Kwanini Serikali ilituficha kuugua kwa Dkt. Magufuli?

Yote sawa, isipokuwa hilo la Gwaji girl! ... kutokana na terror tactics zake, ujuaji na imani potofu alizojilisha Jiwe, ilifika wakati watendaji wake wote wakawa wanangojea maagizo kutoka kwake, kuhusu kila kitu, na si vinginevyo! ... YAANI HAKUKUWA NA NAMNA TENA!
 
Serious gani ulishawai sikia wapi jiwe likiugua? Hayo maombi yalishindikana siku zote anaomba aombewe ndio uje kuomba akiwa mgonjwa
 
Natabiri tu serekali ijayo itakuja kutaja walio muuwa jpm
Membe is on record kuonya vyombo husika vya kuteua candidates wa Urais, wasije teua tena watu wenye traits za kukosa Utanzania.
Watanzania ni wastaarabu, waungwana ,wanavumiliana na siasa ni za kuelewana.
Vitu hivi havikuwepo Awamu iliyopita.
 
Waliogopa angepona angewafukuza Kazi wote


Nimekuelewa lakini ndipo sasa inahitajika Katiba kuweka Sawa mambo kama hayo, haiwezi mtu aamue kufukuza watu sababu ya mtazamo wake tu au hasira zake n.k.

Lakini kuwe na Organ (s) za ku review na ku approve au kupinga kwa vigezo.

Jamaa walikuwa wanamuogopa kupita kiasi, wanaume kwa wanawake waliufyata!

Hivi kwanini ilifikia hatua hiyo?
 
Aliyekuwa anamuogopa Hayati Magufuli basi ni lazima alikuwa sio muwajibikaji.
 
Hakuogopwa yeye bali mabunduki yaliyobebwa na wazee wa kufuata amri. Nje ya mabunduki mbona ni mweupe sana hakuwa na uwezo hata kupigana na mie.

Hata huyu aliyepo sasa akiamua kutumia wazee wa mabunduki na amri mbona ataonekana anagopwa kumbe watu wanaogopa kunyamazishwa kwa bunduki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…