Wakusoma 12
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 5,503
- 15,858
Sijajua kuhusu awamu ya kwanza lakini awamu ya pili ya rais Mwinyi, awamu ya tatu ya Mkapa na awamu ya nne ya Jakaya Kikwete ziliundwa tume za kutosha ili kujibu na kutolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya kijamii na mengine kuyaondoa katika utekelezaji ikiwa jamii ilionekana kutoyaunga mkono.
Lakini pia awamu ya tano japo ilikuwa na mambo mengi ya giza lakini pia ilikuwa inasikia maoni ya wananchi kama wakiona jambo linapingwa ilikuwa inarudi nyuma na kujiosha. Awamu ya sita imekiuka ile kauli ya mamlaka yote hutoka kwa watu, imefanya mambo kwa kiburi hata kama mambo hayo jamii imeyakataa na hili ni suala la kuogopwa sana.
Moja kati ya mambo hayo ni hili la kuhamisha Wamasai, kubinafsisha bandari na kutesa upinzani. Ni nani aliye nyuma ya haya? Moja kati ya vitu inavyoweza awamu hizi ni pamoja na kulazimisha mambo yasiyo na baraka kwa wananchi mfano Uundwaji wa tume ya uchaguzi isiyo na baraka za wananchi wala vyama vyote vya siasa