Zirconium
Senior Member
- Feb 1, 2025
- 196
- 254
Tujifunze kidogo kuhusu hili
Maumivu au kufa ganzi meno kwasababu ya sauti ya mkwaruzo wa vitu (Sound Induced Dental Sensitivity) ni tatizo ambalo limekuwa likiwapata baadhi ya watu inapotokea mtu mwingine amesugua vitu viwili ambavyo hutoa sauti yenye mgandamizo mkubwa wa kimawimbi ambayo sauti hiyo huingia kwenye Meno na kumletea mtu maumivu au ganzi ya ghafla kwenye meno na mwili kusisimka.
Hali hii hutokea wakati gamba gumu la nje la jino (Enamel) inapokuwa limechakaa, mizizi wa jino kuwa wazi baada ya fizi kukimbia, au jino kuwa na tundu, jambo linalofanya mishipa ya jino na mirija ya tabaka la ndani (dentinal tubules) ya jino yenye maji kuguswa na mtikisiko wa sauti hizo hivyo kushindwa kuhimili na moja kwa Moja Ubongo kutoa tafsiri ya haraka ya Maumivi au Ganzi kwenye Meno husika.
Sauti za Mikwaruzo ya vitu inayoleta maumivu au ganzi za meno:
1. Mkwaruzo wa chaki kwenye ubao wa kuandikia
2. Msuguano wa kasha la ndani laini jeupe la kuhifadhia redio, runinga (Television) jokofu n.k. Yachukue maksha hayo shika mkono wa kulia na kushoto yasugue yenyewe pamoja
3. Msuguano wa kitu cha chuma na marumaru (tiles)
4. Msuguano wa msumari na bati kama unalikwangua bati
5. Ukikaa Karibu na mtu mwenye tatizo la kusaga meno (bruxism/tooth grinding) yake bila kujijua
6. Kusugua mchanga kwenye sakafu ya saruji au marumaru
Athari hii huwapata watu ambao wanakuwa na vitu hatarishi vifuatavyo:
1. Kusagika kwa gamba gumu la nje la jino (Enamel) hivyo kuacha tabaka la ndani (dentine) wazi
2. Fizi kushuka na kufichua wazi sehemu ya chini ya jino.
3. Kuharibika kwa kiini cha jino
4. Mpasuko kwenye jino
5. Kama mtu anachangamoto ya afya ya akili iitwayo Misophonia ambapo mtu huyo hukerwa mara kwa mara na suati nyembamba kama za kutafuna,kugonga kitu na kupumua humfanya kukereka na zinamletea msongo wa Mawazo (stress).
Kwa Changamoto za Kinywa na meno usisite Kufika Offisini kwetu kwa mawaslino 0658950085