Pre GE2025 Kwanini Serikali ya Rais Samia imeruhusu maandamano ya CHADEMA?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Katika dunia ya leo, siasa za maandamano ni siasa za kijinga. Ni u-harakati usikuwa na effect yoyote kisiasa. Ni afadhali kuwe na spontaneous maandamano ya wananchi wa itikadi mbalimbali kuliko hayo ya kuandaliwa na chama kimoja cha upinzani.
 
Missile of the Nation umeanza uchambuzi vizuri ila badala ya kujadili hoja na matarajio ya maandamano, ukajikita kueleza sababu za kuyaruhusu maandamano.

Hoja ya kwanza ya maandamano ambayo ni sheria mbovu, umedai kwamba haina mashiko; sawa!

Lakini hukuchambua hoja ya pili ya maandamano ambayo ni ugumu wa maisha.

Je, huoni kwamba hoja ya pili ni pana sana inayogusa Watanzania wengi, na inaweza kumeza hata hoja ya kwanza?

Hivi leo ukiwaambia Watanzania ugumu wa maisha unadhani kati ya raia 10, ni wangapi watakuambia ni magumu kama siyo 9 kati ya 10?
 
Unamaanisha kuwa CHADEMA wanataka mabadiliko ya katiba ta sasa?

Siyo kutaka katiba mpya?
 
Kitendo cha kukubaliwa kuandamana kimewakata chadema maini.
Kwanza imetumika protoko kubwa sana kichama (ccm)
Mpaka hapo chadema ile nguvu hawana tena ni kama wanasindikiza mwenge.
Kwanza wanaandamana ujumbe wanaupeleka wapi
 
Katiba mpya ni muarubaini wa mambo mengi.
 
Kitendo cha kukubaliwa kuandamana kimewakata chadema maini.
Kwanza imetumika protoko kubwa sana kichama (ccm)
Mpaka hapo chadema ile nguvu hawana tena ni kama wanasindikiza mwenge.
Kwanza wanaandamana ujumbe wanaupeleka wapi
Wanaenda UN badala ya kwenda Ikulu.

Sijui UN itasaidia nini kwa kudai "maisha yamekuwa magumu"
 
Siasa za Tanzania sio precision politics kama za wenzetu. Maandamano yenye impact yanapaswa kuishinikiza serikali ifanye mabadiliko. Kwa haya ya kesho hayatakuwa na nguvu isipokuwa tu a practice of democracy kwa pande mbili. Iwapo wapinzani watarudia maandamano hayo say every month yanaweza kuwa na impact lakini serikali haitaruhusu. Lakini hakuna shida tuanzie hapo.
 
Una hoja ya msingi sana.

Tangu Mbowe akutane na viongozi wa Ccm baada ya kuachiwa huru, ajenda ya katiba mpya ilishazikwa kitambo.

Huenda Ccm wameruhusu haya maandamano ili pia kumpunguzia Mbowe shinikizo la wapinzani wake ndani ya Chadema ili aonekana bado ana amshaamsha.

Kiufupi sera za Mbowe kuelekea kudai katiba mpya ndicho Ccm wanachokitaka, huenda ndicho walichokubaliana kwenye yale mazungumzo ya maridhiano.

JokaKuu econonist zitto junior Nguruvi3 brazaj Rabbon

Tindo
 
Kuna jambo hamlioni hapo,

Hiyo agenda ya Tume HURU ya UCHAGUZI ambayo inamuondoa Rais kuteua Election commissionals inataka uje muswada wa Mabadiliko ya SHERIA mama kwanza ambayo ni Katiba iliyopo ibadilishwe kuruhusu kumuondolea Rais mamlaka ya kuteua wajumbe wa kusimama uchaguzi.

Neno Tume HURU, maana yake lazima uguse Katiba na kubadili Ili kumuondoa Rais kuingilia TUME.

Kwa maana ingine, KATIBA iliyopo itatiwa kiraka kipya Ili kupata Tume HURU iliyopendekezwa kwenye Rasimu ya Warioba.

Tunaelekea pazuri sana.
 
..wamewaogopa MABALOZI.

..Na Maza kaalikwa Vatican hawezi kwenda kule akiwa na damu za Watanzania.
 
..kuruhusu maandamano.

..hajaruhusu mabadiliko madogo ya katiba yatakayomuengua kuteua tume ya uchaguzi.
 
Mkuu tunahitaji katiba mpya, kujaza viraka kwenye nguo Chakavu ni sawa sawa na kuiharibu zaidi.

Kiufupi Ccm wamefanikiwa kuzima vuguvugu la katiba mpya kwa kutumia mabavu ya dola, kutumia wapinzani mamluki na kumtumia Mbowe.
 
..kuruhusu maandamano.

..hajaruhusu mabadiliko madogo ya katiba yatakayomuengua kuteua tume ya uchaguzi.
Kuruhusu maandamano ni kuruhusu HOJA za CDM zisikike na Watawala,

Jambo ambalo bungeni walikuwa hawaruhusuwi hata kuongea.

Wingi wa waandamanaji, utalazimisha miswada IRUDISHWE na kupata mabadiliko wananchi wayatakayo.
 
..wamewaogopa MABALOZI.

..Na Maza kaalikwa Vatican hawezi kwenda kule akiwa na damu za Watanzania.
Ila mkuu unakubali haya maandamano hayana jipya cha kuitisha Ccm, maana wameshapata walichokitaka yaani kuua vuguvugu la katiba mpya tena walizawadiwa na Mbowe
 
Mkuu tunahitaji katiba mpya, kujaza viraka kwenye nguo Chakavu ni sawa sawa na kuiharibu zaidi.

Kiufupi Ccm wamefanikiwa kuzima vuguvugu la katiba mpya kwa kutumia mabavu ya dola, kutumia wapinzani mamluki na kumtumia Mbowe.
No unakosea.

Maandamano ndiyo yataibua HOJA zote ikiwamo whether tuingie uchaguzi Kwa kubadili baadhi ya vipengele au kusubiri tupate Katiba mpya ndipo uchaguzi ufuate.

Jambo muhimu hapo, Andika bango lako lisemalo,

"BILA KATIBA MPYA, HAUTAFANYIKA UCHAGUZI WOWOTE WA HAKI"

Hakuna atakayezuia ujumbe wako kusikika.

Alika na majirani wajitokeze Kwa wingi katika maandamano.
 
Mkuu tunahitaji katiba mpya, kujaza viraka kwenye nguo Chakavu ni sawa sawa na kuiharibu zaidi.

Kiufupi Ccm wamefanikiwa kuzima vuguvugu la katiba mpya kwa kutumia mabavu ya dola, kutumia wapinzani mamluki na kumtumia Mbowe.

..vuguvugu si hayo maandamano na mikutano ya hadhara? Au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…