gani hilo? Ukuaji wa uchumi wa rwanda si endelevu kwasababu hautegemei nguvukazi ya wanyarwanda bali mali asili zinazoporwa kutoka drc, vta ya kongo ikikoma hata panadol mtakuwa mnakopa .

Mkuu sisi za kwetu tunaenda kuwatafuta wanaume waje kuzichukua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…