Kwanini Serekali inakopa kama inaweza ku-print noti mpya

Kwanini Serekali inakopa kama inaweza ku-print noti mpya

Daah haya ngoja niweke neno. Kusema serikali haichapishi pesa si kweli, serikali huwa inachapisha pesa kama njia moja wapo ya kuwakopa wananchi wake (pesa kama pesa yenyewe ni worthless kama haiwi backed by goods na services zinazozalishwa au zilizopo)

Yaani serikali inapokosa fedha lets say ya mishahara, basi inaweza ikachapisha kiasi (limited amount) ili kulipa hiyo mishahara, ila hii inabidi ifanyike kwa kiasi kidogo sana ili kuepusha kushuka kwa thamani ya pesa (over inflation) ambapo utakuta mkate unapanda toka 1,000/= hadi 10,000/= pengine,

Hivyo pesa inaweza ikakosa thamani katika manunuzi na ikawa sawa na toilet paper tu. Sasa njia nyingine ya kukopa ndio hiyo ya mabenki ya kibiashara, mikopo toka mataifa rafiki na mashirika ya maendeleo kwa masharti/ riba maalum.

Na ukitaka kuamini serikali huwa inawakopa wananchi wake kwa kuchapisha pesa jiulize kwanini soda ilikuwa inauzwa 150/= ila leo inauzwa 500/=, means imewakopa wananchi na haijawalipa bado, otherwise soda ilipaswa iuzwe bei ile ile ya 150/=
 
kamq umeongea kweli nimekuelewa sana. sasa vipi kwa nchi zenye mitambo ya kuprint pesa, inathibitiwa vipi kuwa haitumiinjia za panya kuprint zao kimya kimya

ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹
Hiyo inaweza kuwork kwa nchi yenye dominant currency labda, yaani USA maana kila mtu huitumia
 
Asanteni wachache mliojaribu kumjibu, swali zuri la uelewa ila anajibiwa kihuni.
Kuchapisha pesa noti kuhudumia mkopo au baadhi ya shughuli kuna sababisha matatizo mengi kuliko suluhisho.

Ujerumani ikijiita Weimar republic waliprint noti nyingi mwaka 1922 kilichotokea ni mfumuko wa bei uliopitiliza(hyper inflation)

Ujerumani ilikuwa na deni kubwa baada ya kushindwa vita vya kwanza vya dunia, njia waliyotumia ni hii ya kuchapisha noti nyingi.

Pesa ikawa nyingi kwenye mzunguko kuliko kile ambacho nchi inaweza kuzalisha.

Mfumuko wa bei ukaibuka na kusababisha thamani ya tharafu yao kushuka thamani, na matokeo yake kushindwa kulipa deni kabisa.

Ukiangalia huo mfano unaweza kuona madhara ya kuchapisha noti nyingi.

Kikawaida kiwango cha noti kinachotolewa kinatakiwa kiendane na level ya uzalishaji wa bidhaa na huduma.

Ili kuelewa zaidi tuchukulie mfano wa muonyesha banda la video.

Uwezo wa banda la video ni kuingiza watu hamsini.

Kwa hiyo mwenye banda la video(mtengeneza noti) atatengeneza tiketi(noti) 50 kila tiketi iwe sh 2.

Kama mwenye banda la video akawa ana uhitaji sh 108, akaamua azalishe 54 kinachofuata hizi tiketi zitapanda bei kwa sababu siti ziko hamsini tu.

Sasa kama kuna mtu mwingine naye anaonyesha video wateja wanaweza kuhamia huko kwa sababu bei ni ya chini. Huyu mwingine atashindwa hata kuipata hiyo 108.

Kwa hiyo hapo njia nzuri ni kuwakopa wale baadhi walionunua tiketi 50, kwa sababu kuna wengine hawatoangalia movie wakati huo kwa hiyo utazikopa zile tiketi mfano 4 (mfano saving au kuuza dhamana za serikali,bond nk) na kuziuza kwa wengine ama kuzifanyia shughuri nyingine.

Ndio maana serikali inapokuwa na uhitaji wa kiasi cha pesa cha ziada na kodi ikawa haitoshi, hukopa kwa kwa kuuza treasury bill, treasury bonds nk au kukopa nje ya nchi kuliko kuchapisha noti mpya kwa sababu uchapishaji wa noti mpya haiongezi uzalishaji bali inaongeza pesa kwenye mzunguko.

