Kwanini Serikali inanunua magari ya Tsh 300M hadi 500M?

Oyaa acheni ujinga hata hayo magari ya mil 300-500 bado Ni ya pesa ndogo Saaaaana,wanatakiwa waendeshwe na Maybach,Rolls Royce,G-Wagon.Kwa wakuu wa mikoa Lamborghini zitawafaa.

Poleni viongozi wa serikali kwa kuumia migongo kwa Sababu ya kuendeshwa na magari ya Bei rahisi.

Wanyonge tuko tayari kuwakanda.
 
Habari za Kikwete na Magufuli walifanya hazina maana yoyote hapa.
Kujisahihisha ndilo la muhimu.
Kosa la mmoja halihalalishi la mwingine.
 
Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere likamilike. Hatutaki kusikia makusanyo ya tozo hayatoshi kuleta winchi ya kubeba mageiti! Sijui najadili kitu gani!
 
Kuna shida gani ikinunuliwa harrier?
Kweli ndugu yangu, nchi inatakiwa kuenenda kulingana na hali yake ya kiuchumi, na sio kuonyesha matumizi anasa' wakati ni maskini! Nchi kama Botswana huwezi kuta wana matumizi ya serikali 'zembe kama unavyoona Tz.....
 
Hiyo sentence yako moja tu ya kuunga mkono tozo, inaonyesha unafikiwako.
 
Kwa nini kama magari wanayapenda wasinunue kwa hela zao wanatumia za walipa kodi ndio maana hata kelele za kodi kubwa kwenye magari hawaisikii kwa sababu muda mwingi wanatumia gari za Serikali..na wengi wao wakistaafu ndio maumivu haya wanaanza kuyapata..
 
Kwani mkuu hujaona serikali wakitumia magari madogo? Hadi bajaji na pikipiki zipo pia
 
Wanazitumia kwa masafa marefu,

Kwani Watanzania ni wajinga kwanini wasinunue pickup double cabin kama ni kwa safari?. Na pili wanaenda wapi wakati kuna viongozi Tanzania nzima. Yaani wewe ni Mkurugenzi Dodoma unaenda Mwanza kufanya nini hasa wakati kule kuna viongozi. Kama ni shughuli au ni kijijini kwenye tumia usafiri wako binafsi.

lakini Watanzania wengine wasio na V8 wanasafiri vipi?
 
Unataka gari ya Raisi wa Nchi inunuliwe harrier?
Unadhani wakati wa nyerere hakukuwa na gari za kifahari ? Mzee wetu ndo pekee aliekuwa anajali shida zetu si hawa walamba asali.
 
kwani suzuki ni shs ngapi? hata landrover zinatosha sana.
 
Sasa wewe mwenyewe unawakandia yet unaunga mkono waongeze kodi!!! Yaani una ndoo unaona kabisa inavuja maji yet una fight iendelee tu kujazwa maji!!!!
 
Sheria,Iko sahihi mitumba ni ghali zaidi, lakini je hakuna magari mapya ya chini ya 300,?hakuna new brand60m? Tuamini kwamba serikali inamiliki magari ya300-500m?
 
Sasa wewe mwenyewe unawakandia yet unaunga mkono waongeze kodi!!! Yaani una ndoo unaona kabisa inavuja maji yet una fight iendelee tu kujazwa maji!!!!

Walipa kodi bado kidogo lakini serikali nayo inatakiwa kupunguza matumizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…