Kwanini Serikali inaogopa wachunguzi wa Kimataifa?

Kwanini Serikali inaogopa wachunguzi wa Kimataifa?

Wakati mwingine uwe unaficha ujinga wako wewe uthamini pesa kuliko utu. Mbona serikali imetumia gharama kubwa kwenye vipimo vya Faru John ambaye huyo alikuwa ni mnyama. Kwenu mnyama ana thamani kuliko binadamu? Subiri siku ukipotea wewe au ndugu ndo utajua.

wewe binafsi utachangia bei gani tuwalete?
 
Embu tuwekeee majina na pembeni sababu za.hao uliosema eanatekwa sijui nini a kwa sababu zipi?

Yaani hata list hamuweki isomeke kutetemesha nchi, mnataka tu kutisha watu. Hamna sera zingine za kupambana na serikali? Raisi kuwabana kwenye mengi wanakalia kusukuma mambo ambayo wakikaa chini na kuangalia yaliyotokea nchi zingine matatizo wanayosukuma kuwa yapo nchini kwa uongo, basi wangekuwa wameshachimba maandaki kujificha hayo yasiwatokee.

Wote muache kutaka kuchafua serikali ya Mh. JPM, kama wanataka kufanya vikao wapate posho waje na mengine na sio haya yasio na kichwa wala miguu wala proof. Watu wameripoti waache uchunguzi uendeleee kwa aliyepotea na wanaopotea na kurudi. Hakuna lililotendwa na serikali hawana proof kabisaa bali kusingizia, waheshimu uchunguzi ufanyike ipasavyo. Eti kwa sababu watu wanaoisoma namba wanayaongelea na kusingizia basi na wao wanadakia.huku mapaparazi wakipokea bahasha kuchochea issue ambazo hazitusaidii wananchi wengi sie wa huku vijijini.

Serikali haina muda kujadili udaku.

Hapa kazi tu
Wewe badala ya kujibu hoja unakuja na mihemko yko kma umevuta bangi mbichi,nafasi za uteuzi zimeisha kuna wenzako jf elizaboni,jingalao,stroke,,ruta wamepiga debe miaka hata ukatibu kata hawakupewa,
Unakuja n porojo zko dhaifu eti hapa kazi tu wakti comedy ndio kazi tu kwasasa hakuna jipya lolote dawa hosp hakuna,ajira hakuna,mishahara shida,makampuni makubwa kma tbl,cocacola,tanzania distillers wanapunguza wafanyakazi.

Wakti tbl ndio mlipa kodi mkubwa no 1 tanzania halafu wewe unakuja na porojo zko za makonda hapa,shubaaamitt
 
Wakati mwingine uwe unaficha ujinga wako wewe uthamini pesa kuliko utu. Mbona serikali imetumia gharama kubwa kwenye vipimo vya Faru John ambaye huyo alikuwa ni mnyama. Kwenu mnyama ana thamani kuliko binadamu? Subiri siku ukipotea wewe au ndugu ndo utajua.
Kweli.watu wengine ni vichwa vigumu Ben ni binaadamu ana familia
 
Police na vyombo vyetu vingine wanaiweza hii kazi haihitaji hayo. Tutawakamata tuuu.
Labda kama atapatikana Mulundi mwingine kutoka Kenya na kwenda kanisani kwa Gwajima kukiri ndiye aliyemteka Ben. Mwenye taarifa za yule Mulundi wa Ulimboka aliishia wapi tunaomba atujulishe, mara ya mwisho alikuwa amegoma kula kule mahabusu. Kitengo kina sanaa nyingi.
 
Ujinga gani umeandika ,utumbo tu uchunguzi wa nje kwani umeambiwa vyombo vya usalama nchini vimeshindwa au unaandika tu na we we uonekana umeandika acha uvivu wa kufikiri na kutukuza wageni huo in utumwa na ukosefu wa afya ya akiri na umasikini wa elimu huku ukisumbuliwa na njaa ndio maana unaikibidhi akiri yako kwa wenyewe uwezo wa kfkr ukiamini watakutatulia shida zako hao wachunguzi hatuwataki vyombo vyetu ni imara na kazi zake vina compliance

Be reasonable what you say. Ametoa maoni na ushauri wake. Kuna tatizo kubwa, watu wamepotea katika mazingira ya kutatanisha, sasa ni miezi sita na zaidi, na hakuna hata dalili kwamba kuna utatuzi umepatikana. Unataka mpaka baba yako apotee ndipo utaoana hilo kama tatizo kubwa? don't be an idiot.
 
