Kwanini Saed Kubenea na Absalom Kibanda wanaweweseka baada ya taarifa ya kutimuliwa Lowassa CCM?

Kwanini Saed Kubenea na Absalom Kibanda wanaweweseka baada ya taarifa ya kutimuliwa Lowassa CCM?

CCM WAMFUKUZE lOWASA AU WAMWACHE BADO MACHUNGU NI YALE YALE .
SASA HIVI CCM WAMEBANWA KWENYE CRITICAL ANGLE .

CCM HAITAFIKA MARCH MWAKA HUU
Tuliambiwa toka 2010 nchi haitatawalika,maandamano yalifanyika nchi nzima.Mijamaa bado inapeta tu.kupambana na CCM kunahitaji akili na si maneno ya mitandaoni
 
Kwa taarifa yako ni kwamba Saed Kubenea alipelekwa masomoni ng'ambo na gharama za masomo zote zimegharamiwa na Lowasa. Pia kanunuliwa gari na kujengewa nyumba. Aliahidiwa kuwa endapo Lowasa atakuwa Rais, atateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu.

Unamfahamu aliesuka mpango wa kujeruhiwa na tindikali ndgu Kubenea???je wajua chanzo cha kuvamiwa kubenea ni issue ya Richmond???
 
Bandugu, natumai kuwa hamjambo na mko vema baada ya kuadhimisha Sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo kwa hakika ilifana sana.

Wakati wa mapumziko ya weekend na Sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilisikika taarifa kuwa Kamati Kuu ya CCM ambayo inaketi leo Zanzibar katika kikao chake cha kawaida ina mpango wa kumfukuza uanachama kada maarufu wa chama hicho na ambaye anausaka urais kwa udi na uvumba huku akimwaga fedha nyingi, Edward Lowasa. Wengi tulifurahia kusikia taarifa hiyo kwa vile tunaamini kuwa LOWASA kupitia fedha anazomwaga kwa wajumbe wa Kamati Kuu na Mkutano mkuu wa CCM anaweza kusababisha chama kisimpendekeze mgombea mwenye sifa.

Huku wengi tukifurahia na tukikaa kitako kupokea kwa mikono miwili maamuzi hayo ya CCM ambapo inadaiwa kuwa Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana ameandaa mashtaka mapya dhidi ya Lowasa, kuna wadau wawili wa habari ambao kwa hakika wamepokea kwa uchungu wa shubiri taarifa za kufukuzwa Lowasa. Wadau hao ni Saed Kubenea ambaye kwa sasa anaandikia gazeti la Mawio baada ya gazeti lake la Mwanaha.lisi kufungiwa kutokana na kukiuka misingi ya utoaji habari. Mwingine anayeweweseka sana ni Absalom Kibanda. Hakika wadau hawa wanaonekana kuchanganyikiwa sana na wanakerwa pale Lowasa anaposemwa kwa ubaya. Mie sijui ila kama kuna wadau wanajua sababu za msingi za waandishi hawa nguli kuchanganyikiwa naomba mtujuze ili na sisi tusioelewa tupate mwanga. Ninachokijua tu juu ya watu hawa ni kwamba hawajawahi kumwandika vibaya Lowasa.

Nawasilisha

Mkuu Muganyizi kakuuliza swali, uonyeshe hizo dalili za kuchanganyikiwa, ulicho jibu ni kuwa kuna tofauti kati ya kuweweseka na kuchanganyikiwa, ukiwa umesahau kuwa kwenye uzi wako umetumia neno kuchanganyikiwa. Mkuu tatizo si lowasa tatizo ni ccm, inabidi chama kijitathmini, kwani kwa sasa kimebeba uozo na kinanuka, hatua muhimu ni chama kijisafishe kwa dhati kwa kuondoa mafisadi wote.
 
Raisi wa mwaka huu ni EDWARD LOWASSA lakini eti CCM wamepanga raisi awe DK. SHEIN Kule visiwani aachiwee MTOTO WA MWINYI KUWA RAISI
 
lowasa anawatesa sana aisee, naona mmemtuma na mtabiri anene yake. tusubiri.
 
Kwa taarifa yako ni kwamba Saed Kubenea alipelekwa masomoni ng'ambo na gharama za masomo zote zimegharamiwa na Lowasa. Pia kanunuliwa gari na kujengewa nyumba. Aliahidiwa kuwa endapo Lowasa atakuwa Rais, atateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu.

Oooohh ssshhh so hot news from Hot Lady... Ooyeees!!!
 
Awo wa naomfukuza Lowasa hebu watuambie wao wanausafi gani kwennye uongozi n chama chao cha CCM?
 
Unamfahamu aliesuka mpango wa kujeruhiwa na tindikali ndgu Kubenea???je wajua chanzo cha kuvamiwa kubenea ni issue ya Richmond???
Mwache huyo hot" aendelee kuwashwa!! Lowasa ni adui mkubwa wa kubenea hata tindikali ulikuwa msuko wa EL.
 
Kwa taarifa yako ni kwamba Saed Kubenea alipelekwa masomoni ng'ambo na gharama za masomo zote zimegharamiwa na Lowasa. Pia kanunuliwa gari na kujengewa nyumba. Aliahidiwa kuwa endapo Lowasa atakuwa Rais, atateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu.

Huu uongo mnaotunga utawapeleka Kaburini Manina zenu
 
Upinzani wanahaha sana Lowassa atimuliwe ili wao wapate mteremko uchaguzi october since wanajua jamaa akipita shughuli ni pevu

Chochoro wa upinzani upo kwa Lowasa. Akiteuliwa yeye na CCM upinzani utashangilia. Hakuna mwenye fedha ya kununua watazania milioni 10. Anaweza kuwahonga wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM lakini si wananchi wote. Uchochoro wa UPINZANI kushinda ni kwa CCM kumteua Lowasa. CCM ikimteua mtu kama Dr. Harison Mwakyembe, au Mzee Salim Ahamed Salim, Au Mzee Sinde Warioba au hata Prof Issa Shivji, upinzani utapata shida sana.
 
Back
Top Bottom