Kwanini Rwanda wametuzidi katika hili?


Ndugu yangu asante sana kwa hili. Mimi nimeitwa mamluki kwenye mtandao mmoja kwa sababu ya msimamo wangu na pia nikaulizwa mbona nimekuwa mkali naikandia nchi yangu sioni chochote kizuri kinachofanyika? Afadhali niitwe majina lakini siwezi kukaa kimya wakati naona nchi yangu inakwenda mrama. Kuna Wamarekani waliitwa wasaliti kwa kupinga vita ya Vietnam, lakini leo historia imewaonyesha kuwa walikuwa wazalendo kweli kweli. Ile vita ilikuwa ya maafa makubwa kwa taifa la Marekani. Vivyo hivyo leo kumsifia Kikwete wakati anaipeleka nchi kusikojulikana si uzalendo hata kidogo. Miaka minane sasa mamlakani alituahidi tatizo la umeme litakuwa historia kufikia Desemba 2007. Sote tunajua mgao wa umeme unaendelea kama kawa. Alituahidi atafanya mabadiliko kwenye mikataba ya madini ili kuwepo win win situation. Bado tuko kwenye win lose situation sisi tukiwa losers. Hapana, nitakubali kuitwa majina ya kila aina lakini hakuna mtu mwenye haki ya kuhoji uzalendo wangu. Asante sana kwa mchango wako ambao umeniongezea ari.
 
Uchumi utakuwaje wakat % kubwa ya fungu la bajeti linatengwa kwa matumiz binafsi na sio kwa maendeleo? Pia hata linalotengwa kwa maendeleo huwa no return hapo uchumi utakuwa kwel
 
Uchumi gani unaosema na wewe mbulula nyie warwanda wa ajabu sana mnaiba madini congo bila ushuru halafu leo mseme uchumi unakua kwenda zako na lwanda yako.
Unatokwa povu tu na uzushi wenu, lini uliona wanaiba madini, mtazusha wenzenu wanasonga mbele. Nyinyi c mmeridhika na biashara ya sembe
 

Wizi wa dhahabu za DRCG
 
Unatokwa povu tu na uzushi wenu, lini uliona wanaiba madini, mtazusha wenzenu wanasonga mbele. Nyinyi c mmeridhika na biashara ya sembe
wewe lazima Utakuwa Mhamiaji Haramu huwezi ukamtetea kagame kiwango hiki!

Huu si Uzushi ni Ukweli na Dunia nzima wanajua Rwanda ni Mwizi number one wa Rasilimali za Congo akifuatiwa na ndugu yake Uganda na Mali ya Congo Ndio imemwinua kiuchumi Kagame na Serikari yake huku fedha nyingi ikitumika kuligharamia Jeshi lake kubwa na waasi wa m23 ambao Ndio wanalinda masilahi ya Rwanda Congo Ndio Maana Kagame sasa anamchukia Rais JK kisa amepeleka Jeshi Congo kuharibu vyanzo vyake vya mapato haramu hizi choko choko zote chanzo ni masilahi ya kagame Rwanda kuguswa kwani Kagame anahofia atafulia pindi akitolewa Congo na itamwia vigumu kuligharamia Jeshi lake Matokeo yake ni Uasi mkubwa kwani Njaa ikipiga hodi Jeshini lazima Majanga yajongee kwa kasi sana .hizi takwimu za kukua kwa Uchumi wa Rwanda zitakuwa aibu siku M23 waking'oka Congo kisha Hakuna njia ya kupora Mali huku wimbi la wahamiaji Haramu Kama wewe mkiendelea kurejeshwa Rwanda.
 
Wahamiaji Haramu wengi wapo Dsm huku wakiwa waumini wakubwa wa JF wakiwa na Lengo la kutumia nguvu kubwa kuutetea uporaji wa Mali za Congo na Nchi jirani kwa namna fulani Mfano harisi na Tanzania imeadhilika sana na Uhamiaji Haramu na Ukimbizi kwani uharibifu wa mazingira uliosababishwa na uhamiaji haramu hauna mfano Wizi ujambazi na uwingizaji wa siraha huko mipakani ni athali za Uhamiaji haramu Hivyo Uchumi wa Tz umemegwa na Hawa kwa staili ya ajabu kwani Tz imejikuta ipo busy kutatua matatizo yanayosababishwa na hao jirani kwa Gharama kubwa pasipo kujijua !ebu jiulize Leo Kama hz pesa zingelielekezwa kwenye maendeleo tungekuwa wapi?Nchi za Ulaya wao hawataki Uhamiaji Haramu na wanajua athali zake kiuchumi Hivyo Tz tujifunze mbinu za kisasa za kupambana na uhamiaji haramu unapora Mali na kuzinufaisha nchi zao kisha Takwimu za Uchumi kusifia Nchi eti zimekuwa kiuchumi wakati zinayumbisha Nchi zingine kiuchumi kwa faida yao .
 

subiri, kichapo wanachopata M23 kitaporomosha kabisa uchumi wa nchi hiyo. kwanza uchumi wa nchi nzima ya Rwanda haulingani hata chembe na uchumi wa Dar pekee
 
-------- mkubwa wewe swali gani hilo? Ukuaji wa uchumi wa rwanda si endelevu kwasababu hautegemei nguvukazi ya wanyarwanda bali mali asili zinazoporwa kutoka drc, vta ya kongo ikikoma hata panadol mtakuwa mnakopa .

hapa kung ukweli ...
 