Ina maana hatuna wachunguzi waliobobea nchini? Usitutie Aibu
 
Jumamosi April 15 mwaka huu umoja wa kizazi cha kuhoji nchini (UTG) ulifanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea juu ya matukio mbalimbali ya watu kupotea, kutekwa na wengine kuuawa. Katika mkutano huo tulieleza baadhi ya hatua tulizochukua kuhusu hali hii ya kuogofya inayoendelea nchini kwa sasa.

Moja ya hatua hizo ni uongozi wa UTG kukaa mezani na uongozi wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini (LHRC) kuomba kituo hicho kupeleka malalamiko rasmi Umoja wa mataifa (UN) juu ya matukio ya watanzania kupotea, kutekwa na kuuawa.

Tuliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuwasiliana na Mkurugenzi wa kituo hicho Dr.Hellen Kijo Bisimba ambaye alishiriki mkutano wa umoja wa mataifa wa taasisi za kiraia zinazoshughulika na masuala haki za binadamu ambapo aliweza kupenyeza hoja kuhusu watanzania kupotea katika mazingira ya kutatanisha akihusisha suala la Ben Saanane ambaye ni Katibu Mkuu wa UTG Tanzania.

Baada ya kuwasilisha hoja hiyo Umoja wa mataifa ulimtaka Dr.Kijo kuwasilisha kwa maandishi malalamimo hayo ili waweze kutuma wataalamu wake kuja kuchunguza. Ieleweke kwamba Umoja wa mataifa una chombo huru cha uchunguzi kiitwacho "The Observer" na kina uwezo wa kuchunguza matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi yoyote mwanachama (Tanzania ikiwemo).

Hivyo basi UTG tulishirikiana na LHRC kuhakikisha kuwa barua hiyo inaandikwa na kufika katika utaratibu rasmi ili waweze kutuma wataalamu hao kuja kuchunguza. Tayari barua hiyo imeshaandikwa na tunasubiri majibu.

Dhumuni la kufanya hivyo ni kwa sababu hatujaridhishwa na utendaji wa vyombo vyetu vya ndani. Tunaamini vyombo vya kimataifa vinaweza kuwa huru zaidi kuchunguza mambo haya ya watanzania kupotea, kutekwa na kuuawa bila hatia.

Leo kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mhe.Freeman Mbowe ameonesha dhamira ileile iliyooneshwa juzi na UTG ya kukosa imani na vyombo vyetu vya ndani. Mhe.Mbowe ameomba serikali iruhusu makachero wa Uingereza maarufu kama "Scottland Yard" waje nchini kufanya upelelezi kuhusiana na matukio ya watanzania kupotea, na Mbowe amekua specific kwa Ben Saanane.

Lakini katika hali ya kushangaza Waziri Mkuu amejibu swali la Mbowe kwa majibu mepesi mno. Amesema vyombo vyetu vya usalama vinaendelea na uchunguzi. Katika kuonesha hakubaliani na kuja kwa vyombo vya kimataifa Waziri Mkuu amesema kwa sasa tuviachie vyombo vyetu vya ndani na serikali ikiona kuna haja ya kuita vyombo vya nje basi itafanya hivyo.

Maana yake ni Kwamba Waziri mkuu hadi sasa haoni haja ya kuita vyombo vya nje. Bado anaamini vyombo vyetu vya ndani vinaweza kuchunguza. Mi nadhani Mheshimiwa Waziri Mkuu anapaswa kutafakari upya. Huu sasa ni mwezi wa 6 tangu Ben apotee serikali inasema bado inaendelea na uchunguzi. Kweli?

