Kwanini samaki wa baharini hawafiki mikoani?

Kanda ya Ziwa pia kuna aina nyng za samak kuna ningu, nembe ila wanaishia huko huko kwann sangara na sato?
Mm nafikir kwasababu ya ladha na kuwa na kuwa na nyama nyngi

Nimeelewa hoja yako, sio samaki wote wa ziwani husambaa nchi nzima.

Ningu, gogogo, nembe, mbete hawaendi mjini.
 
Hata hapa Dar mtaani bado kuna Sato na Sangara tu..
 
Mkuu tatizo ni hawa wavuvi wa kienyeji wanavua samaki wachache kuweza kutosheleza hata soko la dar. Ukitaka kujua hii nchi yetu ina uongozi wa hovyo wewe fikiria eneo kubwa la bahari tulilo nalo, miaka zaidi ya 60 bado hatuna makampuni ya uvuvi yanayomilikiwa either na wakala wa serikali au watu binafsi. Miaka yote serikali ina wakala wa uvuvi, lakini hawana meli za kwenda kuvua bahari kuu, hivi unaweza kusema nchi kama hiyo haijalaaniwa kweli? zingatia asilimia kubwa ya watoto wana matatizo ya utapiamlo, lakini tuna kila aina ya vyakula kuanzia samaki, nyama, nk. ambavyo vina protini nyingi sana, nafikiri aliyeturoga alikwisha kufa.................
 
Sangara siyo origin mwanza maana walipandikizwa
 
Upo mkoa gani? Dodoma tunazo na tunanunua kilo 9000 inategemea na Aina ya samaki ushindwe wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…