Kwanini Serikali ilituficha kuugua kwa Dkt. Magufuli?

Kwanini Serikali ilituficha kuugua kwa Dkt. Magufuli?

Magufuli ameweka standards za uongozi Tanzania wahuni watake wasitake...

Mapinduzi yajayo ya Serikali yatakuwa kwa Jina la Magufuli. Na Nina hofu Magufuli amekufa na CCM mioyoni mwao..
Mimi sio mshabiki wa vyama lakin nikuambie tu. Ccm wataendelea kubakia maana wana mizizi deep down kwenye taasisi za serikali. Hiyo 2025 unayoisemea utakuwa suprised na akili za watanzania.

Watakirudiaha chama kile kile na kuendelea kulaumu kama kawaida
 
Naamini afya ni jambo la mtu binafsi, pili mwenyewe alikuwa na nafasi ya kuzungumzia afya yake, siku anamwapisha bashiru kuwa k/kiongozi akuongea chochote wadadisi wanadai hakuwa vizuri kiafya!
 
Kama sikosei, mpaka sasa Rais Samia keshaongea na waandishi wa habari kama mara mbili hivi.

Ni zaidi ya mwezi sasa tokea alipoongea na wahariri wa vyombo vya habari/ waandishi wa habari toka ikulu ya Dar es Salaam.

Wiki moja au mbili zilizopita, akafanya mahojiano na Salim Kikeke wa BBC.

Katika nyakati zote hizo mbili, sikusikia kabisa akiulizwa ni kwa nini serikali yake ilituficha kuhusu kuugua kwa Rais Magufuli.

Wananchi hatukupata taarifa zozote zile zilizo rasmi hadi tukaishia kutegemea habari umbea na zisizo rasmi kupitia mitandao ya kijamii.

Kimya kilipozidi kutanda, tukaanza kudokezwa dokezwa kuwa hali si nzuri, mara sijui yupo anachapa kazi, mara sijui anafanywa nini…

Haikupendeza hata kidogo. Na hata vyombo vya habari vya kimataifa viliripoti kuhusu tetesi za kutoonekana kwa Magufuli.

Kwangu hili halikubaliki kabisa!

Wananchi kama waajiri wa hawa viongozi wetu, tuna haki ya kujua kuhusu afya za viongozi wetu.

Hapa simaanishi kila kitu kuhusu afya. Namaanisha tu ile kwa ujumla wake.

Kama mtu anaumwa, kalazwa, tuna haki ya kujua.

Mambo ya kuficha/ kufichwa halafu mnakuja tu kuambiwa mtu kaaga dunia, hayafai.
Hivyo, ningependa sana kujua kwa nini wananchi hatukupewa taarifa.

Na itokeapo fursa ingine ya Rais Samia au hata waziri mkuu Majaliwa kuongea na waandishi wa habari, ningependa kuona na kusikia wakiulizwa ni kwa nini hawakutufahamisha kilichokuwa kinaendelea.

Pascal Mayalla take note and spread the word.
Maadui wengi walikuepo wanamtafuta especially mafisadi
 
mbona umepaniki mkuu, kwani kuna mtu amesema anamtafuta mtu aliyemuua Rais? si tunaongea tu.

kuna sehemu nimeandika Rais aliuawa hadi aliyemuua atafutwe !!

Hii ndio sababu naonelea Jf ibakie na tag ya "Where we dare to talk openly" maana hii inaruhusu watu kuongea ongea kama unavyotaka , ila ya "home of great thinkers" ishapwaya kama sensitive issue kama hii inajadiliwa bila hard facts kama udaku wa WCB
 
Nasikia yule baba alikufa akiwa kajificha chumbani kwake kwa sababu ya maradhi yake sugu ya akili
 
Magufuli ameweka standards za uongozi Tanzania wahuni watake wasitake...

Mapinduzi yajayo ya Serikali yatakuwa kwa Jina la Magufuli. Na Nina hofu Magufuli amekufa na CCM mioyoni mwao.

Rais wa Sasa ni either akubali kupumzika 2025 au alazimishe kuendelea ili aiue CCM Rasmi.

Hawa akina Warioba, Pinda, Mangula hawamtaki aendelee ndio maana wanahakikisha Mchakato wa tume huru na Katiba zirejewe haraka, ili wasishindane na Wanaojiita wenye CCM ndani ya CCM.

Akina Sumaye walipelekwa upinzani ili kuandaa njia
Bangi ya Malawi haikufai, acha.
 
No!

We have to hold our leaders [who work for us] to account.

They have a solemn responsibility to be forthright with us.

If we let bygones be bygones, we will be giving them the license to willy-nilly take us for a ride whenever they feel like it and they can invoke that bullshit to eschew their responsibilities knowing that no one cares to know.

I’m not here for it.
Wakati wanatuomba kura hawakujificha ila wakishapata inakuwa halali kwao kutuficha hali zao tena kwa kutudanganya kama watoto. Tunawaaminije sasa?
 
Tuache unafiki.
Hata vitabu vya dini vya kale vinasema auaye kwa upanga atakufa kwa upanga huo huo.

Tusijidai tumesahau ramsha ramsha za kunywa mpaka asubuhi sehemu za Kimara na kwingineko siku ya tangazo la kifo.
Umekumbuka kunywa Kidonge chako cha Ugonjwa wa Akili ( Uwendawazimu ) ulionao leo hii?
 
Mimi sio mshabiki wa vyama lakin nikuambie tu. Ccm wataendelea kubakia maana wana mizizi deep down kwenye taasisi za serikali. Hiyo 2025 unayoisemea utakuwa suprised na akili za watanzania.

Watakirudiaha chama kile kile na kuendelea kulaumu kama kawaida
Tatizo sio CCM kushinda, la hasha, tatizo kura chache za upinzani wapewe wasinyang'anywe, kwani ni halali yao na zinasaidia kuweza kupata ruzuku za kuendesha chama!
 
Nafikiri pia misimamo yake kuhusu korona pia ilichangia hii korona ni mradi wa watu Fulani.wanaoongoza dunia kupita mlango wa nyuma.
 
Back
Top Bottom