Kwanini Saed Kubenea na Absalom Kibanda wanaweweseka baada ya taarifa ya kutimuliwa Lowassa CCM?

Wanamwandika Lowassa kwa sababu ndiye pekee atakayeipeleka inchi yetu kwenye matumaini. Mungu ibariki Tanganyika mungu mlinde Lowassa.
 
Shida ni kutafuta cheo cha Ukurugenzi wa Habari wa Rais kama Salva aliyepewa hadi na ofa ya mdogo mtu kuwa Mkuu wa Wilaya
 
Bandugu, natumai kuwa hamjambo na mko vema baada ya kuadhimisha Sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo kwa hakika ilifana sana.

Wakati wa mapumziko ya weekend na Sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilisikika taarifa kuwa Kamati Kuu ya CCM ambayo inaketi leo Zanzibar katika kikao chake cha kawaida ina mpango wa kumfukuza uanachama kada maarufu wa chama hicho na ambaye anausaka urais kwa udi na uvumba huku akimwaga fedha nyingi, Edward Lowasa. Wengi tulifurahia kusikia taarifa hiyo kwa vile tunaamini kuwa LOWASA kupitia fedha anazomwaga kwa wajumbe wa Kamati Kuu na Mkutano mkuu wa CCM anaweza kusababisha chama kisimpendekeze mgombea mwenye sifa.

Huku wengi tukifurahia na tukikaa kitako kupokea kwa mikono miwili maamuzi hayo ya CCM ambapo inadaiwa kuwa Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ameandaa mashtaka mapya dhidi ya Lowasa, kuna wadau wawili wa habari ambao kwa hakika wamepokea kwa uchungu wa shubiri taarifa za kufukuzwa Lowasa. Wadau hao ni Saed Kubenea ambaye kwa sasa anaandikia gazeti la Mawio baada ya gazeti lake la Mwanaha.lisi kufungiwa kutokana na kukiuka misingi ya utoaji habari. Mwingine anayeweweseka sana ni Absalom Kibanda. Hakika wadau hawa wanaonekana kuchanganyikiwa sana na wanakerwa pale Lowasa anaposemwa kwa ubaya. Mie sijui ila kama kuna wadau wanajua sababu za msingi za waandishi hawa nguli kuchanganyikiwa naomba mtujuze ili na sisi tusioelewa tupate mwanga. Ninachokijua tu juu ya watu hawa ni kwamba hawajawahi kumwandika vibaya Lowasa.

Nawasilisha

Katulie kwanza ndio ulete mada zenye uelewa kwa taarifa yako hakuna wa kumfukuza lowassa ndani ya ccm au nikuulize swali moja ntajie katka wote waliotangaza nia nani ambae amwagi ela.inaelekea jamaa anawaumiza kichwa sana
 
Attachments

  • 1421135779724.jpg
    1421135779724.jpg
    134.9 KB · Views: 367
Kwani fisadi lowasa ameshatimuliwa tayari? magamba yana kazi mwaka huu!
 
Kwa taarifa yako ni kwamba Saed Kubenea alipelekwa masomoni ng'ambo na gharama za masomo zote zimegharamiwa na Lowasa. Pia kanunuliwa gari na kujengewa nyumba. Aliahidiwa kuwa endapo Lowasa atakuwa Rais, atateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu.

Na Pasco unamuweka wapi?
 
Last edited by a moderator:
Kwa taarifa yako ni kwamba Saed Kubenea alipelekwa masomoni ng'ambo na gharama za masomo zote zimegharamiwa na Lowasa. Pia kanunuliwa gari na kujengewa nyumba. Aliahidiwa kuwa endapo Lowasa atakuwa Rais, atateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu.
usisahau uongo nao ni dhambi
 
Bandugu, natumai kuwa hamjambo na mko vema baada ya kuadhimisha Sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo kwa hakika ilifana sana.

Wakati wa mapumziko ya weekend na Sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilisikika taarifa kuwa Kamati Kuu ya CCM ambayo inaketi leo Zanzibar katika kikao chake cha kawaida ina mpango wa kumfukuza uanachama kada maarufu wa chama hicho na ambaye anausaka urais kwa udi na uvumba huku akimwaga fedha nyingi, Edward Lowasa. Wengi tulifurahia kusikia taarifa hiyo kwa vile tunaamini kuwa LOWASA kupitia fedha anazomwaga kwa wajumbe wa Kamati Kuu na Mkutano mkuu wa CCM anaweza kusababisha chama kisimpendekeze mgombea mwenye sifa.

Huku wengi tukifurahia na tukikaa kitako kupokea kwa mikono miwili maamuzi hayo ya CCM ambapo inadaiwa kuwa Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ameandaa mashtaka mapya dhidi ya Lowasa, kuna wadau wawili wa habari ambao kwa hakika wamepokea kwa uchungu wa shubiri taarifa za kufukuzwa Lowasa. Wadau hao ni Saed Kubenea ambaye kwa sasa anaandikia gazeti la Mawio baada ya gazeti lake la Mwanaha.lisi kufungiwa kutokana na kukiuka misingi ya utoaji habari. Mwingine anayeweweseka sana ni Absalom Kibanda. Hakika wadau hawa wanaonekana kuchanganyikiwa sana na wanakerwa pale Lowasa anaposemwa kwa ubaya. Mie sijui ila kama kuna wadau wanajua sababu za msingi za waandishi hawa nguli kuchanganyikiwa naomba mtujuze ili na sisi tusioelewa tupate mwanga. Ninachokijua tu juu ya watu hawa ni kwamba hawajawahi kumwandika vibaya Lowasa.

