Kwanini Serikali inawambia watu ambao haiwezi kuwaajiri waombe nafasi za ajira?

Kwenye tangazo la ajira kada ya afya na ualimu kigezo ni wahitimu waliomaliza kati ya 2012-2019.

Lakini leo bungeni waziri Ummy anasema wataajiri waliomaliza kati ya 2012 na 2015. Sasa kulikuwa na maana gani ya kuwambia waliomaliza kati ya 2016 hadi 2019 kuomba hizi ajira ikiwa kipaumbele ni wahitimu wa 2012?

Jambo lingine la kujiuliza, kipindi cha nyuma mh. Jakaya alikuwa akiajiri wahitimu kwa maelfu, sasa hawa wa 2012 wanatoka wapi au ni wale waliotumbuliwa kwa vyeti feki wanataka kurudishwa kivingine?

Mbona toka serikali ya awamu ya tano ianze kuajiri wahitimu wa miaka ya nyuma wamekuwa wakipewa kipaumbele . Je , wapo wengi kiasi gani kwamba wao hawaishi?
Na kama walidhamiria kuwaajiri waliokuwa wanajitolea kwanini hawakwenda moja kwa moja kwenye mashule tena kwa siri wakachukua majina yao?
 
Ajira zikirudishwa halmashauri ndio majanga zaidi maana ili upate utategemea kuwa na kimojawapo kati ya hivi vitatu
1. Rushwa
2. Kujuana
3. Undugu

Ukikosa kimoja wapo kati ya hivyo utasota milele
Umesahau na kagawa K kwa dada zetu
 
Ajira zikirudishwa halmashauri ndio majanga zaidi maana ili upate utategemea kuwa na kimojawapo kati ya hivi vitatu
1. Rushwa
2. Kujuana
3. Undugu

Ukikosa kimoja wapo kati ya hivyo utasota milele
Sehemu yoyote ambayo kuna binadamu lazima kuwe na risk ya rushwa, kujuana na undugu. Mbona hata tume ya ajira bado wanalalamikiwa kwa hayo?
 
Nikadhani unaliza kwamba haiwezi kuwaajiri kwa kigezo cha wingi wao, lakini hata hapo ulipopagusia bado jibu langu ni lilelile iwapo ungeuliza kwa kigezo cha wingi.

Jibu langu mimi ni hili...
WANAMAKE MONEY. Yeah, wanaunda pesa serikalini kwa kutumia kundi hili lenye watu wengi zaidi nchini (katika maswala ya ajira).

Nakumbuka watu waliliwa hela ndefu tu walipoambiwa waandike maombi na watume kwa posta tena si posta tu bali kwa njia ya EMS lakini cheki kundi la waliotuma na ajira zilizokuja kutoka na vigezo walivyotumia

Kama lengo ilikuwa ni zile ajira elfu 6 kwanini wasiwachague tu (maana taarifa za ufaulu wao zote wanazo). Mtu atasema walifanya vile ili kujua nani yupo nani hayupo. Hoja hiyo inayeyuka kwasababu hata kila walipotoa majina kadhaa walitoa limit ya time katika kureport na ilipofika wakareplace nafasi. Kwa mantiki hiyo wangeweza tu kureplace watu kwa kadri ambavyo ingewezekana mpaka lengo litimie

Kama mtu atabisha abishe tu lakini ukweli ni kwamba wenzenu wanatamani (kama ingewezekana) hata leo hii watangaze kutotambua maombi hayo mtume maombi upya tena!
 
Kuanzia hiyo 2012 watu walipangiwa vituo kabla hata matokeo ya mwisho hayajatoka, ukiona hivyo wengi waliukimbia ualimu na kwenda private, Sasa huko mazingira sio rafiki tena wanaamua kurejesha majeshi.

Wazir ameweka wazi kabisa kuna watu waliripoti na wakala na mishahara kabisa na mpaka kukopa kwenye mabenki na wakakimbia, sasa hapa ndio anatakiwa kuwa makini kwenye hizo ajira kinyume chake anaenda kuajiri majambazi na wahujumu uchumi.
Sasa hao ndo walifanya makusudi wenyw kbs. Hao ata nafasi wasipewe maana wanawazibia wenzao rizki
 
Chini ya hapo kikwete alikuwa anaajiri wote , ni upumbavu Tu kumpa nafas ya pili mjinga wakat kuna watu kibao wanatamani hata hyo first chance.....!! Kama alidharau nafas ya kwanza hakuna haja ya kumpa nafas ya pili katika mazingira ambayo maelf ya vijana wanalilia ajira
Umeongea point nzuri kbs. Hao hawana nafasi ni kwasbb ya upumbavu wao. Wasiwazibie wenzao rizki
 
Kwenye tangazo la ajira kada ya afya na ualimu kigezo ni wahitimu waliomaliza kati ya 2012-2019.