Nadhani wenye uelewa zaidi watakufafanulia.

Baadhi ya link unazoweza pitia.
https://en.wikipedia.org/wiki/National_debt_of_the_United_States
Why do governments borrow money instead of printing it? - Quora
Hyperinflation in the Weimar Republic - Wikipedia
The problem with printing money - Economics Help
 
Daah haya ngoja niweke neno. Kusema serikali haichapishi pesa si kweli, serikali huwa inachapisha pesa kama njia moja wapo ya kuwakopa wananchi wake (pesa kama pesa yenyewe ni worthless kama haiwi backed by goods na services zinazozalishwa au zilizopo), yaani serikali inapokosa fedha lets say ya mishahara, basi inaweza ikachapisha kiasi (limited amount) ili kulipa hiyo mishahara, ila hii inabidi ifanyike kwa kiasi kidogo sana ili kuepusha kushuka kwa thamani ya pesa (over inflation) ambapo utakuta mkate unapanda toka 1,000/= hadi 10,000/= pengine, hivyo pesa inaweza ikakosa thamani katika manunuzi na ikawa sawa na toilet paper tu. Sasa njia nyingine ya kukopa ndio hiyo ya mabenki ya kibiashara, mikopo toka mataifa rafiki na mashirika ya maendeleo kwa masharti/ riba maalum. Na ukitaka kuamini serikali huwa inawakopa wananchi wake kwa kuchapisha pesa jiulize kwanini soda ilikuwa inauzwa 150/= ila leo inauzwa 500/=, means imewakopa wananchi na haijawalipa bado, otherwise soda ilipaswa iuzwe bei ile ile ya 150/=
Kitu ulichoongea hapa ni farsafa kwa mtu mwenye uwelewa wa karibu hawezi kuelewa kabisaaaaa nahisi kama unaitaji kufafanua zaid

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa jibu simple ni kuwa
Kama serikali ikiprint hela nyingi na hizi hela zikawekwa kwenye mzunguko basi kuna madhara kadhaa yataukumba uchumi kwa ujumla na uchumi wa mtu mmoja mmoja.
1. Production itaathirika; kila mtu si ana hela bwana nani akajichoshe kufanya kazi
2. Kutokana na saba bu hiyo hapo juu itapelekea supply ya bidhaa sokoni kupungua sana hivyo bei ya bidhaa itapanda maradufu kwasababu demand itakuwa ni kubwa kuliko supply
3. Kutokana na sababu hiyo hapo juu itapelekea kuwa na inflation kubwa sana, hela unayo lakini aikidhi kununua ha mchele kilo moja.
4. Tutegemee mabenki mengi kufilisika; mabenki mengi yanategemea zaidi kutoa loans ili yaweze kujiendesha, nani akakope wakati kila mtu ana hela mtaani.
5. Asset, bonds na stock kupoteza thamani yake; mfano nyumba iliyokuwa inauzwa million 50 kukikwa na hela nyingi mtaani hii nyumba itakuwa inauzwa million 100 wakati hiyo siyo thamani yake halisi.
Hizo ni athari chache sana kati ya nyingine nyingi
Serikali ikikopa maana yake lazima italipa hiyo hela, so hela ya kulipa itatoka kwenye hela ambazo zipo kwenye mzunguko sema itakuwa imeacha faida kidogo kwenye uchumi
 
Kwa hili nimekupata, ila tatizo hujagusia upande wa kukopa, yaani umeongelea madhara ya kuprint tu.Tupe na faida za kukopa tupime mzani
 
Mwelekeze kama unajua maswala yakukumbuka hata professor alichofundisha mwaka wa 1 wa degree yake hakumbuki. Concept kama unaoua tukumbushe wote kwa faida ya wengine..

