GE2025 Kwanini Serikali huwa inawaajiri Mawakili wenye uwezo mdogo sana?

GE2025 Kwanini Serikali huwa inawaajiri Mawakili wenye uwezo mdogo sana?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kama unafuatilia, utagundua kuwa siyo hii kesi ya Lisu pekee ndiyo iliyodhihirisha uwezo mdogo wa mawakili wa Serikali.
Kama unafuatilia, kesi ya ugaidi dhidi ya Mbowe, kesi zile zilizofanyika nje ya nchi kuhusiana na Serikali kukiuka mikataba ya uwekezaji wa makampuni ya kigeni kwenye sekta ya madini, kote huko ilikuwa ni aibu tupu.

Utambue kuwa hawa mawikili kwenye mahakama za usuluhishi huko nje ya nchi, hawajawahi kushinda kesi yoyote.

Jawa mawakili bila ya kusaidiwa na mahakimu au majaji vipenyo waliotumbukizwa ndani ya mahakama, hawashindi kesi. Ndiyo maana huko mahakama za nje ambako mahakama hazipokee maelekezo kutoka Serikali ya Tanzania, wakati wote huwa wanaangukia pua. Na hata hapa nchini, wakikutana na majaji au mahakimu huru wanaoheshimu taaluma yao, mara nyingi huwa hawashindi. Ushindi wao hutegemea uwepo wa hakimu au jaji kipenyo.
Unatakiwa ujue utofauti kati ya kesi ya kutengenezwa na kesi halisi.
 
Ajira ina miongozo yake.

Hata T.Lisu akiajiriwa atakuwa kama hao waliopo, unaenda kazini, unafanya unachoambiwa unarudi nyumbani, mwisho wa mwezi unalipwa.

Unadhani kwanini majaji hawaifuti kesi hiyo licha ya kasoro zilizoonekana?

Wanalipwa mshahara nao wana mabosi wao, wakifanya kinyume hawana kazi.
 
Ukifuatilia kesi bandia ya Serikali dhidi ya Tundu Lissu, unapata ujumbe mmoja ulio dhahiri kabisa kuwa, "Mawakili wa Serikali wana uwezo mdogo sana wa akili na Taaluma!

Maswali Muhimu ya kujiuliza:

1. Ni kweli mawakili wa Serikali ni watu wenye akili na weledi mdogo sana? Kama ndivyo, kwa nini Serikali huwa inawataka hao mawakili wenye akili na uwezo mdogo sana? Je, yawezekana Serikali inaamini kuwa ikiwaajiri mawakili wenye akili na uwezo mzuri wakakataa kutumika kama vikaragosi?

2. Je, yawezekana hawa mawakili wana akili na uwezo mzuri, bali kwa makusudi huwa wanajifanya wana akili na uwezo mdogo, kama njia ya kupinga kutumika kwao kama vikaragosi?

3. Je, yawezekana wana akili na uwezo mzuri, lakini kutokana na dhamira mbaya na shetani aliyejaa mioyoni mwao, Mungu huamua kuwaaibisha, ili kuonesha ukuu wake?

Kwa kweli uwezo na hoja za mawakili wa Serikali, naamini hata mwanafunzi wa mwaka wa pili wa sheria anaweza kufanya arguments bora zaidi za kisheria kuliko hawa vilaza?
Unajua tatizo la taasisi za serikali na wafanyakazi wake ni ukofesu wa exposure. Sasa unakuta waziri ameenda kwenya kwenye mkutano anatoka hoteli anaenda kwenye mkutano na baadae hotelini wiki nzima then anapata siku 1 anatembelea miradi ya nchi jirani, then atakuja kusimulia ya huko kama mtu mwenye experience wakati alipata 1 day off yakutembea .
 
Back
Top Bottom