Hivi waziri mkuu anajua kwamba katika miezi yote 6 hivyo vyombo anavyovitaja vimeshindwa kukamata hata mshukiwa wa suala la Ben, Vimeshindwa kutrace hata simu moja kati ya simu zilizompigia Ben mwishoni, Vimeshindwa kumhoji hata mwandishi aliyesema Ben anaonekana mtaani, vimeshindwa kufuatilia hata mtu aliyefuta baadhi ya post za Ben kwenye ukurasa wake wa facebook (zilizokua zikihoji PhD ya JPM). Hivi ndio vyombo ambavyo Waziri mkuu anasema tuendelee kuviamini.

Hivi Wairi Mkuu najua kwamba yombo hivyo anavyosema tuviamini vimetuhumiwa hadi bungeni kuhusika na njama za utekaji na utesaji? Waziri Mkuu anajua kamba Wabunge wake wa CCM akiwemo Mhe.Bashe wamevituhumu vyombo hivyo waziwazi kuwa vinahusika na kuteka raia wasio na hatia na kuwatesa hata kuwapoteza?

Sasa ikiwa tuhuma za kina Bashe ni za kweli, Waziri mkuu anapata wapi moral authority ya kutuambia tuendelee kuviamini vyombo hivyo? Kama vyombo hivyo vinatuhumiwa kuteka raia, vinawezaje kujichunguza vyenyewe na vikaleta ripoti ambayo tutaiamini?

Kanuni za msingi za sheria zinazuia mtu/taasisi/chombo kuwa hakimu wa kesi yake yenyewe (Nemo judex in causa sua). Sasa kwanini Waziri mkuu anatushinikiza tuviamini vyombo hivyohivyo vinavyotuhumiwa? Yani chombo kinatuhumiwa kuteka watu, halafu chombo hichohicho kinapewa kazi ya kuchunguza watekaji. What do u expect??

Hata kama tuhuma hizo si za kweli lakini kitendo cha kutuhumiwa tu kinavindolea vyombo hivyo sifa ya kuendelea na uchunguzi.

Kwanini Waziri Mkuu asiruhusu vyombo vya kimataifa vije kuchumguza ambavyo tunaamini vitakua fair and objective zaidi kuliko hivi vya ndani vyenye tuhuma lukuki?

Maazimio ya UTG ni uchunguzi wa madai ya watu kutekwa/kupotea/kuuawa yafanywe na vyombo vya kimataifa. Na tayari UTG kwa kushirikisna na LHRC wameshaandika barua Umoja wa mataifa kuomba wachunguzi hao. Leo mheshimiwa Mbowe naye kaomba makachero wa Uingereza waje kuchunguza. Lakini majibu ya Waziri mkuu yanaonesha serikali haipo tayari kwa wachunguzi hao. Swali la msingi ni kwanini serikali inaogopa wachunguzi wa kimataifa?
we jamaa hovyo sana CHADEMA si wanaccho kitengo cha inteligensia kwa nini wasichunguze mnataka serikali tu? kwa taarifa yako file la uchunguzi kuhusu Ben limeshafungwa mmemficha wenyewe halafu mnasumbua watu
 
Inaogopa !!
Nawe umeona uwadanganye wakudanganywa
 
Hivi wewe mama /mdada una mtoto?kama unao mtoto unajua uchungu wa kuzaa?hapa tunaongelea habari ya mtu kupotea wewe unaleta ushabiki.Hebu vaa hivyo viatu vya ndugu wa Ben Saa8,hebu pata picha yule aliyepotea ni kaka yako wa tumbo moja ungejisikiaje?Kuna mambo ya kuweka ushabiki wa vyama lakini pia kuna ubinadamu.Hebu jiongeze basi wewe Cocochanel!
Kila mchuma janga hula na wa kwao. Ben kachuma janga kwa yote aliyokuwa akiyafanya. Kama madhara kayapata kwa kuwa msaidizi wa karibu wa Mbowe ni yeye ndiye aliyekubari kuwa huko. Kama kupotea kwake ni kwa ajili ya michango kwenye mitandao ya kijamii ni yeye mwenyewe aliamua hivyo. Kama amejificha ili kupata kiki ni yeye mwenyewe aliamua hivyo. Hivyo hana budi kula na wa kwao ambao ni ndigu zake na chama chake. Serikali ilipofikia isubiri mwenye taarifa.
 