Mkuu ina maana hata economics ya form 1 and 2 ilikupita.. Jaribu bas hata kugoogle topic ya supply and demand kuna kitu utajifunza
 
Kwa jibu simple ni kuwa
Kama serikali ikiprint hela nyingi na hizi hela zikawekwa kwenye mzunguko basi kuna madhara kadhaa yataukumba uchumi kwa ujumla na uchumi wa mtu mmoja mmoja.
1. Production itaathirika; kila mtu si ana hela bwana nani akajichoshe kufanya kazi
2. Kutokana na saba bu hiyo hapo juu itapelekea supply ya bidhaa sokoni kupungua sana hivyo bei ya bidhaa itapanda maradufu kwasababu demand itakuwa ni kubwa kuliko supply
3. Kutokana na sababu hiyo hapo juu itapelekea kuwa na inflation kubwa sana, hela unayo lakini aikidhi kununua ha mchele kilo moja.
4. Tutegemee mabenki mengi kufilisika; mabenki mengi yanategemea zaidi kutoa loans ili yaweze kujiendesha, nani akakope wakati kila mtu ana hela mtaani.
5. Asset, bonds na stock kupoteza thamani yake; mfano nyumba iliyokuwa inauzwa million 50 kukikwa na hela nyingi mtaani hii nyumba itakuwa inauzwa million 100 wakati hiyo siyo thamani yake halisi.
Hizo ni athari chache sana kati ya nyingine nyingi
Serikali ikikopa maana yake lazima italipa hiyo hela, so hela ya kulipa itatoka kwenye hela ambazo zipo kwenye mzunguko sema itakuwa imeacha faida kidogo kwenye uchumi
Mbona swali lilikuwa wazi sana, je inaprint hela kama mbadala wa kukopa pesa au huwa haiprint? Jaribu kujikita kwenye swali
 
Kuna kiongozi wa nchi aliamka zake akasema watu wanalia maisha magum hamna pesa, wakaagiza pesa kibao ziwe printed zikaletwa nchini duh ikaharibu uchumi wao completely, kwenye principles of money mojawapo ni it should be scarce, yani pesa isiwe nyingi kwenye mzunguko maana ukiprint mihela mingi currency yako itashuka thamani ndio ka zimbabwe unaenda nunua mkate na bunda la pesa.. it's a very huge aspect this is the real world vitu haviwi solved kirahisi hivyo kijana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna waziri sijui wa zambia au Zimbabwe, aliamka zake akasema watu wanalia maisha magum hamna pesa, wakaagiza pesa kibao ziwe printed zikaletwa nchini duh ikaharibu uchumi wao completely, kwenye principles of money mojawapo ni it should be scarce, yani pesa isiwe nyingi kwenye mzunguko maana ukiprint mihela mingi currency yako itashuka thamani ndio ka zimbabwe unaenda nunua mkate na bunda la pesa.. it's a very huge aspect this is the real world vitu haviwi solved kirahisi hivyo kijana

Sent using Jamii Forums mobile app

Hakuna waziri wa Zambia wala Zimbabwe aliyewahi kusema hivyo,so hio ni chai ya moto ila mengine uliyo yaandika yako sawa.
 
Kwa jibu simple ni kuwa
Kama serikali ikiprint hela nyingi na hizi hela zikawekwa kwenye mzunguko basi kuna madhara kadhaa yataukumba uchumi kwa ujumla na uchumi wa mtu mmoja mmoja.
1. Production itaathirika; kila mtu si ana hela bwana nani akajichoshe kufanya kazi
2. Kutokana na saba bu hiyo hapo juu itapelekea supply ya bidhaa sokoni kupungua sana hivyo bei ya bidhaa itapanda maradufu kwasababu demand itakuwa ni kubwa kuliko supply
3. Kutokana na sababu hiyo hapo juu itapelekea kuwa na inflation kubwa sana, hela unayo lakini aikidhi kununua ha mchele kilo moja.
4. Tutegemee mabenki mengi kufilisika; mabenki mengi yanategemea zaidi kutoa loans ili yaweze kujiendesha, nani akakope wakati kila mtu ana hela mtaani.
5. Asset, bonds na stock kupoteza thamani yake; mfano nyumba iliyokuwa inauzwa million 50 kukikwa na hela nyingi mtaani hii nyumba itakuwa inauzwa million 100 wakati hiyo siyo thamani yake halisi.
Hizo ni athari chache sana kati ya nyingine nyingi
Serikali ikikopa maana yake lazima italipa hiyo hela, so hela ya kulipa itatoka kwenye hela ambazo zipo kwenye mzunguko sema itakuwa imeacha faida kidogo kwenye uchumi
SWALI LA KIJINGA[emoji3]

Je pesa inakuwaje nyingi mtaani kama mshahara unaolipwa ni uleule, au hata ukifanya kibarua pesa unayolipwa ni ileile,?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom