Kwanini Serikali inanunua magari ya Tsh 300M hadi 500M?

Kwanini Serikali inanunua magari ya Tsh 300M hadi 500M?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Haya nayo ni majabu ya Tanzania. Pamoja na kwamba naunga mkono tozo lakini siungi mkono Serikali kununua magari ya kifahari. Magari ya kifahari tuwaachie watu binafsi na sio serikali.

Kwenye hili tusilaumu Serikali iliyopo pekee hata Kikwete na Magufuli walitumia pesa vibaya sana na hasa Magufuli kwenye ziara zake na misafara mikubwa.

Hakuna sababu ya msingi ya Serikali kushindwa kupata magari mazuri tena na warranty kwa 100M za Kitanzania.

Hatuwezi kuendelea kutetea Serikali kama haitachukua hatua za haraka kwenye hili. Serikali imekuwa ikijivuta vuta sana.

Natambua serikali ilitaka kuja na utaratibu wa kukopesha lakini wafanye haraka.

Serikali inaongoza mazuzu, majinga na mapoyoyo yasiyohoji na hayaelewi kama fedha zinazotumiwa na serikali ni zao na wanapaswa kuhoji matumizi yake.

Naiomba serikali inunue magari ya bilioni 1 ,2 au 3 mpk haya matanzania yaamke.
 
Serikali inaongoza mazuzu, majinga na mapoyoyo yasiyohoji na hayaelewi kama fedha zinazotumiwa na serikali ni zao na wanapaswa kuhoji matumizi yake.

Naiomba serikali inunue magari ya bilioni 1 ,2 au 3 mpk haya matanzania yaamke
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Watanzania bwana, kila kitu tozo tuuu wakati imeanzishwa juzi tu na magufuli, na walalamikaji wengi ni walalahoi ambao walikua hawalipi kodi kwa kuhisi inalipwa na matajiri tu kumbe inalipwa na kila mtanzania haijalishi kipato chako sasa imebuni mbinu ya kuwakamua wote kelele nyingiii[emoji23][emoji23]

Kuhusu magari ya serikali mjue tu sheria inawabana, hairuhusu kununua chochote cha mtumba bali mpyaaa na karatasi lake sasa sisi tunanunua ya miaka 10 nyuma tunaona jipya [emoji23]
 
Kwenye tozo mimi nina ropic nzima ya kusema nina unga mkono tozo hilo liwe wazi.

Unasema sheria ya magari mapya mbona kuna magari mapya mengi ya bei ya $30,000 na chini inakuwaje mapya iwe maana ya Tsh 300M hadi 500M.

Hivi ni visingizio nakimbuka zamani kulikuwa na 505, Renaults, Carina sasa tuna barabara nzuri ofisa wa mjini na V8 ya nini? Yaani wafanyakazi wa Dar na mijini wote kuna sababu gani au ulazima wa kuwa na VX

Imekuwa ni aibu wanao tusaidia pesa kwenye shule na afya wanatumia magari ya kawaida. Hapa US viongozi wanatumia jeep na Ford na sisi tuna ushamba wa kujionyesha tena serikali kama sifa vile kununua magari ya tsh 500M
 
Unaunga mkono tozo, halafu unashangaa matumizi ya tozo?

Hii Nchi ina watu wa ajabu sana
Halafu yupo marekani kwa akili hizi za kushikiwa sijui hata kafikaje huko??
 
Sina tatizo na tozo hata kidogo, lakini naona Serikali ituoneshe wazi kwamba inachotueleza umuhimu wa kupata pesa za kugharimia miradi ni muhimu. Na ili kutuonesha hilo ni lazima kihekima Serikali ibane matumizi.

Serikali yetu inanunua magari ya fahari sana ambayo hayaendani na uhalisia wa maisha yetu. Pia viongozi wajipunguzie marupurupu na posho. Na hayo marupurupu kidogo watakayolipana yakatwe kodi.

Vinginevyo kuendelea kuwakamua wananchi kila siku kunajenga chuki kati ya wananchi na serikali yao.

Kila siku tunakutana na wafanyakazi wa serikali Dar es salaam, wanasema wamekuja kikazi. Hao wanalipwa pesa za safari na mengineyo. Sasa kulikuwa na umuhimu gani wa kuhamishia Serikali Dodoma?

Na pia iko haja ya kupunguza idadi ya magari yanayosindikiza msafara wa Mh Raisi wetu. Jamani msafara wa magari zaidi ya 70 wa nini kwa nchi masikini kama Tanzania? Kwenye msafara huo siyo mafuta tu yanatuumiza, ni pamoja na watu kwenye huo msafara lazima walipwe posho.

Jamani hivi kweli kabisa katika dunia ya leo bado tunaamini kwamba msafara mrefu wa magari ndiyo usalama wa Mh Raisi wetu?. Sasa hivi mambo yako kdigital zaidi kuliko analogy. Adui anaweza akafanya jambo baya akiwa yuko miles 10,000. Tafadhali tuliangalie na hilo.
 
Kuhusu Wabunge wetu nilikuwa napendekeza kwamba tununue mabasi 7 na tuyagawe kwa kanda. Wabunge wa Mkoa Ruvuma, Mbeya, Katavi, Iringa na Njombe watumie basi moja ambalo litawabeba wote kuwaleta Bungeni na kuwarudisha.

Na kaskazini pia wabunge wa Arusha, Kilimanjaro, Tanga nk nao watumie basi moja. Kila kanda iwe na basi lake.

Na pale Bungeni tuwajengee Hosteli ama mabweni. Wabunge wawili chumba kimoja. Kunakuwa na wafanyakazi wa kuwapikia, kuwafulia na kupiga pasi.

Hiyo yote itasaidia sana kupunguza gharama na kuwapunguzia wananchi mzigo.
 
Kwenye tozo mimi nina ropic nzima ya kusema nina unga mkono tozo hilo liwe wazi.

Unasema sheria ya magari mapya mbona kuna magari mapya mengi ya bei ya $30,000 na chini inakuwaje mapya iwe maana ya Tsh 300M hadi 500M.!

Hivi ni visingizio nakimbuka zamani kulikuwa na 505, Renaults, Carina sasa tuna barabara nzuri ofisa wa mjini na V8 ya nini? Yaani wafanyakazi wa Dar na mijini wote kuna sababu gani au ulazima wa kuwa na VX

Imekuwa ni aibu wanao tusaidia pesa kwenye shule na afya wanatumia magari ya kawaida. Hapa US viongozi wanatumia jeep na Ford na sisi tuna ushamba wa kujionyesha tena serikali kama sifa vile kununua magari ya tsh 500M
Bado unaunga mkono tozo!!!

Shida yako unataka kufananisha Tz na marekani sijui kwa nini. Na inaonekana unang'ang'ania hapo hapo! Linganisha Tz na nchi yenye mazingira ya Tz ambapo tozo zimefanikiwa....

Mimi naishi mjini na ni wa kipato cha kati kwa kukadiria kwa viwango vyetu. Tozo zinaniathiri kama ifuatavyo kulinganisha na mmarekani wa Texas wa level yangu:

Asilimia kubwa ya watz wanaishi vijijini, ambapo kiwango cha umasikini ni kikubwa.

Maskini wa vijijini wanategemea mtu kama mimi tulioko mjini kupata misaada na tunatuma kwa miamala. Wamarekani/Ulaya hawana social/family dependency kubwa nje ya mke na watoto kama ilivyo sisi, utamaduni huu hawana. Mie kutuma miamala ya misaada inakuwa kama jukumu.

Kwa hiyo serikali inaposema "tunaongeza wigo wa kodi" kwa kuhesabu watu wa vijijini, wanasahau kuwa wanakuwa wameniongezea kodi mie, sababu kule kijijini kilimo hakilipi, mie ndio na sustain maisha kule kwa kupitia miamala. Kama unaijua vizuri TZ utaelewa hili na hii ni tofauti na wamarekani kama nilivyosema.

Mzigo wa kodi kwa mtanzania wa ngazi ya kati na chini ni mkubwa sana kutokana na majukumu ya extended family!!

Jiepushe kulinganisha TZ na marekani. Linganisha TZ na nchi inayoendana nayo kwa kipato na way of life...
 
Back
Top Bottom