Mkuu, wahamiaji haramu wako wengi sana humu jf. kagame anatumia fedha nyingi kuimarisha kitengo cha propaganda nje ya nchi yake. inasadikika kuwa hata ndugu zetu wa CHADEMA ni miongoni mwa wanufaika wa ufadhili huo.
 
-------- mkubwa wewe swali gani hilo? Ukuaji wa uchumi wa rwanda si endelevu kwasababu hautegemei nguvukazi ya wanyarwanda bali mali asili zinazoporwa kutoka drc, vta ya kongo ikikoma hata panadol mtakuwa mnakopa .

Labda sisi tusiweke nia ya kwenda kupora rasilimali za nchi nyingine kama DRC, lakini mbona kila mkoa Tanzania una rasilimali nyingi na hazinufaishi Tanzania wala mkoa husika

Mfano, Shinyanga licha ya kuwa wanalima mpunga na pamba amapo pamba ni zao la biashara na mchele zao la chakula na biashara, pia kuna madini ya dhahabu na almasi

Shinyanga ina migodi 3 na tupo mbioni kuweka wa 4, maisha ya watanzania kule ni ya kusikitisha na wengi ni maskini na mafukara

Je? Kwa muktadha huo wa kwako sisi tunaibiwa na nani na kwa nini anatuibia na kwa nini hatuchukui hatua ili badala ya kwenda kuiba nchi jirani, tujinufaishe kwa urithi wetu tuliopewa na Muumba?
 

watakuita mnyarwanda.....wana akili hao?wanachotaka ni kuona vita
 
subiri, kichapo wanachopata M23 kitaporomosha kabisa uchumi wa nchi hiyo. kwanza uchumi wa nchi nzima ya Rwanda haulingani hata chembe na uchumi wa Dar pekee

hahahahahaa...wabongo zile nyasi tulizoahidiwa na mramba ndo wakati wa kuzila ucha ushabiki wa vita kaka....
 
Mimi ni mtanzania halisi, tatizo lenu wauza unga hampendi kuambiwa ukweli, usifiche mshumaa chini ya uvungu wa kitanda ulete giza utaunguza kitanda na nyumba. Kagame anapiga kazi nchi yake inapiga hatua, nyinyi kupiga domo tu eti anaiba Kongo. Endeleeni kusafiri na mihadarati yetu muimarishe chama wenzenu wanafana mambo ya maendeleo.

Tuleteeni ushahidi acheni kuongozwa na mihemko na chuki zenu kwa Kagame
 
subiri, kichapo wanachopata M23 kitaporomosha kabisa uchumi wa nchi hiyo. kwanza uchumi wa nchi nzima ya Rwanda haulingani hata chembe na uchumi wa Dar pekee

Wazee wa propaganda m23, kwa sasa sioni post zao kwenye facebook.
 
Aisee una akili wewe! sijawahi ona, ni kweli rwanda pamoja na kujisifia na kupiga propaganda kwamba uchumi wao unakua lakini sio endelevu. Hawana rasilimali, hawana viwanda, hawana ardhi ya kutosha kulima na kuzalisha mazao ya chakula na biashara duh nisitaje mengi kifupi wana majanga mengi, watupigie magoti tu sisi baba zao TZ, ila tusiwapokee mpaka kagame atokeee!!

-------- mkubwa wewe swali gani hilo? Ukuaji wa uchumi wa rwanda si endelevu kwasababu hautegemei nguvukazi ya wanyarwanda bali mali asili zinazoporwa kutoka drc, vta ya kongo ikikoma hata panadol mtakuwa mnakopa .
 
-------- mkubwa wewe swali gani hilo? Ukuaji wa uchumi wa rwanda si endelevu kwasababu hautegemei nguvukazi ya wanyarwanda bali mali asili zinazoporwa kutoka drc, vta ya kongo ikikoma hata panadol mtakuwa mnakopa .

Muongo wewe, hakuna ubishi kuwa Kagame amedhibiti ufisadi Rwanda na matumizi mabaya ya rasilimali za umma, fuatilia hata magari wanayotumia viongozi wa Rwanda,
Kama uchumi wa Rwanda unakua kutokana na rasilimali zinazibwa DRC, je Tz yenye rasilimali nyingi na haina vita mbona imeshindwa kupata maendeleo endelevu?
Ukweli ni kwamba wenzetu wako serious na maendeleo ya taifa lao, sisi Tumeacha mafisadi wakituibia na kujificha kwenye kivuli cha chama dola.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…