DOKEZO Kwanini Serikali kupitia Wizara ya Nje, wasishirikiane na Wizara ya Nje ya Congo, kumkamata Tapeli alojiita Nabii kiboko ya wachawi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hujui kuwa hujui. Unajua kazi za wanadiplomasia? Kila wizara ina majukumu yake! Kazi ya Kukamata ni ya wizara ya mambo ya ndani. Fungua mashitaka uone INTERPO haifanyi kazi.
 
Itakuwa matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kwenda kuhangaika na mtu kama huyo , ila ni muhimu kuweka vizuri taratibu zetu ili kuzuia watu wa design kama hio kuingia hapa nchini kwetu tuichukue kama funzo la kujipanga vyema na vizuri zaidi, huyu sio tishio la kiusalama na hana madhara kwa mustakabali wa ustawi wa jamhuri ila tu atasumbua hisia za watu wachache kama wewe.
 
Mimi sijaona utapeli wa huyo jamaa bali nimeona ujinga wa watz.Wajinga ndio waliwao.Huu msemo unafanya kazi kwasehemu kubwa sana hapa bongolala.
 
SINGANO anakushinda huyu mkuu wetu?
 
Kwani huyo kiboko ya wqchawi alitumua dini gani?
mzungu alikuja na biblia
Muarabu alikuja na quran
Na wote walikuahidi mbingu,ukawaacha wakakutawala wakachukua mali yako na nguvu kazi yako wakaenda kujenga Mbingu huko kwao hapahapa duniani..
Kama kuna mbingu na waarabu wanaamini ya nini kujenga miji kama dubai na doha
Au kama mzungu anaamini mbingu ya nini kujilimbikizia mali
 
Ukikwapua mkoba wa mwanamke nchi Kama uk , utakimbizwa hadi na Helcopter, achilia mbali utapeli, futualia kesi ya Nabii Bushiri kule South Africa na ulinganishe na bandiko lako…
Hiyo ni UK sasa Tz ni ulimwengu mwingine, hao waliokua wanaenda kwake ndo wakuwakamata
 
Mtoa Mada ukimpleka huyu mtu mahakamani sijui utamshataki kwa kosa gani. Je sadaka ina risiti? Je kama ulipompa milioni zako au lakitano zako ulikubaliana nae nini? Je ilikua kukuombea au kukupaka mafuta au Maji ya upako? Je alifanya hivyo? Unaudhibitisho wa malipo uliyofanya? Ulilazimishwa? Je wewe kupata unafuu wa kilichokuwa kinakusumbua ni jukumu lake tu au ni pamoja na wewe kuuweka moyo wako tayari kupokea?

Kwenye kesi kama hii hakuna pa kutokea labda kama aliendesha kanisa bila usajili.

Watanzania tujifunze, haya mambo ya kurukaruka kwenye kila tunaloliona mbele yetu si busara. Tu mwombe sana Mungu atusaidie. Tangulini Uponyaji wa Mungu ukauzwa kama njugu? Tangulini utajiri ukapatikana bila kufanya kazi? Mungu anasema nitabariki kazi za mikono yako, pia anasema tutakula kwa Jasho, Je hizi kanuni zimebadilika?

Mungu atuongoze katika kujua njia iliyo kweli.
 


Hivi KOngo ina serikali kweli au ni matapeli pia?

Iko hivi:-
Utawala na uongozi ni kazi takatifu yenye heshima kubwa ya kumwakilisha Mungu.

Ujaji na uhakimu ni kazi takatifu inayomwakilisha Mungu kutoa haki na hukumu.
Jeshi na wale Watumishi wa Mungu (wanaoitwa viongozi wa dini) ni kazi takatifu inayomwakilish Mungu kaika kulinda watu kiroho na kimwili.
mSasa kama una nchi yeny e watawala /viongozi ,majaji ,masheje/wachungaji /manabii/maaskofu na wakuu wa majeshi wasio na hofu ya Mungu basi hili ni taifa lililojikabidhi kwa shetani na yote yanayofanyika ni ya kitapeli na kuwaumiza watu kama mateka na watumwa wao . Angalia hata hao niliowataja wanajipatia na kujilipa mapesa mengi sana na kwenda kufanya starehe huku wakiwa wanawaona watu wao ni wajinga sasio na lolote la kuwafanya.

Kuna waziri aliwahi kusema kuwa Mwanaume gani anaandika jina kwenye kadi ya gari kama IST. Mwingine akasema gari kama IST ni kwa ajili ya kuhonga mwanamke kama soda tu na chips.
Mwingine akasema nyie Watanzania mnalalamikia nchi kukopa kwani hizo pesa mtakuja kugongewa milango yenu ili mlipe.
Mkiona maisha ni magumu hamieni Burundi, Mwingine tena mkabubwa akasema mnahoji hoji kwa sababu ya roho mbaya na wivu tafuteni hela sio kufuatilia maisha ya watu .

Mwingine mnaandamana tutawapiga kipigo cha mbwa koko.
Mwingine "mnawalealea hawa wanatakiwa kupigwa tu."
Mwingine "wakiwakosoa viongozi nyookeni nao"
Wengine nyie watu wa giza wenzetu msiwatafute wanaopotea kwani tumewapoteza sisi .
Wengine "kura zenu ni vikaratasi tu hatuwezi kukabidhi nchi kwa mtakaowachagua nyie"
Wengine ,"Katiba ya nchi ni kijitabu tu "

Wengine "achaneni naye huyo amejitaka na kujipiga risasi mwenyewe.

Wengine "Mpende msipende bandari itauzwa" na leo viongozi wa dini waliopinga leo wamekuja kunywa chai ikulu kushuhudia utiaji saini."

Wengine "wamasaidi wahamishwe tu kwa sababu sio watanzania ni wakenya"

Hizo zote ni kauli za watu walioshiba pesa za dhulma na utapeli na rushwa na ufisadi. Na ni watu wanaotumia ujinga ,woga,ukarimu,shida na njaa za Watanganyila kujipatia mapesa mengi sana.


wzHiyo ni UK sasa Tz ni waulimwengu mwingine, hao waliokua wanaenda kwake ndo wakuwakamata
 
Kwakweli bila waumini wake kucharazwa viboko kwanza Tena hadharani sioni sababu ya huyo kiboko ya wachawi kukamatwa.
 
Mnamkamataje mliyemfukuza? Halafu kwani amefanya kosa gani? Shughuli zake si ziliharalishwa na mamlaka husika? Tangu lini imeanza kuwa kosa kuwaibia watanzania au kuwageuza mazombi?
 
Serikali haiwezi ikaingilia upuuzi, wakristo acha mtapeliwe tu mpk mtie akili kondoo nyie, mkiambiwa kweli mnakimbilia kumshambulia anayewasanua hata kama ana nia nzuri mtamuita kobazi, acha mpigwe pesa tu makondoo nyie
Sawa bwana kobazz
 
Mimi nimefurahi sana na nmemuunga mkono kiboko wa wachawi hakika uliifanya kazi yako vzr.
Watanzania wengi ni wapumbavu hasa linapokuja suala la dini, hvy nafurahi sana mnaponyooshwa.
Na bado kuna matapeli wengine waliopo humu nchini na wao wanasubiri wapigwe na kitu kivito ili waamke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…