Lilikuwa jambo la heri sana kuwa hatimaye serikali imeona ni busara kuhusika katika kugharimia matibabu ya mh. Lissu popote kule duniani. Lilikuwa jambo la heri sana sasa kwa vikwazo vyovyote vilivyoko kuwekwa pembeni kuwezesha hili la wadau wote kuchangia ikiwamo serikali kutokea. Ilikuwa ni jambo la heri kubwa kwa pande zinazohusika kuwekeana wepesi katika hili ili kuhakikisha mgonjwa wetu huyu ambaye ni mtanzania mwenzetu kama ambavyo ingekuwa kwa mwingine awaye yote anatendewa haki japo leo yu mahututi hospitalini.
Waswahili wanasema ndugu wawili wakigombana chukua jembe ukalime.
Mh. Lissu hakutendewa haki na waliojaribu kumtoa uhai wake. Mh. Lissu leo hayuko kwenye nafasi ya kujisimamia mwenyewe kuhusiana na hatima ya matibabu yake kwa sasa. Mh. Lissu asiingizwe katika marumbano haya ya kuchangia tiba yake. Hebu sisi kama ndugu tumtangulize mgonjwa wetu mbele dhidi ya maslahi yoyote yale (au ego yoyote ile). Tusimhukumu mgonjwa wetu kwa kuacha kutoa michango yetu kumsaidia wakati angali mzima. Historia isije ikatuhukumu kwa kuendekeza marumbano ya kuhusiana na michango yetu tukimtelekeza mgonjwa wetu wakati tulikuwa katika nafasi ya kuweza kumsaidia akiwa hai. Ya Arabi sisi, tutaziweka wapi nyuso zetu kwa kumtelekeza mgonjwa wetu wakati nafasi hiyo Mnyazi Mungu alitupa kuonesha huruma yetu na bado tukawa hatukufanya hivyo?
Misahafu inasema: "Heri walio na Huruma maana nao watahurumiwa" na pia "Heri wenye mioyo safi maana hao watamwona Mungu".
"Eeeh mola wetu hebu ukatujalie mioyo ya imani tukaweke tofauti zetu pembeni na kukubaliana kuwa suala la muhimu sana lilopo mbele yetu kwa sasa hivi ni kwa mheshimiwa huyu kupata huruma zetu wote kabisa na kwa umoja wetu na tukamtendee haki kuwa kuhakikisha pesa kuhusiana na tiba yake zipo bila ya kujali nani katoa nini (be it serikali, watu binafsi nk) kwani kutoa ni moyo na si utajiri."
Kimsingi lingekuwa ni jambo la faraja kubwa mno hata kwa mgonjwa wetu kwa serikali kuchukua jukumu kubwa zaidi katika kuhakikisha kuwa hakuna upungufu wa rasilimali katika tiba zake kulingana na madaktari wake huko aliko wanavyoshauri. Hii ni kama ambavyo serikali imekuwa ikifanya kwa wagonjwa wake kwenye hali tete kama hizi za kupigania maisha na hasa uwezekano wa full recovery unapokuwapo.
Baada ya utangulizi huu narejea katika hoja yangu ya leo:
Limekuwa jambo la kujiuliza hasa kuhusiana na kauli ya Mh. Jaji mkuu ya kutohitaji msaada wowote kwenye uchunguzi wa tukio la shambulizi la mh. Lissu.
Ninadhani hapa kinachogomba si msaada bali kuna hali ya kutoaminiana jambo ambalo haliwezi kuondoshwa kwa kukanusha tu kuwa fulani hakuhusika. Kwenye matukio tata kama haya kwa kawaida kumekuwa na matumizi ya chunguzi tofauti na zile za kawaida zilizozoeleka wanazofanya polisi. Serikali au vyombo vyake vinapotuhumiwa kuhusika hapo panakuwa na hali ya kutokuaminiana.
Kulikuwa na issue ya kuuwawa wachimba madini wa Ifakara ambapo kuliundwa na tume ya Jaji Kipenka. Kulikuwa na case za Richmond kulikuwa na tume iliundwa kuchunguza mambo ya Richmond nk nk. Yote haya yakiwa na nia njema ya kuhakikisha kuwa ukweli na ukweli peke yake unawekwa wazi pasipokuwa na pingamizi lolote. Ninaamini tume zote hizi zimekuwa na access ya resources zote ndani na nje ya nchi katika kuhakikisha kuwa ukweli unapatikana down to the ground.
Kwa nini serikali inaona ugumu kwenye kuhakikisha kama ilivyokuwa kwa wafanya biashara wa madini Ifakara, Richmond, au kama ilivyokuwa kwa case za kina Ouko na kina Saitoti Kenya sote kabisa pasipo na kujali tuko upande upi katika kadhia hili tunapata kujiridhisha ni nani kabisa na kwa nini walikuwa nyuma ya tukio hili ili wakatiwa adabu vilivyo bila kujali nyadhifa zao katika kuhakikisha matukio kama haya hayajitokezi tena?
Kwa maslahi ya nani tunaogopa au kupinga uchunguzi huru hata kama utahusisha agencies zozote za nje kutusaidia?
Mbona tunasaidiwa katika nyanja nyingi tu na hata katika kujenga "Fly Overs"?