Wewe unatakiwa kukamatwa na kusema Ben alipo kwani kwa maneno yako inaonekana unajua alipo au alipelekwa wapi au nini kilimpata.
 
Eti wachunguzi wa kimataifa? Kwa matukio yapi haswaa? Au Ben Saanane ambaye bosi wake Mbowe hakushtuka wala kuona umuhimu wa kuripoti tukio la kupotea kwake hadi pale watu walipoanza kupiga kelele mitandaoni.
 
Wewe badala ya kujibu hoja unakuja na mihemko yko kma umevuta bangi mbichi,nafasi za uteuzi zimeisha kuna wenzako jf elizaboni,jingalao,stroke,,ruta wamepiga debe miaka hata ukatibu kata hawakupewa,
Unakuja n porojo zko dhaifu eti hapa kazi tu wakti comedy ndio kazi tu kwasasa hakuna jipya lolote dawa hosp hakuna,ajira hakuna,mishahara shida,makampuni makubwa kma tbl,cocacola,tanzania distillers wanapunguza wafanyakazi.

Wakti tbl ndio mlipa kodi mkubwa no 1 tanzania halafu wewe unakuja na porojo zko za makonda hapa,shubaaamitt
Kwahiyo wewe unaepiga porojo mamvi ashakupa kitu gani ?
 
Nahisi ni afadhali Maumivu ya kufiwa na mtu(ndugu, jamaa, rafiki, mtoto n.k) sababu unajua ameshafariki na hutoonana nae tena hapa duniani kuliko Maumivu ya kupotelewa na mtu ambae hufahamu yuwapi aidha amekufa au bado mzima. Inauma na kusikitisha sana. Mwenyezi mungu aipe subra na moyo wenye imani familia ya ndugu Ben maana ninaimani tutampata akiwa mzima inshaallah.
 
Embu tuwekeee majina na pembeni sababu za.hao uliosema eanatekwa sijui nini a kwa sababu zipi?

Yaani hata list hamuweki isomeke kutetemesha nchi, mnataka tu kutisha watu. Hamna sera zingine za kupambana na serikali? Raisi kuwabana kwenye mengi wanakalia kusukuma mambo ambayo wakikaa chini na kuangalia yaliyotokea nchi zingine matatizo wanayosukuma kuwa yapo nchini kwa uongo, basi wangekuwa wameshachimba maandaki kujificha hayo yasiwatokee.

Wote muache kutaka kuchafua serikali ya Mh. JPM, kama wanataka kufanya vikao wapate posho waje na mengine na sio haya yasio na kichwa wala miguu wala proof. Watu wameripoti waache uchunguzi uendeleee kwa aliyepotea na wanaopotea na kurudi. Hakuna lililotendwa na serikali hawana proof kabisaa bali kusingizia, waheshimu uchunguzi ufanyike ipasavyo. Eti kwa sababu watu wanaoisoma namba wanayaongelea na kusingizia basi na wao wanadakia.huku mapaparazi wakipokea bahasha kuchochea issue ambazo hazitusaidii wananchi wengi sie wa huku vijijini.

Serikali haina muda kujadili udaku.

Hapa kazi tu
Mungu huwa anafundisha na kutoa majibu kwa muda autakao,kama sio wewe basi ndugu au jamaa zako au kizazi chako kinaweza kuja kupata kadhia kama hii.kweli ndugu yako au jamaa yako angepotea kwenye mazingira kama haya miezi sita imeshapita kweli ungeandika kama ulivyoandika?
 
we jamaa hovyo sana CHADEMA si wanaccho kitengo cha inteligensia kwa nini wasichunguze mnataka serikali tu? kwa taarifa yako file la uchunguzi kuhusu Ben limeshafungwa mmemficha wenyewe halafu mnasumbua watu
kama ben kafichwa na chadema wenyewe bc waruhusu intelejisia za kimataifa waje wachunguze tujue chadema ndio wamefanya na km wamefanya wao wewe hauoni n mtaji tosha kwa CCM kwenye chaguzi zijazo...
 
Back
Top Bottom