...jasusi.....ukifatilia huu uzi utadhihirisha ule usemi wa siku hizi kuwa...anaeonekana kuzungumzia madhaifu ya TZ ya leo anaonekana msaliti....ama si mzalendo.....ukweli huu unajidhirisha kwenye uzi huu kwa michango ya watu....na ndio sababu hata kupambana na mambo kama ufisadi...ama biashara chafu za unga inakua shida nchi hii...maana lazima watatoka wapuuzi wengi kutetea uchuro uliotufanya kufika hapa kama nchi....tena wanatetea kwa kigezo cha kipubavu...eti watu wanakosa uzalendo....hapa ndipo tumefika kama nchi....na inasikitisha unakuta hawa na graduates ambapo wanategemewa kesho waijenge TZ......
.....Tukija kwenye issue ya Rwanda na maendeleo yao ya haraka ukilinganisha na wengine(kama TZ)...hawa wanaosema kuwa Rwanda wanaendelea kwa kutumia raslimali wanazopora DRC...mbona hawajiulizi kwanini basi TZ isiendlee kwa raslimali tele ilizonazo???...ama nazo zinaporwa na Rwanda????.....ujinga huu wa kifikra.....
....Ukweli unabaki pale pale kuwa Rwanda wanaongozwa na kiongozi ambae anaongoza kwa ideology ya "self dependency ..as a country"...as opposed to mtawala wa TZ(JK)...ambaye anaendesha nchi kwa ideology ya "begging for survival".....huu ni ukweli mchungu....na ndio tofauti kubwa kati ya uongozi wa Rwanda na TZ.....
....In fact tofauti kwenye ideology za kiuongozi inaweza kuwa ndicho kikwazo kikubwa kinachofanya TZ ionekane kama inatengwa kwenye issue za EAC.....pamoja na kuwa watu wengi wamekazia kuwa yote yanatokana na ugomvi wa PG na JK...mimi naona ugomvi huu ni catalyst tu ya issue zilizojificha....ambazo(unfortunately)watu hawaziongelei......
...Pale ambapo PG na marais wengine karibu wote wa EAC wanapita na kuhuburi "self dependency as countries"....ni JK pekee kati ya wote ambae anapita dunia nzima bila aibu(tena openly)akihubiri "begging for survival as a country"....Huu ni ukweli usiofichika na ndio umeiweka TZ katika hali iliyopo.....na sioni kwanini usiifanye TZ kutengwa na wengine....pamoja na resources zilizopo.....Ni wajinga pekee watabeza maendeleo ya Rwanda...huku wakisahau uchuro uliopo TZ unaofanywa na watawala wao.....
.....Hata kule Zimbabwe kwa Mugabe...ambae JK na ccm yake wanamtumia kama role model.....yeye naye Mugabe ideology yake kiutawala pia ni "self dependency as a country"...na ndio imemfanya hata atengwe na nchi za magharibi....lakini utashangaa serikali ya ccm wanatoka kinafiki na kujifanya eti waumini wa sera za Mugabe.....wakati si kweli kimsingi......Tofauti kubwa ya PG na JK kiutawala ni kuwa mmoja ni "self dependent leader"....na mwingine ni "world begger"......huu ni ukweli mchungu kwa wajinga wengi TZ........
Ndugu yangu asante sana kwa hili. Mimi nimeitwa mamluki kwenye mtandao mmoja kwa sababu ya msimamo wangu na pia nikaulizwa mbona nimekuwa mkali naikandia nchi yangu sioni chochote kizuri kinachofanyika? Afadhali niitwe majina lakini siwezi kukaa kimya wakati naona nchi yangu inakwenda mrama. Kuna Wamarekani waliitwa wasaliti kwa kupinga vita ya Vietnam, lakini leo historia imewaonyesha kuwa walikuwa wazalendo kweli kweli. Ile vita ilikuwa ya maafa makubwa kwa taifa la Marekani. Vivyo hivyo leo kumsifia Kikwete wakati anaipeleka nchi kusikojulikana si uzalendo hata kidogo. Miaka minane sasa mamlakani alituahidi tatizo la umeme litakuwa historia kufikia Desemba 2007. Sote tunajua mgao wa umeme unaendelea kama kawa. Alituahidi atafanya mabadiliko kwenye mikataba ya madini ili kuwepo win win situation. Bado tuko kwenye win lose situation sisi tukiwa losers. Hapana, nitakubali kuitwa majina ya kila aina lakini hakuna mtu mwenye haki ya kuhoji uzalendo wangu. Asante sana kwa mchango wako ambao umeniongezea ari.