Niko nafwatilia speech za viongozi wa afrika huko UN lakini mpaka sasa sijaona jina la rais wetu Samia. Je nini tatizo?
NB: Mara ya mwisho nilimuona juzi akiwa jukwaani huko mtwara na akina Harmonize.
Anatapanya pesa kulipa wasanii badala kuwaza vyanzo vipya vya umeme.
Nchi hii imelogwa, alisema Magufuli.
Magufuli asingevumilia taabu hii ya umeme, mnyonge anyongwe lkn haki yake asinyang'anywe.
Tumerudi enzi za Kikwete...giza, rushwa na kutokuwajibika.
Kikwete anaenda UN kama nani?
UN ndiko marais hutafuta fursa kwa ajili ya nchi, marais wanakutana kirahisi na kubadilishana fursa za kiuchumi za watu wao.
Samia bibi, mama na dada yetu anatuangusha sana.
Hajui kuweka vitu vya kwanza, kwanza.
Ziara ya Kusini sio mbaya lakini ingeweza kusubiri arudi UN kwani ratiba yake ilijulikana mapema.
Nasemaje? Kama nchi tunapishana na muda, wengine wanaenda mbele, sisi Tz tunarudi nyuma kwa speed.
Nchi haina umeme.
Welders hawana kaxi
Vinyozi na wasusi hawana kazi
Watumia umeme kiuchumi wanalia....NANI ANAJALI?