Kwanini Serikali huwa inatangaza bajeti kubwa kuliko uwezo wa makusanyo na vyanzo vya mapato?

Kwanini Serikali huwa inatangaza bajeti kubwa kuliko uwezo wa makusanyo na vyanzo vya mapato?

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Nilikuwa najisomea taarifa ya mkaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka 2018/2019, hizi taarifa zinaonyesha serikali ya wanyonge inavyodanganya wanyonge wake.

Serikali ya wanyonge imekua ikitaja bajeti kubwa sana lakini uhalisia unaoneysha kua hizi taarifa ni kama vile hua zinaandaliwa na watu ambao hawakwenda shule au wanaziandaa tu kufurahisha wajinga.
IMG_20200409_093538.jpg

Tusome hicho kiambatanisho hapo juu kinaeleza kila kitu.

Mwaka 2018/2019 bajeti Trillioni 32.48, makusanyo yote Trillioni 25.82, hii ni sawa na 79% ya malengo ya bajeti, hivyo serikali iliweza kukusanya 79% ya malengo yake kwa mwaka, 21% haikukusanya ambayo ni Trillion 7. Hiyo 79% mapato ya kodi ni 60% ambayo ni Trillioni 15 sawa na 46% ya bajeti, jumla ya mapato bila mikopo ni Trillioni 17 sawa na 53% ya bajeti. 47% ya mapato yote ya 2018/2019 ni mikopo na misaada.

Mwaka 2017/2018 bajeti Trillioni 31.7, makusanyo Trillion 27.7, hii ni sawa na 87% ya malengo, 13% ya malengo sawa na Trillion 4 haikukusanywa. Hii 87% mapato ya kodi ni 55% sawa na Trillion 15.2 sawa na 48% ya bajeti, jumla ya mapato bila kodi ni Trillion 16.62, sawa na 60% ya mapato yote au 53% ya bajeti, 40% ni mikopo na misaada.

Mwaka 2016/2017, hii ndio ilikua bajeti ya kwanza ya serikali ya wanyonge, hapa tulisikia matamko ya majigambo hatujawahi kusikia. Hapa mdio pale 1.5T haikuonekana matumizi yake na ikapelekea CAG aliekuwepo kutimuliwa kazi. Twende kwenye hesabu.
Bajeti ilikua Trillion 29.5, tukakusanya 25.3 sawa na 86% ya bejeti. Hii 86% mapato ya kodi ni 57% sawa na Trillion 14.4, sawa na 48% ya bajeti, mapato yote kabla ya mikopo na midaasa ni 65% sawa na Trillion 16.45, sawa na 56% sawa ya bajeti, iliyobaki 35% ya mapato ni misaada na mikopo.

Kwanza, CAG yuko sahihi, TRA haijawahi kufikia lengo(yeye mwenyewe akiwemo) walikua wanapika taarifa kuwadanganya wanyonge.

TRA hawajawahi kukusanya zaidi ya 50% ya bajeti, uliangalia kuanzia 2016 hadi 2019 wamefanikiwa kuongeza Bilioni 700 tu kwenye makusanyo yao, 2016 walifikisha 14.4T, 2019 wakafikisha 15.2T.

Mapato yetu ya ndani hayajawahi kuvuka 55% ya bajeti na 65% ya makusanyo yetu yote.

Swali, kwa nini hua tunataja kiwango kikubwa cha bajeti huku mapato yetu hayazidi 55% ya bajeti, hivi kweli unaweza kuandaa bajeti ambayo zaidi ya 45% unategemea ukope au upewe msaada, je wakopeshaji wakikukatalia ama wanaotoa msaada wasipotoa? Ni kwa nini tusitaje bajeti ya Trillion 18 au 19 ambazo tuna uhakika wa kuzipata kwa 95% kuliko kutaja 32 ambayo uhakika wa kuipata ni 55%, tunamdanganya nani au kumfurahisha nani?

Kwa miaka yote 4 ina maana serikali haikutekeleza bajeti yake kwa zaidi ya 20%, hii matangazo ya tunatekeleza yanatoka wapi?

Tunajua mapato ya kodi tu hayawezi kulipa mishahara na kulipa madeni ya nje, ina maana matumizi ya mishahara na madeni pekee yamakomba mapato yetu yote ya ndani, bado oc, hela yote inayobaki inaenda stiglers na sgr, hela imeisha.

Uchambuzi unaendelea.
 
Natomana gete gete!
Ango baleyomba tole na mahela mingi
Neyo lolo
 
Kwasababu tunajua kuishi na watu, tuna marafiki wengi watatufadhili, bahati mbaya jamaa wanapunguza misaada, but bado tunaendelea kuwategemea tu kwenye kila bajeti.

Madini na vyote tulivyonavyo tunaona sio kitu, tumeishadumaa akili.

CCM oyeee..!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me mwenyewe hiki kitu huwa nakishangaa sana maana unakuta serikali inapitisha bajeti ambayo haitekelezwi kabisa. Kwa mfano suala la ajira, unakuta serikali Inatangaza kabisa kuwa kwa mwaka huu wa fedha serikali imepanga labda wizara fulani kuajiri watumishi wapya labda 5000. Lakini cha ajabu mwaka unaisha hata mtumishi mpya mmoja kwenye wizara hiyo haja ajiriwa.

Sasa kunakuaga na maana gani kutaja idadi ya watumishi wapya mtakao ajiri arafu Mwaka unaisha wizara haiajiri mtumishi hata mmoja? Ni kwa nini tu msiseme wizara itaajiri watumishi 50 na kweli mkafanya hivyo kuliko kusema 5000 arafu huajiri kabisaaa.


Serikali isifanye wananchi wajinga maana ni bora umpe mtu shilingi hamsini nzima kuliko kumpa shilingi mia mbovu.
 
Huwa wanasema higher

Wengine wanasema think globally and act locally
 
Back
Top Bottom