Lakini leo bungeni waziri Ummy anasema wataajiri waliomaliza kati ya 2012 na 2015. Sasa kulikuwa na maana gani ya kuwambia waliomaliza kati ya 2016 hadi 2019 kuomba hizi ajira ikiwa kipaumbele ni wahitimu wa 2012?

Jambo lingine la kujiuliza, kipindi cha nyuma mh. Jakaya alikuwa akiajiri wahitimu kwa maelfu, sasa hawa wa 2012 wanatoka wapi au ni wale waliotumbuliwa kwa vyeti feki wanataka kurudishwa kivingine?

Mbona toka serikali ya awamu ya tano ianze kuajiri wahitimu wa miaka ya nyuma wamekuwa wakipewa kipaumbele . Je , wapo wengi kiasi gani kwamba wao hawaishi?
Yani sasa hivi ni full kuvurugana. NB; mwanangu hatokuja kua mtumwa wa ajira kama ninavyopambana baba ake sasa hivi...
 
Kuanzia hiyo 2012 watu walipangiwa vituo kabla hata matokeo ya mwisho hayajatoka, ukiona hivyo wengi waliukimbia ualimu na kwenda private, Sasa huko mazingira sio rafiki tena wanaamua kurejesha majeshi.

Wazir ameweka wazi kabisa kuna watu waliripoti na wakala na mishahara kabisa na mpaka kukopa kwenye mabenki na wakakimbia, sasa hapa ndio anatakiwa kuwa makini kwenye hizo ajira kinyume chake anaenda kuajiri majambazi na wahujumu uchumi.
Mfumo wa serikali mtu hawezi kuajiriwa mara mbili yaani hakuna check namba mbili Kwa mtu mmoja.
 
Chini ya hapo kikwete alikuwa anaajiri wote , ni upumbavu Tu kumpa nafas ya pili mjinga wakat kuna watu kibao wanatamani hata hyo first chance.....!! Kama alidharau nafas ya kwanza hakuna haja ya kumpa nafas ya pili katika mazingira ambayo maelf ya vijana wanalilia ajira
Upo sahihi sana mkuu maana haingilii akilini mtu uliyemwajiri akakimbia baadaye anarudi kuomba kazi ile ile. Sasa Mtu kama huyu ukimpa ajira unakuwa na uhakika gani kwamba hatakukimbia tena??
 
Hawa wa 2012 ni wale walianza private ili badae waingie serikalini sasa baada ya kuona upepo hautabiliki nao wanaomba waajiliwe na serikali
Halafu mbona kwenye tangazo la ajira la mwaka jana year interval ilikuwa wahitimu wa 2014-2019 iweje mwaka huu warudishe miaka nyuma hadi wa 2012 & 2013??. Kuna kitu hapa sio bure
 
Chini ya hapo kikwete alikuwa anaajiri wote , ni upumbavu Tu kumpa nafas ya pili mjinga wakat kuna watu kibao wanatamani hata hyo first chance.....!! Kama alidharau nafas ya kwanza hakuna haja ya kumpa nafas ya pili katika mazingira ambayo maelf ya vijana wanalilia ajira
Umemnena sahihi kaka,kama mtu hakuajiliwa kipindi cha JK huenda aliikimbia kazi hasahasa ya ualimu
 
Mfumo wa serikali mtu hawezi kuajiriwa mara mbili yaani hakuna check namba mbili Kwa mtu mmoja.
Hiyo mbona issue ndogo ya mtu kwenda mahakamani kula kiapo cha kubadili majina kazi inakuwa imeisha
 
Sehemu yoyote ambayo kuna binadamu lazima kuwe na risk ya rushwa, kujuana na undugu. Mbona hata tume ya ajira bado wanalalamikiwa kwa hayo?
Tume ya ajira ilikuwa ikilalamikiwa zamani lakini baada ya kuanzishwa kwa ajira portal sijasikia tena malalamiko kama hayo
 
Back
Top Bottom