msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 863
- 1,534
Kwenye tangazo la ajira kada ya afya na ualimu kigezo ni wahitimu waliomaliza kati ya 2012-2019.
Lakini leo bungeni waziri Ummy anasema wataajiri waliomaliza kati ya 2012 na 2015. Sasa kulikuwa na maana gani ya kuwambia waliomaliza kati ya 2016 hadi 2019 kuomba hizi ajira ikiwa kipaumbele ni wahitimu wa 2012?
Jambo lingine la kujiuliza, kipindi cha nyuma mh. Jakaya alikuwa akiajiri wahitimu kwa maelfu, sasa hawa wa 2012 wanatoka wapi au ni wale waliotumbuliwa kwa vyeti feki wanataka kurudishwa kivingine?
Mbona toka serikali ya awamu ya tano ianze kuajiri wahitimu wa miaka ya nyuma wamekuwa wakipewa kipaumbele . Je , wapo wengi kiasi gani kwamba wao hawaishi?