Kwanini Serikali haiwajali wanafunzi Kama inavyowajali wafungwa?

Kwanini Serikali haiwajali wanafunzi Kama inavyowajali wafungwa?

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Ni jambo la kushangaza na kuumiza moyo kuona kuwa wafungwa walioko magerezani wanahakikishiwa huduma zote muhimu kama vile chakula, mavazi (mavazi ya gereza), malazi, huduma za afya na hata baadhi yao kupata fursa ya elimu.
images - 2025-07-01T214544.772.jpeg

Hili ni jambo jema kwa kuwa hata mfungwa anastahili haki zake za kibinadamu na huko ni sehemu ya yeye kujirekebisha tabia zake. Lakini swali linalozidi kuumiza ni hili: Je, kwa nini watoto wa shule za msingi za serikali hawapewi huduma za msingi kwa kiwango hicho hicho?
images - 2025-07-01T214622.930.jpeg

Watoto ni msingi wa taifa letu la kesho. Hawa ndio viongozi wa baadaye, madaktari, walimu, wahandisi, na hata wazazi wa taifa linalokuja. Lakini kwa masikitiko makubwa, wengi wao wanakosa sare za shule, madaftari, kalamu, na hata mlo mmoja wa uhakika kwa siku wakiwa shuleni. Tunaishia kufurahi na kucheka kuona watoto wanakula ice cream za shilingi mia moja.
images - 2025-07-01T214555.456.jpeg

Kuna wanafunzi ambao huamka asubuhi wakiwa hawajala, wanatembea kilomita nyingi kwenda shule, wakifika hawana hata daftari la kuandika, na walio na madaftari yamechakaa sana na bado tunategemea wapate elimu bora. Hii siyo haki hata kidogo.
images - 2025-07-01T214640.968.jpeg

Ikiwa serikali inaweza kugharamia chakula cha wafungwa, mavazi ya kila mmoja, huduma za afya na hata usalama wao, basi ni dhahiri kuwa ina uwezo pia wa kugharamia sare za shule kwa watoto wa shule za msingi, kuwapatia chakula shuleni, na vifaa vya kujifunzia.
images - 2025-07-01T214544.772.jpeg

Hili ni suala la vipaumbele ingawa kwa wengi watalitazama kwa umakini mdogo kwani watoto wao hawapo kwenye hizo shule. Asilimia kubwa kama sio yote ya wabunge na viongozi wanaosimamia elimu wamewapeleka watoto wao shule za kiwango cha juu.
images - 2025-07-01T214622.930.jpeg

Mfumo wa elimu ya msingi unahitaji mageuzi ya kweli. Tunahitaji sera madhubuti itakayowezesha kila mtoto anayeandikishwa shule ya msingi ya serikali apate sare bure, vifaa vya shule kama begi, madaftari na kalamu bure, pamoja na mlo wa mchana bure. Hili sio jambo gumu, bali ni suala la dhamira ya kisiasa na kipaumbele katika bajeti ya kitaifa.
images - 2025-07-01T214555.456.jpeg

Mtoto anayesoma akiwa na furaha, akiwa na tumbo lililoshiba, na akiwa na mahitaji yake yote ya shule, ana nafasi kubwa zaidi ya kufaulu na kulisaidia taifa lake hapo baadaye.
images - 2025-07-01T214640.968.jpeg

Tuache unafiki wa kisiasa—tuwekeze kwa mtoto wa Kitanzania. Kama tunavyowapatua huduma wafungwa, tuwajali pia watoto wetu. Kwani wao ndio matumaini pekee ya taifa hili.
 
Wanafunzi si wana wazazi wao
Yaani wewe uzae, serikali iwajibike kumlisha mtoto wako
Wazazi tuwajibike, nyege na starehe zako usumbue serikali
Serikali imelipa walimu, unataka ilishe tena
 
Back
Top Bottom