Weston Songoro
JF-Expert Member
- Feb 17, 2014
- 2,793
- 1,085
Bandugu, natumai kuwa hamjambo na mko vema baada ya kuadhimisha Sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo kwa hakika ilifana sana.
Wakati wa mapumziko ya weekend na Sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilisikika taarifa kuwa Kamati Kuu ya CCM ambayo inaketi leo Zanzibar katika kikao chake cha kawaida ina mpango wa kumfukuza uanachama kada maarufu wa chama hicho na ambaye anausaka urais kwa udi na uvumba huku akimwaga fedha nyingi, Edward Lowasa. Wengi tulifurahia kusikia taarifa hiyo kwa vile tunaamini kuwa LOWASA kupitia fedha anazomwaga kwa wajumbe wa Kamati Kuu na Mkutano mkuu wa CCM anaweza kusababisha chama kisimpendekeze mgombea mwenye sifa.
Huku wengi tukifurahia na tukikaa kitako kupokea kwa mikono miwili maamuzi hayo ya CCM ambapo inadaiwa kuwa Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ameandaa mashtaka mapya dhidi ya Lowasa, kuna wadau wawili wa habari ambao kwa hakika wamepokea kwa uchungu wa shubiri taarifa za kufukuzwa Lowasa. Wadau hao ni Saed Kubenea ambaye kwa sasa anaandikia gazeti la Mawio baada ya gazeti lake la Mwanaha.lisi kufungiwa kutokana na kukiuka misingi ya utoaji habari. Mwingine anayeweweseka sana ni Absalom Kibanda. Hakika wadau hawa wanaonekana kuchanganyikiwa sana na wanakerwa pale Lowasa anaposemwa kwa ubaya. Mie sijui ila kama kuna wadau wanajua sababu za msingi za waandishi hawa nguli kuchanganyikiwa naomba mtujuze ili na sisi tusioelewa tupate mwanga. Ninachokijua tu juu ya watu hawa ni kwamba hawajawahi kumwandika vibaya Lowasa.
Nawasilisha