Nawasilisha

Mkuu, kukata mkono wa mtu aliyekufa kwa kansa hakuwezi kurejesha uhai wa marehemu huyo; ccm ni marehemu tayari kumfukuza au kutomfukuza lowasa hakutaiponya ccm.

Kuhuisu Kubenea na Kibanda 'kuchukizwa' na tetesi za watu hao kufukuzwa CCM hiyo ni hoja ya umbeya wako tuu, fuatilia, soma kwa kina kisha fanya uchambuzi kabla ya kuamua kuhusu mwelekeo au maoni ya mwandishi badala ya kuleta jukwaani mambo ambayo huwezi kuyaelezea kwa kina au kuyafafanua.
 
Kwa upande wa Kubenea, naamini kabisa kutokana na msimamo wake, hadi gazeti lake pendwa na lililokuwa na ujasiri wa hali ya juu, kufichua ufisadi wa aina mbalimbali nchini, hadi gazeti lake, kupata kifungo cha maisha, ambapo ni rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na chombo chochote cha habari hapa TZ, siyo rahisi kwa huyo mtu kununuliwa.

Kwa maana hiyo inaonyesha waziwazi, mleta post, ameamua tu kumchafua kwa makusudi, mpanbanaji huyu shujaa Saed Kubenea.

Kwa upande wa Absolom Kibanda, Mhariri Mtendaji mkuu wa New Habari Corporation, wanaochapisha magazeti ya Mtanzania na Rai, ambayo share holders wake wakuu ni Rostam Aziz na mzee wa mamvi.

Kwa hiyo kwa huyo Kibanda, kulazimika kutomwandika vibaya 'bosi' wake EL ni kwa huyo ndugu kutekeleza ile principle isemayo mtumikie kafiri upate mradi wako!
 
Hao ni paparazi wa UKAWA specific chadema, wanakifanya ni kwamba kila mgogoro unaotokea ndan ccm wao wana-u-pressurize(chochea) ili ccm kigawanyike na badae wakuu wao wachukue nchi haopo october 2015

Tafadhali usiusishe Chadema kama huna uwakika
 
Walau tupate signs za hao watu kuchanganyikiwa. Umewakuta uchi? Wanaogea peke yao? Wako hospital. Swali jingine...........wale waandishi wa Uhuru na Daily news kutomuandika vibaya JK nao wamechanganyikiwa?
Big umemaliza kabisa!! big up for such logical argument
 
Kibanda aliahidi kwamba anamalizia kuandika kitabu chake kuhusu ubovu wa Samwel Sitta miaka mitatu sasa kimya.
 
kubenea na lowasa ni paka na panya hakuna mtu amewahi kumchafua lowasa ama kumuandika vibaya lowasa kama said kubenea
 
Mwaka 1995 kulikuwa na mchujo wa uraisi vijana walikuwa kikwete, mkapa, lowassa
Wazee walikuwa warioba, boman, malecela

Kwa group la kwanza kabaki lowassa hapo hvyo msilie sana
 
Bandugu, natumai kuwa hamjambo na mko vema baada ya kuadhimisha Sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo kwa hakika ilifana sana.

Wakati wa mapumziko ya weekend na Sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilisikika taarifa kuwa Kamati Kuu ya CCM ambayo inaketi leo Zanzibar katika kikao chake cha kawaida ina mpango wa kumfukuza uanachama kada maarufu wa chama hicho na ambaye anausaka urais kwa udi na uvumba huku akimwaga fedha nyingi, Edward Lowasa. Wengi tulifurahia kusikia taarifa hiyo kwa vile tunaamini kuwa LOWASA kupitia fedha anazomwaga kwa wajumbe wa Kamati Kuu na Mkutano mkuu wa CCM anaweza kusababisha chama kisimpendekeze mgombea mwenye sifa.

Huku wengi tukifurahia na tukikaa kitako kupokea kwa mikono miwili maamuzi hayo ya CCM ambapo inadaiwa kuwa Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ameandaa mashtaka mapya dhidi ya Lowasa, kuna wadau wawili wa habari ambao kwa hakika wamepokea kwa uchungu wa shubiri taarifa za kufukuzwa Lowasa. Wadau hao ni Saed Kubenea ambaye kwa sasa anaandikia gazeti la Mawio baada ya gazeti lake la Mwanaha.lisi kufungiwa kutokana na kukiuka misingi ya utoaji habari. Mwingine anayeweweseka sana ni Absalom Kibanda. Hakika wadau hawa wanaonekana kuchanganyikiwa sana na wanakerwa pale Lowasa anaposemwa kwa ubaya. Mie sijui ila kama kuna wadau wanajua sababu za msingi za waandishi hawa nguli kuchanganyikiwa naomba mtujuze ili na sisi tusioelewa tupate mwanga. Ninachokijua tu juu ya watu hawa ni kwamba hawajawahi kumwandika vibaya Lowasa.

Nawasilisha

Daydreaming!
 
Back
Top Bottom